Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Mrisho Kikwete atafanya ziara ya siku
mbili mkoani Singida kuanzia tarehe 4 hadi 5 Novemba mwaka huu wa 2012
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa Singida Dokta Parseko V.Kone
wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake akifafanuzi uwepo wa ziara ya Raisi mkoa wa Singida
Dokta Kone amefafanua kuwa Rais atatembelea Miradi
mbalimbali ya barabara pamoja na kuweka
jiwe la msingi katika mradi wa maji Singida mjini unaotekelezwa na Serikali ya
Tanzania pamoja na mkopo nafuu kutoka kwa wahisani
Hii ni mara ya kwanza kwa rais Kikwete kufanya ziara mkoani
Singida tangu kumalizikia kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 uliomweka madarakani
kwa kipindi cha pili na cha mwisho kwa mujibu wa katiba ya Tanzania
Hadi sasa Rais Kikwete yuko mkoani Manyara kwa ziara ya
kikazi baada ya kutoka mkoani arusha ambako amefanya mikutano na viongozi na
wananchi wa mikoa hiyo.
No comments:
Post a Comment