Na Edilitruda Chami
Askofu wa kanisa katoliki jimbo la Shinyanga Mhashamu
Aloysious Balina amefariki dunia jana majira ya saa 5 asubuhi katika hospitali
ya Bugando mkoani Mwanza alikokuwa akitibiwa kwa muda mrefu.
Marehemu Askofu Balina
alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani kwa muda mrefu
hadi mauti yalipomkuta. Alizaliwa Julai
21, mwaka 1945 na amefariki akiwa anamtumikia Mungu Kwa miaka 45 ya upandre na
miaka 27 ya uaskofu.
Mwili wa marehemu utazikwa katika kanisa la mama Maria
mfanyakazi - Ngokolo mkoani Shinyanga siku ya jumamosi saa nne asubuhi.{MUNGU
AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMINA}
No comments:
Post a Comment