NA Phesthow sanga
Shirika lisilo la kiserikali {SIKIKA] ambalo ofisi
yake kuu ipo
Dodoma na ambalo linajihusisha
na mambo ya wizara
ya Afya nchini
hivi majuzi limemaliza kazi zake
za Ufuatiliaji wa Uwajibikaji
jamii, katika Uwajibikaji wa Watoa huduma
na wenye Mamlaka
katika kuhakikisha haki
za Binadamu na jamii Zinapatikana .
Timu hiyo
ambayo iliundwa na wajumbe
waliochaguliwa katika makundi
mbali mbali ya jamii,wakiwepo pia madiwani
wa kamati ya
Huduma za jamii pamoja na Viongozi
wa
Dini na Madhehebu yaliyopo
katika wiliaya
ya Iramba walianza
kazi tangu
Okt 25 na kumaliza nov 24 mwaka huu.
Akiongea na Wanahabari,
Mkuu wa Ofisi ya Sikika Dodoma bw. Patrick N.Kinemo ,Amesema kuwa
shirika hilo katika miaka yake
kumi tangu lianzishwe
limejikita Na mambo
ya Wizara ya Afya ikwemo kufuatilia
mambo ya madawa, Raslimali Watu ,vifaa Na
Mambo yote yanayohusu
wizara ya Afya
kwa Ujumla .
Akizitaja kero na
mapungufu pamoja na
mambo mengine yaliyoibuliwa wakati
timu ya {PSAM} Ilipokuwa
ikitembelea zahanati Na Vituo
vya Afya katika
wilaya ya Iramba Ni Pamoja
na Akina mama Wajawazito kutozwa gharama
za Kadi za
klinik iwapo mama huyo
atakuwa
amepoteza kadi yake .
Hali hiyo ilkutwa
katika Kituo cha Afya cha
Mgongo ambapo Wananchi
walitoa malalalmiko yao
kuwa wanalipizwa tshs. Elfu Tano kwa mjamzito
kama kapoteza
kadi yake , pia malalamiko kama hayo
yalitolewa na wananchi
katika Zahanati ya
Shelui kuwa wajawazito
hulipizwa shilingi Elfu mbili kama amepoteza
kadi yake huku katika
kituo cha Afya
cha Ndago Akina mama hulipizwa tshs Elfu moja kwa
upotevu wa kadi.
Mambo Mengine
ni Upungufu mkubwa
wa Watumishi , Uchakavu wa
Majengo , magari katika Vituo
vya Afya , Madawa , Vifaa
Tiba, Ulinzi , Usimamizi wa Fedha ,matibabu ya Wazee
mizani za watoto katika Zahanati nyingi , Semina kwa
watoa Huduma.
Aidha Timu ya
public service accountability monitoring {PSAM} Imegundua madawa
ya thamani ya tshs
.1,342,400.yameharibika na kutofaa tena
katika matumizi ya
Binadamu bado Hayaja teketezwa
na kuchomwa kama ilivyoagizwa
na amri {order} no.244
ya mwaka 1997 na hakuna
hatua zozote
Zilizochukuilwa na Uongozi wa
Halmashauri hiyo.
Kutokana na taarifa
ya Timu ya
PSAM, Iligundua pia
Akiba kubwa ya Vyandarua katika
stoo ya hospitali ya
wilaya Neti ambazo
hazijagawiwa ;4811 ambazo
zilitolewa na MEDA , Tangu Januari 2011; na uongozi
wa Halmashauri upo na hakuna hatua yoyote ilyochukuliwa kuhusiana
na vyandarua hivyo .
Akijibu na
kutolea Ufafanuzi kuhusu
Taarifa Iliyotolewa na Timu
ya psam Kaimu Mganga Mkuu wa
Wilaya
Dr. Mbulu alieleza kuwa katika mambo yote
yaliyosemwa yanatekelezwa kulingana
na bajeti ,aidha alikiri
kuwa mambo Mengine Watayafuatilia ,kama Utozwaji wa kadi
za klinik kwa
akina Mama wajawazito
No comments:
Post a Comment