Na Phesthow
Sanga
Walemavu wa ngozi [ALBINO}
Mkoani Singida Wameshauriwa
Kujitambua na Kukubali hali
Waliyonayo, kuwa ni
sawa na Watu
Wengine Wenye Ngozi
Nyeusi kote duniani.
Wito huo umetolewa na Ofisa
Ustawi wa Jamii Emanuely
Mramba kwa niaba
ya Mkuu wa Wilaya ya Iramba Yahya
Nawanda, katika Mdahalo
wa chama cha maalbino Mkoa wa Singida ,watumishi wa
Serikali, Viongozi wa Dini na Wadau Wengine uliofanyika
katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya
ya Iramba.
Akisoma
Risala kwa Mgeni rasmi
katibu wa Albino Mkoa wa Singida Mwanahamisi
Msembo, alisema kuwa chama cha Albino
Mkoa wa Singida kilianzishwa
Septemba mwaka 1991 na aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho marehemu Hamisi
maimu kukiwa na albino 15 tu.
Mwanahamisi alijuza
kuwa mpaka sasa
Mkoa wa Singida
Unawana chama 338 waliosajiliwa na waliosambaa katika wilaya zote nne za mkoa wa Singida.
Aidha Mdahalo huo, ulikuwa Unahoji kuhusu Ushirikishwaji wa
watu wenye Ualbino katika
shughuli za kimaendeleo
ngazi za wilaya
mkoani singida,ki-afya ,elimu ,pamoja na Ulinzi na Usalama katika maeneo yote walipo albino kutokanan na
vitisho na changamoto zote zinazowakabili.
Akijibu hoja
za Afya kaimu mganga mkuu wa hospitali ya wilaya Dr.JabirJuma alisema kuwa hospitali yake
Imeweka mikakati dhabiti ya kupata daktari pamoja na kilniki ya watu wa Ulemavu wa ngonzi
katika wilaya ya
Iramba kwa muda mfupi ujao .
Hata hivyo
kwa upande wa Elimu ofisa elimu maalum
Iramba Bw. Mathew Njoghomi
aliwaeleza wanamdahalo kuwa
Idara yake inatoa
Elimu kwa walemavu wa ngozi {Albino} katika shule ya Kizega sawa na watoto wengine
pia wanapewa Ulinzi
wakutosha wakati wote kutoka kwa jeshi
la Polisi pamoja na Jamii
No comments:
Post a Comment