Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete amesema Tanzania haina mpango wowote wa kuingia vitani na nchi ya Malawi kugombea mpaka wake katika ziwa Nyasa ambalo Malawi huliita ziwa Malawi
Na. Prosper Kwigize
Dodoma
Kauli hiyo ameitoa jumapili
November 11, 2012 katika mkutano mkuu wa nane wa Chama cha Mapinduzi CCM mjini
Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine chama hicho kitafanya uchaguzi wa
viongozi wa chama hicho
Rais Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa taifa wa chama cha
mapinduzi amekiri kuwepo kwa mgogoro wa kimpaka baina ya Tanzania na Malawi ambapo
Tanzania inatoa hoja kuwa mpaka huo uko katikati ya ziwa huku Malawi wao
wakidai kuwa mpaka uko ufukweni upande wa Tanzania eneo la mbambabay
Hata hivyo rais Kikwete amebainisha kuwa pamoja na
kutokuwepo na nia ya kuingia vitani na Malawi, Tanzania inaendelea kuimarisha
uwezo wa majeshi yake kwa kutoa mafunzo na kuongeza zana za kivita ili kuwaweka
tayari wapiganaji kulinda mipaka na usalama wa watanzania
Aidha ameonya kuwepo kwa watu wanaoichafua nchi kuwa
serikali imepeleka vikosi mpakani kwa nia ya kujiandaa kupigana na Malawi na
ametaja kuwa huo ni uongo na Tanzania haina mpango huo na wanaoeneza uvumi huo
hawana nia njema na taifa la Tanzania.
Wakati huo huo Dr. Kikwete ametoa wito kwa watanzania kuacha
malumbano na chuki za kutafuta vyeo badala yake wasimamie utekelezaji wa ilani
ya uchaguzi ya CCM na pale penye mafanikio watembee kifua mbele na wasitishwe
na washindani wa CCM ambao wamekuwa wakidai kuwa CCM hakijafanya kitu
Rais Kikwete ameinadi miradi mikubwa ua jenzi wa barabara,
elimu, Nishati na utaratibu wa kutumia mapato ya ndani kupitia makusanyo ya
kodi kuwa ni kiashiria cha CCM kufanya vema katika kuleta maendeleo kwa
watanzania
WAKATI HUO HUO kamati kuu ya CCM imempendekeza Dr. Muhamed Ally Shein na Philp Mangula kuwa wagombea wa nafasi ya makamu mwenyekiti baada ya Tamko la kustaafu kwa Aman Karume wa Zanzibar na Pius Msekwa wa Bara.
WAKATI HUO HUO kamati kuu ya CCM imempendekeza Dr. Muhamed Ally Shein na Philp Mangula kuwa wagombea wa nafasi ya makamu mwenyekiti baada ya Tamko la kustaafu kwa Aman Karume wa Zanzibar na Pius Msekwa wa Bara.
1 comment:
HONGERA RAIS WETU KWA KAULI HIYO, VITA SI TIBA YA UKOROFI WA JIRANI YETU MALAWI BALI ELIMU NA MAZUNGUMZO YATATUWEZESHA KUSHINDA.
ASANTE STANDARD KWA KUTUPA HABARI HII HARAKA IWEZEKANAVYO, NAJUA MAGAZETI YATALETA HABARI ZA DODOMA KESHO
Post a Comment