Muungano wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania umetoa vifaa vya kazi (vitendea kazi) vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 35 kwa kila klabu ya wanahabari kwa lengo la kuboresha utendaji kazi, weledi na kujenga uchumi wa vilabu hivyo
Akikabidhi vifaa hivyo kwa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Kigoma, vifaa ambavyo ni pamoja na kamera, computer, runinga na zana za kisasa za mikutano na semina (projector), Rais wa UTPC Bw. Kenny Simbaya amehimiza utunzaji wa zana hizo pamoja na nidhamu ya matumizi

Bw. Simbaya ameeleza kuwa zana hizo ni matokeo ya utekelezaji wa mradi wa kuimarisha Press Club nchini, mpango ambao umefadhiliwa na mradi wa maendeleo wa Ubalozi wa Sweeden Tanzania

Tanzania ina jumla ya Vilabu vya waandishi wa habari 23 hadi sasa na upo uwezekano wa kuongezeka kufuatia serikali kuongeza idadi ya mikoa nchini
No comments:
Post a Comment