Edilitruda Chami Na
Eufrasia Mathias
Singida ni mkoa uliopo katikati ya Tanzania na ni mkoa ambao
una shida ya maji kwa sababu ya ukame kiasi kwamba baadhi ya maeneo hawalimi
mazao yanayohitaji unyevunyevu na maji kwa muda mrefu kama mahindi, maharage na
mbogamboga
Imani ya watu wengi Singida ni kwamba ni vigumu kuwa na ukijani
katika mkoa huo kutokana na upungufu wa maji na mvua ambazo hunyesha kwa misimu
isiyokuwa na mpangilio na wakati mwingine mvua kutokunyesha kwa muda mrefu
Ninachotaka kukuambia msomaji wa hiki ninachokiandika ni
kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na ukijani katika mkoa wa Singida hasa kwa
wale wajanja wanaojua matumizi ya rasilimali chache na adimu kama maji katika
mkoa wa Singida
Sizungumzi kwa maneno tu ila kwa kile nilichokiona na
kukishuhudia tena katikati ya mkoa wa Singida ambapo bustani ya mboga mboga
imeng’aa na ukijani kama uliopo mwambao wa bahari nzuri ndipo nikaamini kuwa kama wewe
unashindwa kuwa na bustani kutokana na ukame kuna mwingine ana bustani naye
anakuuzia mbogamboga unazokula kwako
“jaribu nawe uone!”
No comments:
Post a Comment