Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar na
katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad leo anaanza ziara mkoani Kigoma
akifuatana na mwenyekiti wake wa taifa Ibrahim Haruna Lipumba
Akiwa mkoani Kigoma atafanya mikutano
kadhaa ya hadhara ambapo leo atakuwa mjini Kasulu kuhutubia wananchi katika
uwanja wa maengesho ya magari mjini hapa.
Uwanja huo unatumiwa na makamu huyo wa
rais siku chache baada ya kamati ya ulinzi na usalama wilayani Kasulu kupiga
marufuku matumizi ya eneo hilo lililopo katikati ya soko kuu kwa shughuli za
mikutano ya kisiasa kwa hofu za kiusalama
Hadi sasa viongozi wa wilaya ya Kasulu
na mkoa wa Kigoma wa Chama cha Wananchi CUF hawajasema maudhui ya ujio wa
viongozi wao wa kitaifa mkoani Kigoma
Hata hivyo tetesi zinadai kuwa ziara
hiyo ni sehemu ya kuvunja nguvu za Chama cha Demokrasia na Maendeleo pamoja an
NCCR mageuzi mkoani humo
Mkoa wa Kigoma kwa sehemu kubwa wabunge
wake wanatokana na vyama vya upinzani ambapo NCCR ina wabunge wane (4) Chadema
mmoja (1) na CCM wabunge watatu (3)
Ziara hiy ya Maalim Seif na Lipumba
inakuja pia siku chache baada ya Baba wa Upinzani mkoani Kigoma Dr. Aman Kaburu
aliyekuwa kiongozi wa juu wa CHADEMA nchini aliyehamia CCM na kuwa mbunge wa
Afrika mashariki, kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa
Kigoma
No comments:
Post a Comment