Saturday, November 10, 2012

HALI NGUMU YA MAISHA NA HATARI KWA WATOTO

Edilitruda Chami na Phesthow  Sanga
Hali ngumu ya maisha, uzembe katika kufikiri, kupanga mipango ya familia pamoja na uchumi mgumu katika nchi yetu unasababisha baadhi ya wazazi kuwaachia watoto wadogo  majukumu ya  malezi ya wadogo zao, bila kujali hali ya usalama wao
Standard radio imekumbana na hali hiyo katika pita pita za kazi zake mtaa wa ginnery mjini Singida na kuwakuta watoto hao wakileana huku wengine wakiendelea na shughuli walizoachiwa na wazazi wao
Standard  ilijionea yenyewe mtoto mmoja akichuja mafuta ya alizeti katika pipa kubwa lenye ujazo wa lita 240  yanayopikwa kienyeji yanayoitwa {UGIDO} kwa jina maarufu huku wenzake waliobebana wakimchungulia jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa watoto hao
Hii ni hatari sana kwa maisha ya watoto wa mkoa huu kama wazazi hawataliona jambo hili   ”Tuwathamini na kuwalinda watoto wetu”

No comments: