Na Phesthow Sanga.
Iramba
Watoto hawa
hawasomi?
Siku
hizi si ajabu wala aibu kuwakuta watu wazima katika michezo mbalimbali muda wa
kazi, na michezo inayovuma kwa sasa ni pamoja na mchezo wa POOL ambao nchi
nyingine huchezwa na matajiri tena wakati wa mapumziko ya jioni
Kwa
Tanzania hili ni kinyume chake kabisa, pool huchezwa na vijana pamoja na watoto
tena hohe hahe, wale wasio na ajira, wale ambao ama wana migogoro ya kifamilia
na wenye tabia mbaya katika jamii yao hususani ulevi wa viloba, gongo nk
Nikiwa
katika mji wa Kiomboi huku ikipita huku na huku
nakutana na watoto wa kiume
wanatembea wawili watatu wengine wana
karanga vikapuni wanauza.
Katika hali ambayo sikuwa na jibu nilipata jibu haraka nilipofika
katika eneo la stendi kuu ya mabasi kiomboi ambapo kuna sehemu kumewekwa meza za Pool na
watu hucheza mchezo huo tena mbaya zaid
hucheza kamari ambapo husababisha mara
nyingine Ugomvi kutokea.
“Tafadhali wazazi na wote tunao husika
na malezi ya watoto, Tushirikiane
tulivunje jinamizi hili kwa watoto ili tuondoe wimbi la watoto kuwaita ni watoto wanaoishi katika mazingira
hatarishi.” Pooll ni mchezo mzuri hata hivyo haufai kwa watoto tena
wanafunzi
Mwisho.
No comments:
Post a Comment