Mkuu wa wilaya ya IrambaBwana Yahya Nawanda; amewaasa viongozi na wanachama wa
Klabu ya waandishi wa habari Singida(SINGPRESSkuyafuata yale waliyoafikiana katika mkutano na kuhakikisha kuwa
hawaendi kinyume na mabadiliko hayo.
Akihutubia wanachama hao katika mkutano
wao wa marekebisho ya katiba ya SINGPRESS uliofanika katika kijiji cha Kiomboi
wilaya ya Iramba mkoani Singida; Nawanda aliwawataka wanachama hao kuwa mfano
mzuri wa kuigwa kwa kufuata maadili ya kazi yao.
“Siku hizi tasnia ya uandishi wa
habari imekuwa inaingiliwa sana
na watu na watu wasiokuwa na maadiliambao ndio wanaofanya kazi hii na heshima mbele ya jamii, kwani uandishi
ni maadili.” Alisisitiza Nawanda.
Kwa upande mwingine Nawanda
aliwataka wanachama hao kuepukana na ushabiki wa kisiasa ili waweze kufanya
kazi yao kwa ufanisi zaidi na kwa kuzingatia
maadili ya kazi yao.“Baadhi yenu mmekuwa wanasiasa tena wa wazi
wazi. Mnafanya kazi yaviongozi wa
siasa. Mimi nawaasa mfuate maadili ya uandishi wa habari na kuachana na siasa.”
Nawanda.
Lichaya hayoNawanda aliwaomba wanachama hao kuandika pia mambo mazuri ambayo
yamefanyika hapa mkoani ikiwemo ujenzi wa hospitali ya kisasa ya rufaa,
barabara za lami na makazi bora.
“Tutawapa ushirikiano mkubwa
waandishi wa habari kwani nyie ni watu muhimu kuhabarisha Watanzania kile
tunachokifanya katika maendeleo ya mkoa wetu. Wasaidieni kuandika makundi
maalumu kamavile walemavu, changamoto zao na ustawi wao kwa ujumla na sio kujikita
kwenye siasa tu. Sasa Tanzania
tunajua mwandishi bora ni yule anayejikita kwenye siasa tu.”Nawanda
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
SINGPRESS Bwana Seif Takaza alimshukuru mkuu huyo wa wilayakwa kuitikia wito wa kuwa mgeni wa heshima
katika mkutano wao na pia kwa kuwapatia ukumbi uliowawezesha kuikamilisha kazi
hiyo muhimu kwa maendeleo ya Klabu.
“Hii ni awamu ya pili kwa waandishi wa habari
kufika katika wilaya ya Irambaawmu ya
kwanza ilikuwa ni Mei 3 mwaka huu siku ya uhuru wa vyuombo vya habari ambapo
tulikwenda kwa Wahadzabe na kutoa msaada wa chakula na vifaa vya shule. Leo
tena awamu ya pili tunafanya mkutano huu hapa.
Katika mkutano huo uliojumuisha wanachama kumi
na saba (17) wa SINGPRESS wanachama walipata fursa ya kuipitia kwa umakini
katiba hiyo na baadhi ya vipengele vilivyoongezeka katika katiba hiyo.”
Waandishi wa habari mkoani Kigoma wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Kigoma Bw. ramadhan Maneno pamoja na wakufunzi kutoka MCT Bw. Deodatus Balile mhariri mtendaji wa gazeti la JAMHURI na Bi. Rose Mwalongo kutoka tume ya haki za binadamu na utawala bora na pia mwandishi wa gazeti la Guardian
Baraza la habari Tanzania linatoa mafunzo ya maadili na kulitangaza azimio la Dar es salaam kuhusu uhuru wa uhariri na uwajibikaji wa vyombo vya habari nchini Tanzania
Tama tamko la Dar es salaam litazingatiwa ni dhahiri kuwa kazi ya uandishi wa habari itakuwa rahisi na yenye tija kwa taifa la Tanzania
Tidha maadili ni jambo la muhimu ili kufanikisha utekelezwaji wa tamko hilo
Arcado
Denis Ntagazwa ni mmoja wa wasomi wa enzi hizo ambaye akitokea kijiji cha
KIzazi wilayani Kibondo mkoani Kigoma alifanikiwa kushika nyadhifa nyingi
ikiwemoo ubunge na uwaziri kwa nyakati tofauti tangu wakati wa Rais wa kwanza
wa Tanzania hayati baba wa taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere
Ntagazwa
ambaye amewahi kujinadi kama mbunge wa kudumu wa jimbo la Muhambwe aliangushwa
na mwana usalama wa Ikulu Felix Ntibenda katika kinyang’anyiro cha Ubunge
katika kura za maoni ndani ya CCM
Haikuwa jambo
jepesi kumng’oa Ntagazwa kwani alikuwa amejizatiti vilivyo kwa kuwaweka sawa
vijana, wanawake na wazee waliokuwa wamelishwa yamini kwa Khanga, Baiskeli na
simu za mkononi alizowagawia kuwashawishi wamwamini kuwa ndiye anayefaa kuwa
mbunge kwa miaka mingine 5 atimize miaka 30 ya ubunge
Leo
Ntagazwa ni kamanda wa CHADEMA amekuwa akizunguka huku na kule kukinanga chama
chake cha zamani CCM akiwatuhumu kuwa nii vinala wa Rushwa na wanadidimiza
maendeleo
Ntagazwa
hakukurupuka kwenda CHADEMA, kutokana na umakini na ufahamu wake alijipa muda
wa kutafakari tangu mwaka 2005 hadi 2010 alipojaribu tena kugombea katika kura
za maoni za CCM na kushindwa
Je? anapopambana leo na CCM kwa tuhuma za RUSHWA
ni dhamira ya dhati au HASIRA ZA KUUKOSA UBUNGE ndani ya CCM na hata huko
chadema alikokwenda baadaye
Wanaharakati
hasa vijana tunapaswa kujiridhisha na DHAMIRA ya NTAGAZWA na tujiulize pia kama
yeye hakuwa mtoa rushwa kabla ya kuhujumiwa na wapiga kura waliokula vya kwake
na kasha kumtosa katika karatasi za kura
Hizi siasa
za watanzania wanaokuwa watakatifu mara wanapokosa nafasi CCM na kuhamia
upinzani huku wakituaminisha kuwa wao ni wema na wanayajua madhambi ya zamani
nadhani ni busara kama wakitanguliza kuomba radhi kwa maovu waliyafanya kabla
ya kututangazia utakatifu wao baada ya kuhama CCM
Huo ndio
uungwana na sisi tutawaamini
Haya ni Maoni
yangu ninakaribisha mjadala katika hili
Baada ya mazungumzo kati ya Malawi na Tanzania kuhusu mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa kugonga mwamba, Tanzania imesema mazungumzo mengine yatafanyika tarehe 10 mwezi ujao kujaribu tena kutatua mzozo uliopo.
Katika mazungumzo yaliofanyika nchini Malawi mjini Mzuzu, Malawi ilitaka mzozo huo utatuliwe katika mahakama ya kimataifa ya ICJ.
Kwa upande wake Tanzania imepinga suaa hilo kutatuliwa na mahakama ya kimataifa badala yake kuwepo na mazungumzo zaidi
Hata hivyo serikali ya tanzania imeendelea na msimamo wake wa kupiga marufuku shughuli za utafiti wa mafuta zinazoendeshwa na Malawi
Hofu bado imetanda juu ya uwezekano mkubwa wa kuibuka kwa vita kali ya kugombania mpaka kama ilivyokuwa kwa Idd Amin Dada mwaka 1978
Nchi ya Malawi imelimega ziwa lote na kulifanya kuwa ndilo mpaka wa nchi zetu lakini haikufanya hivyo kwa upande wa Msumbiji ambao wao wanagawana ziwa hilo katikati
inakuwaje tanzania ihujumiwe kuwa ziwa lote ni la malawi lakini haifanyi hivyo kwa Mozambique?
angalia ramani hizi
Hii ni ramani inayoonesha mipaka ya Tanzania na nchi jirani kama ilivyochorwa tangu mwaka 1913, eneo la Ziwa Nyasa ambalo leo Malawi wanaliita Ziwa Malawi mpaka wa Tanzania na Malawi uko katikati ya ziwa, lakini malawi walibadili mpaka huo
Ramani hii inaonesha sehemu ya ziwa Nyansa kama ilivyobadilishwa na Malawi miaka ya 1964 baada ya uhuru wa Taifa lao, eneo la ziwa linaiondoa Tanzania katika umiliki wa sehemu wa Ziwa hilo lakini ukitazama kwa chini eneo la Mozambique kitendo hicho hakikufanyika, wao wanagawana ziwa hilo katikati, Je ni nini hoja ya Malawi kwa Tanzania?
Mhariri mtendaji wa gazeti la JAMHURI Bw. Deodatus Balile
amebainisha kutofurahishwa na tabia ya ngwaandishi wengi nchini kugeuzwa kuwa
mabango ya makampuni na taasisi mbalimbali kwa kuvaa mavazi hususani fulana
(tshirt) zenye matangazo
Balile amesema hayo mjini Kigoma wakati wa mafunzo ya
maadili kwa waandishi wa habari mkoani humo sambamba na kufafanua azimio la Dar
es salaam juu ya UHURU WA UHARIRI NA UWAJIBIKAJI yanayosimamiwa na Barala la
Habari Tanzania MCT
Ameeleza kuwa maeneo mengi hususani mikoani waandishi wa
habari wengi wamekuwa wakivaa kila e matangazo ya makampuni Fulani, jambo
ambalo tafsri yake ni kwamba habari nyingi zinazoandikwa na waandishi hao ni
zile zilizogharimiwa na mashirika, kampuni au taasisi iliyomgwia fulana au
kofia.
“jamani vaeni mavani yenu tena yawe ya heshima, si kuvaa
nguo za kupewa, kwani ninyi hamuwezi kujinunulia nguo? Hta hivyo nawapongza Kigoma
hamna tabia hiyo ya kuguzwa kuwa mabango ya makampuni na mashirika kwa kuvaa
mavazi yao” alisema Balileoni
Tanzania ni miongoni mwa nchi chini ya jangwa la sahara ambazo waandishi wake wa habari wanaishi kwa kipato cha chini sana kutokana na wamiliki wa vyombo vya habari kutowapa mikataba na pia kuwalipa kiwango kidogo cha mishahara au posho za kazi zao
kwa waandishi wa mikoani hasa wanaoandika habari za magazeti, wengi wao hawapati malipo kutoka kwa vyobo vyao na hivyo maisha yao huyaendesha kwa kutegemea posho kutoka kwa wadau wa habari, mashirika na taasisi mbalimbali za serikali, pindi wanapokuwa na jambo la kuandikwa au kutangazwa na vyombo vya habari hulazimika kutoa chochote (mshiko) ili habari zao ziandikwe
Jambo hili linachangia sana kuporomoka kwa maadili ya uandishi wa habari na vyobo vya habari.
Mkuu wa wilaya ya Manyoni mkoani Singida Bibi Fatuma Toufiq akitembelea moja ya kaya wakati za zoezi la sensa
Doris Meghji Jumatatu
Manyoni – Singida
Zoezi la sensa ya watu na makazi
wilayani Manyoni linaendelea vizuri licha ya changamoto mbali mbali
zilizojotokeza kwenye utekelezaji wa zoezi hilo katika baadhi ya vitongoji na
vijiji juu ya suala la mipaka kati wilaya ya Uyui, Bahi,Sikonge na Manyoni
Mkuu wa wilaya ya Manyoni Bi Fatuma
Toufiq ametoa taarifa hiyo wilayani humo jana mara baada ya kutembelea baadhi
ya maeneo na kujua hali ya zoezi hilo limekwendaje
Bi Toufiq amesema kuhusu suala la
mipaka katika vijiji vilivyoko mpakani kati ya wilaya yake na wilaya za
Uyui,Bahi na Ikungu limetatuliwa kwa vijiji hivyo kuhesabiwa kuwa viko manyoni
kutokana na ramani za kuhesabia maeneo (EA) zinavyoonyesha kwa makarani wa
sensa ya watu na makazi wilayani humo
Aidha amesema katika wilaya yake
wananchi wengi wameitikia zeozi hilo kwa kutoa ushrikiano kwa makarani wa sensa
ya watu na makazi wa madodoso yote kwa kutoa taarifa sahihi kwa makarani huku
akiwataka wananchi kutohujumu zoezhi hilo kwa kutoa ushrikiano kwa makarani wa
sensa
Amesema “Ni kaya mmoja nilivyopewa
taarifa kuna mtu alikataa kuhesabiwa akidai yeye ni muislam,lakini baada ya
kuelimishwa na karani wetu alikubali kuhesabiwa kwa hiyo mwandishi hilo ni kaya
moja ambayo alijitokeza mtu asiyetaka kuhesabiwa na kutatuliwa” alisema Mkuu
huyo.
Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya
amesisitiza wananchi kuendelea kutoa ushrikiano kwa makarani hao wa sensa ili
kufanikisha zoezi hilo la sensa ya watu na makazi litakalodumu kwa muda wa siku
saba huku wilaya hiyo ikiwa na jumla ya kata thelathini.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) jana kilitikisa Jimbo la Igunga mkoani Tabora, kwa kufanya mkutano
mkubwa wa hadhara ikiwa ni mara ya kwanza tangu Mahakama Kuu Kanda Tabora
kutengua ubunge wa Dk Dalaly Kafumu wa Chama Cha Mapinduzi, huku kikiionya CCM
kuwa kitaumbuka iwapo kitakata rufaa kwa uamuzi huo wa mahakama.
Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika Viwanja vya Sokoine, Katibu
Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa alisema CCM kisithubutu kukata rufaa kwani
kitaumbuka kwa kuwa kilicheza faulo nyingi katika uchaguzi huo.
Alisema ameshangazwa na kauli ya CCM kusema kuwa kitakata rufaa katika kesi
hiyo wakati kisheria, kwa kesi za uchaguzi na pia katika hatua hiyo chama
hakina nafasi yoyote bali mgombea au mwanachama wa chama husika, ndiye
anayeweza kwenda mahakamani kufungua kesi na kupinga.
Katika mkutano huo uliofurika maelfu ya wanachama na washabiki wa wa chama
hicho, Dk Slaa alisema kuwa Chadema kitakiangusha vibaya CCM hata ikiwa
uchaguzi katika Jimbo la Igunga utarudiwa.
Huku akitoa mifano mbalimbali ya jinsi baadhi ya wanachama wa CCM walivyokuwa
wakitoa rushwa, Dk Slaa alimtuhumu Mweka Hazina wa chama hicho, Mwigulu
Nchemba, ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi kwamba alikuwa kinara wa
kutoa rushwa katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Igunga Oktoba mwaka uliopita.
“Chadema imejipanga kwa rufaa hiyo ya CCM ikiwa ni pamoja na kufungua kesi
nyingine dhidi ya vigogo wa CCM, walioshiriki katika kampeni za uchaguzi
huo,”alisema Dk Slaa.
Dk Slaa pia alimponda Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akieleza kuwa mdomo
wake umemponza kwa sababu alikuwa akizungumza mambo ambayo hakujua madhara
yake.
Wakati akitoa hukumu ya kesi hiyo, Jaji Mary Nsimbo Shangali wa Mahakama Kuu
alisema moja ya hoja saba zilizotolewa na Chadema ambayo mahakama iliikubali ni
ile ya Mukama kudai Chadema kilipeleka makomandoo katika uchaguzi huo na
kupanga kuuvuruga.
Dk Slaa alisema: “Mukama alikurupuka kwa kutamka maneno bila kufanya utafiti
hali iliyosababisha CCM kupoteza jimbo.”
Alikwenda mbali zaidi na kueleza kuwa suala la CCM kuingiza silaha ndani ya
nchi, bila kibali wala leseni na kuwapatia vijana wake mafunzo katika kambi za
Ilemo, Iramba mkoani Singida linamhusu mwenyekiti wa chama hicho na siyo mtu
mwingine.
Alidai kuwa wakati wa uchaguzi wa Igunga, vijana hao walikuwa wakipewa mafunzo
ya kijeshi akisisitiza kuwa suala hilo linamhusu mwenyekiti wa chama hicho
akimtaka atoe majibu na ufafanuzi juu ya hilo.
Dk Slaa alisema kuwa siku ya jana ilikuwa ni kwa ajili ya wananchi wa Igunga
kusherehekea na kupongezana kwa mshikamano waliouonyesha wakati wote wa
kusikilizwa kwa kesi hiyo, huku akitoa pongezi kwa mawakili waliosimamia kesi
hiyo kwa kuiwakilisha vyema Chadema katika kesi hiyo.
Naye upande wake aliyekuwa mgombea wa Chadema katika uchaguzi mdogo wa Igunga
Oktoba mwaka uliopita, Joseph Kashindye aliwashukuru wananchi walioiunga mkono
Chadema akieleza kuwa wameonyesha ushirikiano mkubwa uliokipa ushindi chama
hicho kikuu cha upinzani nchini.
Kashindye aliwashukuru pia wananchi wa Igunga kwa kukichangia Chadema Sh6
milioni zilizosaidia kulipia gharama za kesi hiyo pamoja na malazi kwa
mashahidi mbalimbali waliotoa ushahidi kwenye kesi dhidi ya CCM iliyotolewa
hukumu wiki iliyopita kwa kutengua ushindi wa Dk Dalaly Kafumu wa CCM.
“Mahakama imetenda haki kwa kuwa imetoa hukumu ya haki…, nimeamini kuwa haki ya
mtu haipotei. Awali nilidhani kuwa mahakama ni mali ya CCM kumbe si kweli,”
alisema Kashindye na kushangiliwa na mamia ya watu waliofurika katika uwanja
huo.
Kashindye aliponda ahadi zilizokuwa zikitolewa na Waziri wa Ujenzi, Dk John
Magufuli, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kwamba ndizo zilizofanya CCM kushindwa
kesi.
“Watu wa ajabu sana, wametoa ahadi za kujenga madaraja, kusaidia chakula wakati
hilo ni jukumu la Serikali,” alisema Kashindye akionyesha kushangaa.
Alibainisha kuwa wakati kesi hiyo ikinguruma mahakamani, alikuwa akitafutwa na
wanachama wa CCM, lakini kutokana na kujua mbinu zao, aliamua kujichimbia
kusikojulikana.
Dk Kafumu aliibuka mshindi katika uchaguzi huo mdogo uliofanyika Oktoba 2,
mwaka jana kuziba nafasi ya Rostam Aziz ambaye alijiuzulu kwa madai kwamba
anaachana na siasa chafu ndani ya CCM.
Katika uchaguzi huo kulikuwa na upinzani mkubwa kati ya Dk Kafumu na aliyekuwa
mgombea wa Chadema, Joseph Kashindye ambaye hakuridhishwa na mwenendo wa
uchaguzi huo, hivyo kuamua kupinga matokeo hayo mahakamani. Kesi hiyo
ilifunguliwa Machi 26, mwaka huu.
Karani wa Sensa akijaza takwimu muhimu za sensa katika Dodoso, hapo ni nyumbani kwa mkurugenzi wa Standard Radio Fm Bw. Prosper Kwigize mjini Kasulu mkoani Kigoma
Standard
Radio fm
The Voice
of Voiceless
90.1 mhz
SINGIDA
TANZANIA
UONGOZI WA
MAKAMPUNI YA BUHANZO ENTERPRISES, STANDARD VOICE LTD NA STANDARD RADIO FM TUNAWATAKIA WATANZANIA
USHIRIKI MZURI WA ZOEZI LA SENSA YA WATU NA MAKAZI KWA AJILI YA KUPATA TAKWIMU
SAHIHI KWA MAENDELEO
TUNAWASIHI
WATANZANIA KUJIOKEZA KUSHIRIKI ZOEZI HILI
SERIKALI ya wilaya mpya Mkalama mkoani Singida, imeahidi kutoa nyama pori ya kutosha kwa Wahadzabe wa kitongoji cha Kipamba kata ya Mwangeza, ili waweze kushiriki sensa ya kitaifa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchini kote agosti 26 mwaka huu.
Mkuu wa wilaya hiyo Edward Ole Lenga,amesema msaada wa nyama ya wanyama pori hiyo, utasaidia jamii ya Wahdzabe kubaki kwenye kaya zao kipindi chote cha sensa.
Akizungumza muda mfupi kabla ya kumkaribisha mkuu wa mkoa wa SIngida, Dk. Parseko Kone, awahamasishe Wadzabe na wakazi wengine wa kata ya Munguli, kushiriki sensa,Lenga alisema msaada huo wa nyama pori, unatokana na ombi liliotolewa na jamii hiyo ambayo chakula chake kikuu ni,nyamapori,mizizi,matunda pori na asali.
Akifafanua, alisema Wahdzabe hao wanaokadiriwa kufikia 227, wametoa ombi hilo ili wakati wote wa sensa wasiende porini kuwinda na badala yake wabaki kwenye kaya zao wakisubiri kuhesabiwa.
“Mheshimiwa mkuu wa mkoa, ndugu zetu hawa Wahdzabe, waliomba wapatiwe nyamapori ambayo ndiyo chakula chao kikuu, ili siku ya sensa wasiende kuwinda porini, kwa kweli endapo watapatiwa nyama hiyo, wamenihakikishia watabaki majumbani kusubiri makarani wa sensa”,alisema.
Mkuu huyo wa wilaya,alisema ombi hilo tayari limeishakubaliwa na maandalizi yote muhimu ya kuwinda wanyama pori siku moja kabla ya siku ya sensa, yamekwisha kamilika.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa Dk. Kone, yeyey alitoa msaada wa chakula chenye uzito wa zaidi ya tani moja, ambacho kitakidhi mahitaji kuanzia sasa hadi zoezi la sensa litakapokamilika.
“nimewaletea hiki chakula amacho ni mchele uliochangwa na vyakula mbali mbali ikiwemo pia mboga mboga ,kutoka shirika lisilo la kiserikali la International Africa Outreach la nchini Marekani. Chakula hiki ni kizuri mno, kina virutubisho vingi”alifafanua Dk.Kone.
Alisema kwa hali hiyo, kipindi chote cha sensa, hapatakuwepo na haja kwenda porini kutafuta wanyama pori, asali, matunda pori au mizizi.
Katika hatua nyingine,aliwataka wahakikishe kila mmoja anahesabiwa mara moja tu, kwa madai kuwa wakishafahamika idadi yao na hali zao za maisha, itasaidia serikali kujipanga namna bora ya kuwahudumia na kuwaletea maendeleo.
Wakati huo huo Dk. Kone, alisema pamoja na kunid la wawindaji, pia makundi mengine ya wavuvi, wachungaji wanaohama hama hama, watafutaji madini na baadhi ya wakulima ambao wana mashamba yaliyo mbali na makazi au makambi yoa ya kawaida, warejee kwenye kaya na makambi yao,ili waweze kuhesabiwa siku ya sensa.
DIFFERENTIAL
DIAGNOSIS OF:NEW CASES, OLD CASES AND
AMBULATORIES NEW CASES.
•EPILEPSY
•ACUTE
PSYCHOSIS
•SCHIZOPHRENIA
•TOXICOMANY
•MENTAL
RETARDATION
•DEMENCE
SENILLE
•DEPRESSION
•BIPOLAR
•ANXIETY
•ALCOHOLISM
•There are different pathologies in SDPC. The first one is: ‘’Epilepsy’’.
SDPC is known as a subject which stabilize people who are suffering from
Epilepsy, Psychosis and Schizophrenia. The centre receives also the
Toxicomanies because Toxicomany has been observed in Kigoma region and its
really affect peoples more especially young ones.
SERIKALI wilayani Singida, imeahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGos) ikiwemo shirika la World vision, ili kuharakisha upatikanaji wa maendeleo endelevu kwa wakazi wa wilaya hiyo.
Ahadi hiyo imetolewa juzi na mkuu wa wilaya ya singida, Queen Mlozi, wakati akifungua warsha ya siku tatu iliyohusu kuwasilisha mpango wa STF/EMLAP unaotekelezwa na shirika la World vision.
Alisema mlango wa ofisi yake upo wazi wakati wote kwa mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau mbali mbali wa maendeleo, katika kushirikiana kutatua kero zinazowakabili wananchi.
“Mimi naomba tufanye kazi kama timu moja, wimbo wetu uwe moja, nao ni kuwaletea wananchi wetu maendeleo ya kweli.Kwa njia hii, tutaharakisha kuboresha maisha yawananchikiuchumi na kijamii",lifafanua Mlozi.
Dc huyo alifafanua zaidi kwa kusema, serikali kwa upande wake, haina uwezo wa kutosha kufanya kila kitu kwa maendeleo ya wananchi, kwa hiyo ushirikiano wa NGos na wadau wengine, ni muhimu mno.
Katika hatua nyingine, Mlozi alitumia fursa hiyo kulipongeza shirika la World vision kwa juhudi zake za makusudikuanzisha miradi mbali mbali wilayani Singida na hasa katika tarafa ya Mtinko.
“Wananchi wa wilaya ya Singida, tunapaswa kutunza na kuilinda miradi hii iliyoanzishwa na World vision, iweze kudumu kwa muda mrefu.Kwa njia hii, tutakuwa tunawatia moyo wenzetu wa World vision kuendelea kuleta neema ya miradi zaidi wilayani kwetu”,alisema.
Awali mratibu wa World vision Mtinko ADP,Edwin Maleko, alisema kwa mwaka huu, wametumia zaidi ya shilingi milioni 107.8 kugharamia utekelezaji wa mradi wa afya katika tarafa ya Mtinko.
Alitaja baadhi ya shughuli walizotekeleza kuwa ni kutoa mafunzo kwa vitendo kwa vikundi 51 vya lishe kuhusu njia sahihi za ulishaji wa watoto wadogo na wachanga na kugharamia kilniki tembezi 22 kwa vijiji vya Minyenye na Mughanga.
Maleko alitaja shughuli zingine kuwa ni kukarabati mtando wa maji unaohudumia vijiji vya Mtinko,Nduu,Malolo na Kijota na kuwezesha michezo ya mpira wa miguu,pete na kikapu baina ya vijana wa vijiji 19 ,kwa lengo la kutoa ujumbe unaohusu VVU na UKIMWI.
MWENYEKITI wa Chama cha United Peoples Democratic (UPDP), Fahmi Dovutwa, amemfananisha Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa na Waziri Mkuu Mstaafu, marehemu Rashid Kawawa.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Dovutwa alisema Lowassa hana tofauti na Kawawa, ambaye katika uhai wake akiwa waziri mkuu alibeba lawama za Serikali katika utawala wa awamu ya kwanza.
Dovutwa ambaye mwaka 2010 aligombea urais, alisema Lowassa hakuhusika katika kashfa ya rushwa iliyotokana na mkataba tata wa Richmond na kwamba alijiuzulu uwaziri mkuu ili kulinda heshima ya Serikali na si vinginevyo.
“Mwalimu Nyerere alipata kutoa hotuba siku moja akisema kwamba: ‘Namshukuru sana mzee Rashidi Mfaume Kawawa, amenisaidia sana.
‘Mambo yote ambayo amekuwa akilaumiwa Kawawa niliyafanya mimi na yeye (Kawawa) alibeba tuhuma hizo kwa ajili yangu’, haya ni maneno ya Baba wa Taifa na hotuba zake hizi zipo,” alisema Dovutwa akimnukuu Mwalimu.
Dovutwa aliongeza: “Kwa kauli hiyo ya Baba wa Taifa ni wazi Lowassa hakuhusika na kashfa ya Richmond. Kwa sababu maamuzi ya kiutendaji wa Serikali yako mikononi mwa Baraza la Mawaziri ambalo mwenyekiti wake ni Rais.
“Waziri yeyote hana uwezo wala mamlaka ya kuamua jambo bila ridhaa ya Rais. Lowassa aliwajibika ili kuilinda Serikali ya CCM chini ya Rais Kikwete isianguke na kupisha uchaguzi mwingine,” alisema.
“Mwalimu Nyerere alielewa vizuri dhana ya uwajibikaji na Watanzania wengi hawakumwelewa Mwalimu Nyerere alipokuwa akiwarudisha baadhi ya watumishi ambao awali waliwajibika kwa tuhuma za kiutumishi.
“Kimsingi tuhuma alizokuwa amelaumiwa kiongozi mwandamizi wa Serikali zilikuwa ni tuhuma za kiongozi mkuu wa Serikali ambaye ndiye mwenye mamlaka ya kuamua kufanya jambo au kulikataa.
“Ili kuilinda Serikali na kiongozi mkuu wa Serikali ndipo hutokea mtumishi mmoja wa Serikali kubeba lawama na tuhuma za wizara yake kwa manufaa ya Serikali yenyewe.
Hivyo dhana ya kuwajibika ilieleweka vizuri kwa Mwalimu Nyerere kuliko wasomi walio wengi wa ndani na nje ya CCM,” alisema Dovutwa.
Dovutwa alisema Lowassa ni kiongozi makini mwenye ujasiri ambaye aliweza kufanya mambo akiwa waziri mkuu, huku akiwatahadharisha wananchi kuwa makini na baadhi ya viongozi.
“Watanzania tusikumbuke kufanya mabadiliko ambayo huenda tukaondoa wala rushwa wadogo na kuingiza wala rushwa wakubwa zaidi,” alisema.
Dovutwa aliwataka Watanzania kutafakari juu ya mwenendo wa vyama vilivyoko bungeni, hasa kutokana na Bunge kuchafuka kutokana na kashfa ya rushwa inayowahusisha wabunge.
As african country we should have enough time to think on our problem and how to recover lather than still fighting, one mistake made by one of the african country should be a lesson to another, But what Burundi could teach Rwanda? please follow this story from Bujumbura
Rose Hakizimana's mother and four
sisters were killed by Burundian Hutu rebels while they were housed in a camp
for ethnic Tutsis forced to flee their homes.
She remembers finding her mother's body by identifying her legs. For a full
year after the burial she had nightmares.
When people think of genocide in Africa, neighbouring Rwanda usually comes to
mind after the slaughter of some 800,000 Tutsi and moderate Hutus in 100 days in
1994.
What we are seeing now is a government that is not against
Hutu or Tutsi, but a government that targets individuals who don't agree with
their policies”
End QuoteRose HakizimanaBurundian political commentator
But over the years Burundi, which has a similar ethnic
make-up and tensions, has also faced killings by both Tutsi and Hutus, driving a
wedge into the fabric of the nation.
The most shocking was in 1972, when some estimate up to 300,000 Hutus were
massacred in six weeks.
Ms Hazikimana has kept an album documenting acts of genocide in 1993 in which
some 25,000 Tutsis are believed to have died, so that the crimes are not
forgotten.
She went on to become an MP in the transitional government that brought peace
to Burundi.
Now retired, she has a regular slot on local radio as a political commentator
and says ethnicity is no longer an issue in politics.
"If you look at the current situation in the country, though we have a
Hutu-dominated government that is not the problem," she told the BBC.
"What we are seeing now is a government that is not against Hutu or Tutsi,
but a government that targets individuals who don't agree with their policies."
Her comments reveal how Burundi is now coping with ethnicity far better than
its better-known neighbour.
1965: More than 80 leading Hutu politicians shot after an abortive coup
1972: Between 150,000 and 300,000 mainly Hutus killed following an
insurgency
1988: Between 15,000 and 25,000 mainly Hutus killed after violence in the
north
1993: Some 25,000 Tutsis killed following the assassination of Hutu
President Melchoir Ndadaye by Tutsi soldiers
Rwanda:
1959: Thousands of Tutsis killed following a Hutu revolt
1963: Between 10,000 and 20,000 Tutsis killed after an incursion by
pro-monarchist Tutsi rebels based in Burundi
1991: Hundreds of Bagogwe - a Tutsi subgroup - killed over several months in
the north-west following an invasion by Tutsi rebels based in Uganda
1994: 800,000 mainly Tutsis and moderate Hutus killed in 100 days
1995: Rwanda's new armed forces attack Kibeho camp housing Hutu refugees -
some 5,000 people killed and more than 20,000 others died after fleeing the
camp
1996: Rwanda troops invade Zaire, now DR Congo, to pursue Hutu militia
involved in the genocide. Thousands of Hutus killed
This may be down to the Arusha Peace Accord, brokered by
South Africa's former President Nelson Mandela.
Signed in August 2000, the ceasefire led to talks that eventually helped end
the long, drawn-out conflict and got politicians from both sides of the ethnic
divide talking - it put ethnicity centre stage.
The accord recognised the tensions between the dominant Tutsi minority and
the Hutu majority as a catalyst to the conflict and came up with a 60-40 formula
of proportional representation.
Two years ago, ex-rebel Godefroid Niyombare became the first ever Hutu army
chief of general staff.
According to President Pierre Nkurunziza - a former rebel Hutu leader who
came to power in the first democratic elections in 2005 - this new-look army is
a testimony to reconciliation efforts.
"The base of our problems during former times were the army and the police -
now we have both ethnic groups represented," the president told the BBC.
Such a comment from Rwanda's President Paul Kagame would be unthinkable, as
tribal references are banned and considered tantamount to a denial of the
genocide - a criminal offence.
A Rwandan opposition leader is currently on trial for propagating ethnic
hatred because she has questioned why the official memorial to the 1994 genocide
only mentions the Tutsis killed, not the Hutu victims.
Mr Kagame says such strong-arm tactics are needed to prevent a repeat of the
massacres, but his critics say he is only keeping a lid on the tensions, which
could boil over. Ethnic jokes
In Burundi where it was once also a taboo to mention ethnicity, politicians
now make light of their ethnic differences in public debates, something analysts
say has contributed to the healing process.
Rebuilding and reshaping Rwanda
For example, traditionally Tutsis, who reared cattle, were thought to drink
more milk than Hutus, who were farmers.
So a Tutsi might jest with a Hutu colleague who reaches out for the milk
during an office tea-break: "You Hutus, you want to drink all the milk now."
Such banter, even in a bar, would be careless talk in Rwanda that could land
you in jail.
This is not to say that Rwanda is not witnessing some reconciliation.
The show village of Bugesera, outside the Rwandan capital of Kigali, is an
example.
Set up by a non-governmental organisation to show that enemies can live as
neighbours, it has been Laurence Niyongira's home for the last 10 years.
The killers of her family are not only her friends, but people she now refers
to as family.
Her neighbour's husband organised the killing of her family - a fact both
families cannot hide.
"[But] we have reached reconciliation and have forgiven each other," she
admits - words often repeated from other Bugesera residents. Truth and reconciliation
Rwanda has also made much more progress when it comes to seeking justice for
genocide victims, setting up community "gacaca" courts which tried close to two
million people for their involvement.
Unlike Rwanda, Burundi does not
have that many visible massacre memorials
In contrast Burundi has been slow in setting up national institutions to deal
with the crimes committed.
But the government hopes that once there is funding and systems in place they
will be able to let justice take its course - a Truth and Reconciliation
Commission has been promised.
And unlike its neighbour, the symbols of reconciliation are not many or that
obvious.
There is a mausoleum in the capital, Bujumbura, to remember Melchior Ndadaye
- the first democratically elected Hutu president, who was assassinated in
October 1993 by Tutsi soldiers.
Melchior Ndadaye was Burundi's
first democratically elected Hutu president - assassinated in 1993
A similar monument honours independence hero Louis Rwagsore, a royal prince
who won respect from both the Tutsi and Hutu communities.
But the ethnic divide that Burundi experienced - with Tutsis dominating every
sphere of society and neighbourhoods split along ethnic lines - is all but
over.
Burundians consider themselves to be free and are confident that their
country will not be torn apart by ethnic enmity again.
Human rights bodies like Amnesty International laud Burundi for embracing
democracy and having a much better grasp of it than Rwanda.
For Ms Hazikimana, who knows that the former rebels now in power killed her
family, the root cause of the misdeeds of Burundi's past was never
ethnicity.
"Burundians never hated each other. It was all about politics and done for
political gain. Politicians used money to convince people to carry out crimes
and killings."
WAZIRI Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi (57), amefariki dunia juzi usiku mjini Brussels, Ubelgiji alikokuwa akitibiwa.Taarifa iliyotangazwa na Televisheni ya Taifa ya Ethiopia, imeeleza kuwa Zenawi alifariki dunia saa 5:15 usiku.
Kutokana na Katiba ya nchi hiyo, nafasi ya kiongozi huyo mwenye historia ya kipekee nchini humo, itashikiliwa na Naibu Waziri Mkuu, Hailemariam Desalegn.
Mpaka anakutwa na mauti, hakuna taarifa zozote ambazo zilithibitisha hasa ugonjwa uliosababisha kifo chake. Kiongozi huyo alikuwa madarakani tangu mwaka 1991 alipompindua Mengistu Haile Mariam. Hata hivyo, taarifa ambazo hazijathibitishwa zinaeleza kuwa Zenawi alikuwa akisumbuliwa na uvimbe kwenye ubongo.
Habari kwamba kiongozi huyo wa zamani wa vita ya msituni alikuwa mgonjwa, zilianza kusambaa tangu aliposhindwa kuhudhuria mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika, Addis Ababa mwezi uliopita. Tangu kipindi hicho, wasiwasi ulitanda nchini humo hasa alipochukua likizo. Uvumi huo ulipingwa na Msemaji wa Serikali ya Ethiopia, Bereket Semon ambaye amekuwa akirejea kauli yake hiyo ya kupinga uvumi mara kwa mara.
Msemaji huyo amekuwa akisisitiza kuwa afya ya kiongozi huyo haikuwa mbaya kama ilivyokuwa ikidaiwa na kusisitiza kwamba alichukua likizo baada ya kupewa ushauri na daktari. Zenawi atakumbukwa kwa sera yake ya kiutawala ambayo ilijulikana kama ‘shirikisho la makabila,’ iliyoyafanya makabila mbalimbali ya nchi hiyo kujitawala yenyewe, lakini bado utawala wake uliendelea kuwa na nguvu.
Zenawi alikuwa mwanasiasa mjanja ambaye aliipenda siasa tangu akiwa kijana mdogo. Alitokea kwenye kundi maarufu la TPLF, ambalo lilikuwa likiongoza mapambano dhidi ya utawala wa kijeshi wa Ethiopia miaka ya 1970 na 1980.
Kiongozi huyo aliyeacha watoto watatu, aliwahi kutajwa kama mmoja wa viongozi wenye ushawishi mkubwa na ambaye utawala wake ulikumbwa na utata barani Afrika.
Wakati Zenawi anafariki dunia, Naibu Waziri Mkuu, Desalegn alikuwa katika mkutano China. Katika hatua nyingine, Serikali ya Ethiopia ilisema kwamba haitafanya uchaguzi kwa kuwa viongozi waliopo wako imara.
Simon alisema kwa sasa Serikali inashughulika na mazishi ya kiongozi huyo na kwamba mwisho wake wa kuwa madarakani kwa mujibu wa katiba ni mwaka 2015.
“Hakuna wasiwasi wowote na uongozi uliopo madarakani kwani chama kilichopo madarakani kipo katika hali nzuri na kina viongozi imara,” alisema.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepata pigo baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, kutengua matokeo ya ubunge Jimbo la Igunga yaliyompa ushindi mgombea wake, Dk Dalaly Peter Kafumu.Dk Kafumu aliibuka mshindi katika uchaguzi mdogo uliofanyika Oktoba 2, mwaka jana kuziba nafasi ya Rostam Aziz ambaye alijiuzulu kwa madai kwamba anaachana na siasa chafu ndani ya CCM.
Uchaguzi huo ulikuwa wa ushindani mkubwa kati ya Dk Kafumu na aliyekuwa mgombea wa Chadema, Joseph Kashindye ambaye hakuridhishwa na mwenendo wa uchaguzi huo, hivyo kuamua kupinga matokeo hayo mahakamani. Kesi hiyo ilifunguliwa Machi 26, mwaka huu.
Akitoa hukumu hiyo, Jaji Mary Nsimbo Shangali alisema Mahakama ilipokea malalamiko 15 ambayo yaliridhiwa na pande zote mbili, lakini baadaye yakaongezwa madai mengine mawili hivyo kufikia 17. “Madai yaliyopokewa na Mahakama ni 17 na kati yake imethibitisha madai saba,” alisema Jaji Shangali katika hukumu hiyo.
Mbali na Dk Kafumu, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uchaguzi walikuwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Igunga aliyetangaza matokeo hayo.
Dk Kafumu akizungumza na Radio One jana alisema tangu awali, hakuwa na imani na jaji aliyesikiliza kesi hiyo. Alisema hana mpango wa kukata rufaa, bali anawaachia viongozi wa CCM kufanya hilo.
Alisema baada ya ubunge wake kutenguliwa, anaendelea na shughuli zake za madini kwa kuwa ni mtaalamu wa sekta hiyo... “Ndugu mwandishi karibu Singida, mimi narudi kuendelea na shughuli zangu za madini.” Sababu za kutengua matokeo
Alisema hoja zilizothibitishwa na Mahakama na ambazo zimetumika kutengua matokeo hayo ni pamoja madai kwamba Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli alitumia nafasi yake ya uwaziri kutoa ahadi ya ujenzi wa Daraja la Mbutu ambalo lilikuwa ni moja ya kero kubwa kwa wananchi wa Jimbo la Igunga.
Dk Magufuli akiwa katika moja ya kampeni za uchaguzi huo, alitumia nafasi ya uwaziri kwa kuwatisha wapigakura wa jimbo hilo kwa kusema kama hawatamchagua mgombea wa CCM, watawekwa ndani.
Jaji Shangali aliendelea kueleza kuwa Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage alitangaza kuwa mgombea wa Chadema alikuwa amejitoa katika uchaguzi huo, jambo ambalo Mahakama imeridhishwa na ushahidi uliokuwa ukitolewa.
Jaji Shangali alitaja hoja nyingine iliyotumika kufuta matokeo hayo kuwa ni kauli ya Imamu Swaleh Mohamed wa Msikiti wa Ijumaa Igunga, kuwatangazia waumini wa msikiti huo kuwa wasikichague Chadema, kwa kuwa baadhi ya viongozi wake wamemdhalilisha Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario.Alisema hoja nyingine ni Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama kudai kuwa Chadema kilileta makomandoo katika uchaguzi huo na kupanga kuuvuruga.
Hoja nyingine ambayo Jaji Shangali aliikubali ni ugawaji wa mahindi ya kuwawezesha wakazi wa Igunga kukabiliana na njaa wakati wa uchaguzi huo kwamba ulitumiwa vibaya na baadhi ya wanasiasa kuwashawishi wananchi wawapigie kura.
Jaji huyo alihoji iwapo wakazi wa Jimbo la Igunga walikuwa na njaa sana wakati wa uchaguzi huo kiasi cha viongozi wa Serikali kuona kuwa ulikuwa wakati mwafaka wa kugawa mahindi hayo.
Kuhusu hoja ya upande wa utetezi kwamba mgombea wa Chadema, Kashindye alipaswa kupeleka malalamiko hayo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), alisema siyo ya msingi yanayoweza kumzuia mlalamikaji kupeleka malalamiko hayo katika Mahakama Kuu na hakuna kifungu chochote kinachomzuia mlalamikaji kufanya hivyo.
Kutokana na hali hiyo, Jaji Shangali alisema kuanzia sasa Jimbo la Igunga lipo wazi na kwamba: “Milango iko wazi kwa walalamikiwa kukata rufaa ikiwa hawajaridhika na uamuzi.”
Hali ya usalama katika mahakama hiyo ilikuwa imeimarishwa, huku wafuasi wa Chadema wakiwa wengi zaidi na wakionekana kuwa na furaha hasa baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo.
Dk Slaa, Nape wazungumza Baada ya hukumu hiyo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema: “Mahakama imedhihirisha yale ambayo tumekuwa tukisema kila wakati kwamba CCM inatumia mabavu.”
Alisema anashukuru Mahakama kwa kutoa haki na kukubaliana na Chadema kuwa CCM iligawa vyakula kwa wananchi ili kuwashawishi wawapigie kura.
Pia alisema kwamba imeudhihirishia umma kauli kwamba CCM kinatumia vibaya rasilimali za nchi katika mambo ya siasa akitoa mfano wa mawaziri kuwalazimisha watu wawachague wagombea wao.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema alikuwa hana taarifa kuhusu hukumu ya kesi hiyo. Hata alipopata taarifa kuhusu matokeo hayo, alisema atakuwa tayari kuyazungumzia pindi akiyapata kutoka katika mfumo wa chama chao.“Siwezi kuzungumzia matokeo ya hukumu unayoniambia wewe. Nitakuwa tayari pindi nitakapoyapata rasmi kutoka kule Igunga (CCM),” alisema Nape.
Uchaguzi Oktoba 3 mwaka jana Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Igunga, Magayane Protas alimtangaza Dk Kafumu kushinda ubunge kwa kura 26,484 akifuatiwa na Kashindye ambaye alipata kura 23,260, huku Leopold Mahona wa CUF akipata kura 2,104.
Ushindi huo wa CCM ulihitimisha mojawapo ya michuano mikali ya kisiasa nchini ambayo Chadema, CUF na CCM vilionekana kufukuzana vikali. Dk Kafumu kabla ya nafasi yake hiyo alikuwa Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini.
Ushindi wa CCM katika jimbo hilo ulikuwa ni pigo kubwa kwa Chadema kwani ulikifanya chama hicho kushindwa kuibuka na ushindi hata katika mazingira ambayo kilitarajiwa au kuonekana kukubalika zaidi. Chaguzi nyingine ambazo Chadema kilidhaniwa kushinda ni zile za Babati, Busanda na Biharamulo ambako kote CCM kilitetea viti vyake. Nyongeza na Leon Bahati.
“Nimeteseka sana, nimetengwa sana, na
nimeumizwa sana pamoja na kuwaumiza wenzangu, yote haya ni kwa sababu ya
matumizi ya madawa ya kulevya, pombe kali hasa viloba hadi akili yangu
ikaharibika nikajikuta nimekuwa mwehu nikitembea hovyo mitaani, kutukana na
hata kupigana, hakika kwa sasa ninalo funzo kwa vijana wenzangu”
Hii ni Kauli
ya kijana mmoja kutoka Dar es salaam ambaye sasa anatibiwa na kutunzwa katika
kijiji cha Marumba wilayani Kasulu ambako alifikishwa na ndugu zake miezi
kadhaa iliyopita baada ya kuugua ugonjwa wa akili na sasa akili yake japo kwa
mwendo wa kinyonga inaanza kurejea.
Matumizi ya
pombe kali VILOBA ni moja ya chanzo cha vijana wengi kuwa na matatizo ya akili
na hata kupoteza afya ya mwili pia, si ajabu kuwakuta wapenzi na wanywaji wa
viloba wakiwa maumbile yaliyokonda na kuchoka, kuungua midomo na hata kunyonyoa
nywele, kukosa uwezo wa kufikiri na mwili kukosa nguvu
Si ajabu
kumkuta kijana mpiga viloba akitetemeka mwili kila wakati anaposhika au kubeba
chochote mikononi mwake, wengu wanashindwa hata kufanya kazi yoyote
Taifa limepoteza
nguvu kazi kutokana na viloba na ulevi mwingine wa kupindukia pamoja na
matumizi ya madawa ya kulevya,
Hii ndiyo sababu shirika la kitawa la BROTHERS OF CHARITY
liliamua kuanzisha kitengo cha afya ya akili na kuanza kutoa tiba ya magonjwa
hayo pamoja na matunzo ya kijamii na kisaikolojia kwa wagonjwa wa akili maarufu
kama WEHU.