Wednesday, November 21, 2012

UVIVU, UZEMBE NA UBISHI NA MAJUNGU NI ADUI WA AJIRA KWA WATANZANIA

MR. James J. Daud Mkurugenzi mtendaji wa Standard Voice na Buhanzo Enterprises LTD

Na Edilitruda Chami
Dar es Salaam

Mkurugenzi wa makampuni ya Standard Voice limited na Buhanzo enterprises Limited Bw. James Japhet Daud amesema watanzania wengi wanalalamika juu ya ukosekanaji wa ajira, huku wenye ajira nao wakisahau Kuwa uangalifu na uadilifu mahala pa kazi ni jambo muhimu sana ikiwa ni pamoja  na kuheshimu kazi uliyoipata na kujituma kwa juhudi ili kile ulichokipata kisikuponyoke.

Akizungumza na standard radio  ofisini kwake  Bw. Daudi  amesema ushirikiano, upendo, maadili ya kazi ndiyo njia pekee inayoweza kumfanya mfanyakazi  akaishi maisha mazuri akiwa kazini huku akiamini kuwa majungu, fitina na  uvivu  ni adui mkubwa katika makampuni mengi.

Aidha Bw. Daud amesisitiza kuwa kila binadamu huwa anakumbana na changamoto mbalimbali na kujiona kama vile hana njia ya kuzitafutia ufumbuzi, kumbe kutafuta ufumbuzi  katika changamoto zozote yapasa kutumia akili na uwezo kwani  hakuna jambo linaloshindikana ila uzembe na kujiona kuwa jambo haliwezekani

Pamoja na hayo;  baadhi ya wafanyakazi  wa kampuni ya Buhanzo wamekiri kuwa umakini katika kazi ni jambo zuri sana hasa ukizingatia maadili ya kazi,  kila kitu kitakwenda sawia na siyo kwenda kinyume  halafu kazi ikianza kwenda ndivyo sivyo malalamishi yanakwenda kwa mwajiri bila kutizama chanzo cha changamoto  hizo.

Pichani ni baadhi ya watumishi wa kampuni ya Buhanzo Enterprises ya Jijini Dar es salaam wakiwa katika majukumu yao
Ustaadhi Hamis Manyema, afisa masoko msaidizi Buhanzo Enterprises Dar es Salaam
 

 
 
Mr. Prosper Ngairo Meneja msoko
 
 

 

2 comments:

Anonymous said...

Imetulia sana na ina mashiko ndani yake. kwa mwenye akili timamu akae chini kuisoma na kuitafakari!

Anonymous said...

ujumbe makini