Mamlaka ya mawasilanao Tanzania imeshauriwa kuhakikisha
vituo vyote vya Runinga vya Tanzania vinaonekana Bure katika mfumo wa digitali
kupitia katika ving’amuzi vinavyouzwa kwa watanzania
Rai hiyo imetolewa na George Nangale mkurugenzi wa TV Sibuka
na Radio Sibuka wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya waziri wa
mawasiliano, sayansi na teknolojia prof. Makame Mbalawa (MB) na mkurugenzi wa TCRA Prof. John Nkoma kutangaza kuwepo kwa vituo 5 vya TV ambavyo
vitaonekana bure baada yakuzima mitambo ya analogia
Nangale amesisitiza kuwa, kwa sasa TCRA ina Urasimuu ambao
umekwamisha vituo vingine tofauti na TBC, ITV, Channel ten, Star TV na EATV
kuonekana bure kupitia ving’amuzi vya digitali
Aidha amesisitiza kuwepo na mkakati mahususi wa kuhakikisha
elimu zaidi inapelekwa vijijini ili watanzania wote waufahamu mfumo huo mpya wa
matangazo ili pia iwasaidie kujipanga kifikra na kiuchumi kununua ving’amuzi
vya digitali,
Bw. Nangale amekiri kuwa kwa sasa bado watanzania wengi
hawana ufahamu wa kutosha kuhusu uhamisho huo wa analogia kwenda digitali
katika mfumo wa matangazo ya Runinga na Radio nchini Tanzania
Baadhi ya vituo ambavyo havimo katika mpango huo wa
kuonekana bure ni pamoja na Sibuka, Mlimani TV, Clouds TV, na TV Imani
No comments:
Post a Comment