Sinida
WAISLAMU nchini
Tanzania, wametakiwa kuongeza kasi zaidi kujikita kumuabudu mungu, ili pamoja na mambo
mengine, wasitumiwe ovyo kwenye mambo yasiyokuwa na tija yakiwemo ya maandamano
na vurugu.
Hayo yamesemwa
na mbunge wa viti maalumu (CCM) mkoani Singida, Martha Mlata,
wakati akizungumza kwenye hafla ya harambee ya kuchangia kumalizia ujenzi wa
msikiti wa Almasijidi Muhidini Baytulah, wa kitongoji cha Mbuyuni Senene kijiji
cha Iguguno, wilayani Mkalama.
Alisema baadhi ya
waislamu wamekuwa wakirubuniwa na baadhi ya wanasiasa kuchochea vurugu na
wamesahau kuwa wako hapa duniani ili kumuabudu mungu wao na kuwa maisha ya sasa
ni magumu hivyo wafanye kazi kwa bidii ili kwa hali hiyo watakuwa wamejijengea
mazingira mazuri ya kumudu maisha yao, lakini pia watakuwa na uwezo mpana wa
kutambua mema na mabaya.
Mlata alisema kundi
kubwa la baadhi ya waislamu hao ni vijana hivyo wakifanya hivyo hawataweza
kutumikishwa ovyo ikiwemo kuandamana kwa manufaa ya watu binafsi wanaojitafutia
umaarufu, ukiwemo wa kisiasa.
Katika hatu
anyingine, mbunge huyo alisema kuwa amani na upendo vinapaswa kuanzia katika
ngazi ya kila kaya.
“Kama kwenye familia
zetu, hakutakuwepo na amani, upendo na utulivu, basi taifa letu linaweza
kuyumba katika juhudi zake za kudumisha amani na utulivu uliopo ambao umedumu
kwa muda mrefu sasa”,alifafanua.
Akifafanua
zaidi,mbuge huyo,alisema amani na utulivu, vitaendelea kulindwa na kuimarishwa
tu, endapo wakazi wa mkoa wa Singida na Watanzania kwa ujumla, watatumia
miskiti na makanisa, kumwabudu Mugu kwa uadilifu mkubwa.
Aidha, Mlata alitumia
fursa hiyo kuwaasa wazazi walezi kuendelea kuwalea watoto wao katika maadili
mema na kuwahimiza watumie nyumba za ibada kwa ajili ya kuwabudu Mungu wao.
Awali Imam wa
msikiti wa Nuru Salama Unyankindi Sindia mjini, Yahaya Mahiki, alitumia fursa
hiyo kuwataka vijana wa kiislamu na wasio waislamu, kutafuta elimu kwa nguvu
zao zote.
Alisema dunia ya
sasa, bila elimu ya kutosha, maisha bora kwa kila mtanzania, yatabaki kuwa
ndoto.
“Bila kuwa na elimu
ya kukidhi mahitaji, wewe kijana utakuwa kama bendera ambayo kazi yake ni
kufuata mwelekeo wa upepo. Nenda kwenye maandamano yanayofanyika hivi sasa,
utakuwa waandamaji karibu wote ni vijana. Wanashiriki maandamano bila kujua
faida zake wala madhara yake”,alisema Mahiki.
Akifafanua zaidi,
alisema wanashiriki maandamano kwa vile hawana elimu ya kutosha ya kupambanua
jema na baya na yote hayo, yanasababishwa na vijana kutokuwa na elimu.
No comments:
Post a Comment