Na,
Doris Meghji Jumatatu
Singida
Uzidishaji
wa uzito wa mizigo kwenye magari barabarani,Uwizi wa alama za barabarani,
umwagaji oili, Mafuta ya dizeli na Petroli kwenye barabara za lami ni miongoni
mwa changamoto zinazoikabili sekta barabara nchini kutodumu kwa
muda mrefu wakati serikali inatumia fedha nyingi katika ujenzi wa barabara hizo
nchini
Changamoto
hizo zimetolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
DKT.Jakaya Mrisho Kikwete katika ziara ya kikazi ya siku mbili
mkoani singida kwenye uzinduzi wa kukamilika kwa
barabara ya Mayoni Issuna mkoani Singida yenye urefu
wa kilomita 54 kwa fedha za serikali ya Tanzania kwa gharama ya shilling billion
32 kwa kiwango cha lami yenye kuuganinisha Manyoni na mkoa wa Singida kwa
barabara ya lami kuwataka wananchi kutuza barabara hizo ili ziweze kudumu kwa
muda mrefu kwa kuwa ndio mishipa ya damu ya uchumi na maendeleo ya wananchi wa
Tanzania.
Dkt.
Kikwete amesema kukamilika kwa barabra hiyo kumeondolea aibu kwa nchi ya
Tanzania kwa watanzania wa wanaokwenda mikoa ya Mwanza na Kagera kulazimika
kupita nchi jirani ili kuweza kufika katika mikoa na kipande hicho cha manyoni
Isuna kuwa kipande korofi kwa magari kukwama kwa kukwamisha maendeleo ya chni
yetu
Naye
Dkt John Pombe Magufuli waziri wa ujenzi amesema kukamilka kwa barabara hiyo ni
ukombozi mkubwa kwa uchumi wa wananchi wa wilaya ya manyoni na mkoa wa singida
kwa ujumla kwa kuwa sasa magari mengi kupita hapo kwa kufanya biashara zao
kwenye magari yanayokwenda nchi jirani za Rwanda,
Burundi na Uganda kupita katika barabara hiyo mkoani Singida.
Aidha
Dr. Magufuli amewataka wananchi kuzingatia sheria namba sita ya barabara kwa
kuwa hifadhi ya barabara ni mita 30 na wale waliokwisha lipwa fiadia na kurudi
kujenga katika eneo la hifadhi ya barabara kubomolewa nyumba zao bila kulipwa
fidia yeyete katika kipande cha kilomita nne kinachoingia mjini
Manyoni.
Mkoa
wa singida una jumla kilomita 1998 za mtandao wa barabara kati ya kilomita hizo
kilomita 357 zimejengwa kwa kiwango cha lami katika ndani cha kipindi cha miaka
saba.
No comments:
Post a Comment