Baada ya kubaini na hatimae kukiri kuwa idara za serikali za
mitaa zinanuka kwa rushwa nchini Tanzania Taasisi ya kuzuia na kupambana na
rusha nchini TAKUKURU imeanza kutoa mafunzo kwa kamati za maadilii za
halmashauri za wilaya, manispaa, miji na majiji nchini
Mkoani Kigoma mafunzo hayo yameanza jana yakihusisha kamati
za maadili kutoka miko aya Kigoma, Kagera na Shinyanga ambapo zaidi ya
washiriki 30 wamehudhuria mafunzo maalumu ya mkakati wa pili wa kupambana na Rushwa
NASCAP II
Jumla ya halmashauri kumi na moja (11) zimetuma wawakilishi
kushiriki mafunzo hayo
Cha kujiuliza ni je, kamati hizi za maadili zina nguvu gani
ya kisheria ya kudhibiti vitendo vya rushwa miongoni mwa watumishi wa serikali
za mitaa ambao wanatajwa kujilimbikizia mali kuliko hata kiwango vha mishahara
yao na umri katika utumishi?
Je ni nani mteuzi wa kamati hizi ambazo miongoni mwa wajumbe
wake nao ni watuhumiwa wa vitendo vya uvunjifu wa maadili, uzembe kazini na Rushwa?
Je! Kanuni ya uhakiki wa mali za watumishi ambayo imekuwa
ikiwaandama wabunge na mawaziri, huku chini inatumika kudhibiti utajiri wa
ghafla mara tu mtu anapopata ajira au uwakilishi wa wananchi katika halmashauri
za wilaya, miji, manspaa na Jiji?
Hebu tuchangie hoja hii,
“kwa kuwapa mafunzo wajumbe wakamati za maadili za
halmashauri, TAKUKURU itafanikiwa kudhibiti Ruswa katika ofisi za utoaji wa
huduma kwa wananchi hususani idara ya Mipango, Utumishi, Ugavi, fedha na Afya? “
Tuma maoni yako kupitia srfm2011@gmail.com
au tuma maoni yako kwenye kisanduku cha maoni chini ya habari hii, pia unaweza
kupiga simu namba 0786200518 au 0763837396
UNAO UHURU WA KUSEMA CHOCHOTE NASI TUTAPEPERUSHA MAONI YAKO
KWA UMAKINI
STANDARD RADIO FM
SAUTI YA WASIO SIKIKA
1 comment:
Mie naona hiyo siyo dawa, Rushwa ni moyo wa mtu, kwani hao wajumbe wao ni salama? sina hakika
Post a Comment