Edson Raymond
MWANZA.
Usiku wa kuamkia Nov 14, 2012, kuliripotiwa kuuwawa
kwa majambazi wawili kwa kupigwa risasi na askari polisi kwa kile kilichodaiwa kutaka
kuhusika kwenye tukio la ujambazi eneo la kilimahewa (big Bite) jiji Mwanza.
Kuuwawa kwa watu hao
ni mwendelezo wa kazi
zinazofanywa na jeshi la polisi jijini mwanza kupambana na uharifu
sambamba na kutokomeza mtandao wa majambazi na hadi sasa takribani watu wanane
wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameuwawa na polisi.
Kutokana na mfululizo wa matukio hayo, nimeanza
kupata wasiwasi juu ya uwezo wa jeshi letu la polisi kukabiliana na ujambazi
unaoonekana kushika kasi sio mwanza tu bali hata sehemu kubwa ya nchi yetu.
Nimekuwa nikijiuliza kwamba kwa mtindo huu wa
kuwauwa majambazi tutamaliza mtandao wao?. Hivi polisi hawana njia
madhubuti/mbadala ya kuwakamata majambazi wakiwa hai paosipo kuwauwa?
Nauliza hivyo kwa kuzingatia umuhimu wa kuwakamata
majambazi wakiwa hai, ili kujua nani kawatuma, kama tunavyojua kuwa majambazi
walio wengi wanakuwa na watu nyuma wanaowawezesha kwa hali na mali maarufu kama
wamiliki wa mtandao wa ujambazi, hii ingesaidia kuwahoji na kuufichua mtandao
wao badala yake tunaishia kuwauwa?!
Ndiyo tunajua hata hao majambazi wanakuwa wamejizatiti kama vile kuwa na
bunduki za hali ya juu mfano Sub Machine Gun (SMG), lakini polisi ni taasisi
kubwa iliyopata mafunzo ya kina ya kukabiliana na adui kwa kila namna pasipo
kumuua. Mfano kuna mafunzo ya kulenga shabaha, hivi haiwezekani kutumia ujuzi
huo hata kulenga sehemu ambayo itampunguzia makali jambazi mfano mguu au mkono?
Akiongea na waandishi wa Habari ofisi kwake mrakibu
mwandamizi wa jeshi la polisi mkoani Mwanza SSP Lily Matola, alisema kuwa tukio
hilo la big bite polisi walikuwa kwenye shughuli zao za kulinda usalama mara
wakasikia watu wanawashia risasi ndo hapo na wao wakaanza kujibizana na ndipo
wakafanyikiwa kuwauwa watu hao wawili huku watatu wakikimbia!
Kwa kauli hiyo ya Bi: lily kunadhihirisha kuwa
polisi wa leo hawahitaji kutumia ujuzi walionao wala kujihangaisha kutumia
juhudi zozote za kuhakikisha wanawatia majambazi nguvuni wakiwa hai na badala
yake wao wanawauwa tu.
Kwa mtindo huo tutajuaje kuwa hao watu walikuwa ni
majambazi? Wametumwa na nani kufanya nini?, wametoka wapi?, na je hao
waliokimbia walikimbilia wapi na wamekimbia na nini?
Kumekuwa na malalamiko juu ya askari polisi
kuhusishwa na ujambazi! Sasa hisia hizi zitaishaje endapo hao majambazi
wasipokamatwa na kuhojiwa na kuwafahamu wahusika wakuu?
Bila jeshi la polisi kuchukua hatua wananchi
tusishabikie vitendo vya polisi kuwauwa majambazi pasipo kuwa tia nguvuni
wakiwa hai kufanya hivyo watakuwa wanauwawa hawa na wapya wanaibuka kwa sababu
wanaowafadhili bado wapo.
No comments:
Post a Comment