Saturday, November 24, 2012

JACKTON MANYERERE NA HUKUMU YA KIFO


Jackton Manyerere Mwanahabari mwandamizi na Mhariri wa gazeti la JAMHURI

Wiki hii Blog hii iliweka taarifa ya msimamo na maelezo ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon kuhusu hukumu ya kifo, habari hiyo imesomwa na watu wengi ndan na nje ya afrika na wengi wamekuwa na hoja nyingi kuhusu hukumu ya kifo. haya hapa chini ni maoni ya Ndg MANYERERE
 

Hawa jamaa wa UN wasitake kutuchezea akili. Adhabu ya kifo ni mbaya, sawa; lakini inastahili. Nimepata kumhoji Jaji Samatta juu ya adhabu hiyo, yeye anaiunga mkono.

 

Hoja yake ni kwamba kuna kesi ukiisikiliza, ukajua namna mhusika alivyoshiriki kumuua binadamu mwenzake, kama kweli ni Jaji mtenda haki, atamhukumu adhabu ya kifo.

 

Juzi hapa wanajeshi wamehukumiwa kifo kwa kumuua Swetu. Hawa watu ukiwakuta mitaani wanavyoadhibu binadamu wengine hadi kuwaua, hakika huwezi kuwaonea huruma nao wanapohukumiwa.

Fikiria, majambazi wanaingia nyumbani kwako na kuiua familia yako, kisha wanaambulia kuchukua sh laki moja, au kuku, au mbuzi. Katika mazingira kama hayo, wahusika wakipatikana hakuna adhabu sahihi kwao zaidi ya kunyongwa, tena si kunyongwa tu, bali kunyongwa hadi kufa.

Kama kweli UN wanaona adhabu hii haifai, basi waanze na wafadhili wao wakuu, "mabwana" wa demokrasia-Marekani ili nao waache kufanya hivyo. Saddam Husseina alinyongwa, Gaddafi kauawa na wakala wao Wamarekani na Wafaransa; iweje kuwaua hawa iwe halali, lakini sisi kuwanyonga wanaowanyonga ndugu zetu iwe si haki?

Afrika Kusini walijipendekeza kufuta adhabu hiyo kwa busara zas Jaji Mwalusanya wa Tanzania. Sasa wanajuta! Wanataka adhabu ya kifo irejeshwe maana ushenzi umepindukia nchini humo.


Tuache kuimba wimbo wa UN pamoja na asasi za kiraia ambazo kazi yake ni kusaka fedha. Adhabu ya kifo inawafaa sana wale wanaoistahili. Haki ya kuishi isiwe kwa muuaji tu, bali tutazame na yule aliyeuawa anatendewa haki vipi!


Manyerere

Nawasilisha

 

No comments: