Na.Khadija. A.Mahamba
Kutoendelea kwetu Tanzania kimiundombinu muda mwingine sisi ndio chanzo cha kurudi nyuma, Hili limedhihirika katika kijiji cha Msisi mkoani Singida pale wananchi walipoamua kuharibu barabara ya lami.
Walichukua maamuzi hayo baada ya mtoto Fazila Silaji kugongwa na gari abiria litokalo Geita kwenda Dar es salaam MJ safari lenye namba T 729 ASN na kufariki papo hapo.
Sehemu ya barabara iliyoharibiwa na wananchi wa Musisi Singida wakishinikiza wakala wa barabara tanroads kujenga tuta kuepusha ajali kwa watoto wanaovuka barabara hiyo
Hata hivyo jeshi la polisi linaamua kutumia nguvu kuzuia uharibifu huo kwa kutembeza kichapo kwa wananchi ambapo watu kadhaa wanajeruhiwa huku wengine wakipelekwa mahabusu kwa kosa la kujichukulia hatua mkononi
Mmoja wa wananchi waliopata kipigo toka kwa Polisi wa kutuliza ghasia FFU Singida
Wakiongea na Standard Radio wamedai kuwa kwa muda mrefu wamekua wakiiomba serekali ijenge matuta katika barabara hiyo kwa kuwa iko karibu na shule ya msingi Msisi bila mafanikio, hali inayosababisha kutokea ajali mara kwa mara
Wamethibitisha kuwa katika miezi mitatu iliyopita zimetokea ajali kadhaa zilizosababisha vifo vya takribani watu watano pamoja na mifungo mbalimbali
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa vikosi vya usalama barabarani mkoa wa Singida ASP Mohamed Likwata amesema mtoto Fazila Sija mwenye umri wa miaka kumi wa shule ya msingi msisi darasa la nne amefariki papohapo baada ya kugongwa na basi hilo
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Singida ASP Mohamed akifafanua kuhussu tukio hilo la uvunjivu wa amani na ajali iliyosababisha kifo cha mtoto
Mwili wa marehemu umehifandhiwa katika hospitali ya mkoa wa Singida
Aidha jeshi la polisi mkoani Singida linawashikilia watu kadhaa waliohusika na fujo na uharibifu wa barabara na kwa mujibu wa kamanda Likwata Raia hao wapatao tisa waliodai kuwa na hasira wanafunguliwa mashtaka ya chochea fujo na kuharibu miundo
No comments:
Post a Comment