Na Evarista Lucas
Singida
Nov
21,2012
Klabu ya Waandishi wa
Habari Singida(SINGPRESS) mapema wiki hii imepokea vifaa vya ofisi vyenye thamani ya shilingi milioni
thelathini na tano kwa ajili ya matumizi ya ofisi na ikiwa utekelezaji wa
mpango mkakati wa Muungano wa Klabu za
Waandishi wa Habari Tanzania(UTPC).
Akikabidhi vifaa
hivyo mapema wiki hii kwa uongozi wa
SINGPRESS; Afisa Programu, mahusiano ya Klabu na ufuatiliaji; Bwana Victor
Maleko alisema; “Vifaa hivi tulivyoleta
ni kwaajili ya kuziwezesha Klabu za Waandishi wa habari nchini kuweza
kujiendesha zenyewe kwa kutumia vifaa hivi ambavyo vitakuwa kama chanzo cha
mapato ya Klabu. Pia ni utekelezaji wa mpango mkakati waUTPC na mkataba
uliotiwa saini na Klabu wanachama
ikiwemo mafunzo yanayoendelea kutolewa na UTPC.”
Wakielezea kufarijika
kwao na kupatiwa vifaa hivyo; baadhi ya viongozi wa SINGPRESS wamesema kuwa
hiyo ni hatua moja kubwa sana kwa Klabu na wanachama wa SINGPRESS kwa ujumla. “
Tutapata na kuongeza kipato cha Klabu
kupitia mmradi wa huduma ya steshenari na ukodishaji wa vifaa mbali mbali vya
Klabu kama kamera na vinasa sauti hata projekta.” Alisema kaimu katibu Mtendaji
wa SINGPRESS Bwana Elisante John.
Baadhi ya Vifaa vilivyopokelewa katika ofisi
ya SINGPRESS ni pamoja na kamera ya picha za mnato, vidadavuzi, projekta,
kinasa sauti, mashine ya kutolea kopi,
video(TV Flat Screen) deki ya DvD ,na
mashine ya kuchomea (laminator) vyenye thamani ya shilingi milioni
thelathini na tano tu.
Kwa upande mwingine
licha ya kupata vifaa hivyo ambavyo vitawasaidia katika utendaji kazi wao wa
kila siku; wanachama wa SINGPRESS wamekuwa wakinufaika na mafunzo mbali mbali
yanayoendelea kutolewa na MUungano wa Klabu za Waandishi wa Habri Tanzania
ikiwa ni utekelezaji wa mpango mkakati na hati ya makubaliano baina ya UTPC na
SINGPRESS uliotiwa saini mnamo mwaka jana.
2 comments:
Try to edit the story before publish.
thank you very much for visiting our bolog and we are happy to receive and publish your online comment. we promise to use it
Post a Comment