Tuesday, November 20, 2012

WATANZANIA ACHENI MALALAMIKO, TIMIZENI WAJIBU WENU

     
Na  Phesthow  Sanga 
      Iramba

Wananchi Wilayani Iramba  Mkoani Singida Wameshauriwa Kuacha Kulalamika Barabarani  na Mitaani  Kuhusu Matatizo Mbalimbali Badala  Yake Waende Ofisini Kwa Wahusika  Kutoa  Malalamiko na Duku-duku  zao.

Ushauri Huo  Ulitolewa  Jana  na Mjumbe  Wa Halmashauri Kuu ya Taifa {NEC}Wilaya  ya Iramba  Juma  Hassan Killimbah Kwenye  Mkutano wa  Hadhara  Uliofanyika  katika  Uwanja  wa Ofisi ya CCM. Wilayani  hapo.

Killimbah  aliwaeleza  Wananchi Kuwa  Tabia ya Kulalamikia  Matatizo fulani Mitaani  Siyo  ya Kistaarabu,”huo mara  nyingi  huwa  ni unafiki mkurugenzi yupo ,DC yupo maofisa  Elimu wapo  wahandisi wa maji  na ujenzi  nao wapo pamoja  na maneja  wa Tanesco yupo pelekeni malalamiko yenu mahali  husika.”alisisitiza  killimbah.

Wananchi hao wamekuwa  wakilalamikia juu ya mbolea ya Ruzuku  kutoka  Serikalini  pamoja na mbegu kuwa zinauzwa  kwa bei  ya juu  hivyo walitaka  kufahamu  bei ya Serikali ni  ipi, kutofautisha na ya wazabuni waliopewa tenda hizo wilayani hapo.

No comments: