Source:SR/Chami
Ed:
BM
Date: Feb 11/02/2013
SINGIDA
Wito umetolewa kwa wananchi wa mkoa wa Singida kufuata utii
wa sheria bila shuruti na kuwa makini na fedha bandia zinazoingia ndani ya mkoa
huo
Kamanda
wa polisi mkoa wa singida ACP Linus Sinzumwa ametoa wito huo leo, wakati akitoa
taarifa za matukio ya wiki kwa waandishi
wa habari ofisini kwake. Ametaja ukio la
mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Hassan Kisuwa kukamatwa na fedha bandia katika
maeneo ya Singida Motel mkoani Singida
Kamanda
Sinzumwa amesema kuwa mshtakiwa alikutwa na noti mbili za shilingi elfu tano kila
moja, zikiwa na namba B 40012036 na nyingine ikiwa na namba DT 1547949 na kusema
kuwa mtuhumiwa anatarajiwa kifikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika
Kamanda
Sinzumwa amelitaja tukio jingine ni la mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Juma Husein
mwenye umri wa miaka 50, kujeruhiwa kwa kukatwa mapanga na mtu aitwae John
Shayo katika maeneo ya mwenge, na kwamba chanzo cha tukio hilo hakijajulikana na
mshtakiwa amekamatwa kwa mahojiano zaidi
Aidha
ameendelea kwa kutaja tukio jingine lililotokea tarehe 8 ambapo watu watatu ambao
ni John Lewala, Eliasi George, na Mateo
Leornad walijeruhiwa kwa kukatwa mapanga katika eneo la Unyamikumi kwa kile kilichotajwa
kuwa ni mgogoro wa ardhi na kwamba watu watano wamekamatwa kwa kuhusikana tukio
hilo ambao ni Christopher Kimoteo, Emanueli Edward, Hamisi Joseph, Agustino
Daniel, na Edward Simbu
Kamanda amesema jumla ya matukio mawili yameripotiwa kwa wiki
iliyopita na moja la siku ya leo. Amesema ni vyema uhalifu unapotokea kutoa taarifa
mapema kwa vyombo vya sheria na si kujichukulia sheria mkononi
Source:SR/
Ed:
BM
Date: Feb 11/02/2013
SINGIDA
Wafanyabiashara ndogo ndogo
wa soko kuu la manispaa ya Singida wameiomba serikali kuwapatia mikopo isiyokuwa
na riba ili kufikia malengo wanayoyahitaji.
Baadhi ya wafanyabiashara
wa soko hilo wakati wakizungumza na Standard radio.
Akizungumza kwa niaba
ya wafanya biashara wenzake, Bw. Omari shabani amesema chanzo hasa cha kuzorota
kwa biashara zao ni kutokana na kudaiwa riba, pindi wanapochukua mikopo kitu
kinachopelekea kupata hasara siku hadi siku.
Vilevile ameendelea kusema Serikali iangalie suala
la ushuru kwani hakuna kiwango
maalum cha kulipia ushuru, badala
yake wamekuwa wakipandishiwa ushuru mara kwa mara.
Naye Bw Shabani Saidi
ambaye pia ni mfanyabiashara wa soko hilo ameiomba serikali kuongeza kiwango
cha mikopo ili kukuza biashara zao
Sambamba na hayo wamesema
wafanyabiashara washirikiane na kuunda kamati maalum ya kusimamia biashara zao
ili kuhakikisha wanapata haki zao.
Source:SR/
Ed:
BM
Date: Feb 11/02/2013
SUMBAWANGA
Mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Mkoe kata ya Nyangalua ambaye ni
mlemavu wa ngozi Albino, amevamiwa nyumbani kwake na kukatwa mkono na watu
wasiojulikana alfajiri ya leo na kutoweka nao kusikojulikana.
Akizungumza mapema leo, Daktari anayemuhudumia mama huyo hosipitali ya
Rukwa Dk, Rashidi Lugisha, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema
majeruhi huyo alifikishwa hospitalini hapo akiwa amepoteza fahamu kutokana na
kuvuja damu nyingi.
Aidha, Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Rukwa, Jacob Maluwanda
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema tayari wameshafika kwenye eneo
la tukio, umbali wa kilomita sitini
kutoka Sumbawanga mjini.
Amesema upelelezi unaendelea ili kuwabaini watu waliotenda unyama huo
na kuahidi kutoa taarifa endapo uchunguzi ukikamilika.
Source:SR/
Ed:
BM
Date: Feb 11/02/2013
MWANZA
Mwanachuo wa chuo kikuu
cha SAUT kilichopo Nyegezi Malimbe mkoani Mwanza amevamiwa na watu wanne
waodhaniwa kuwa ni majambazi na kumpora baadhi ya vitu vyake.
Kamanda wa polisi mkoa
wa Mwanza Ernest Mangu amesema kuwa
tukio hilo limetokea jana majira ya saa 9 usiku eneo la Nyegezi Malimbe Kata ya
Mkolani wilaya ya Nyamagana.
Amemtaja mwanachuo
aliyeporwa vitu vyake kuwa ni Catherine Antony ambapo
majambazi hao wakiwa na mapanga, na kupora kompyuta Laptop aina ya HP na simu mbili aina ya Samsung
Galaxy vyote vikiwa na thamani ya shilingi
milioni moja na laki moja na elfu
tisini.
Kamanda huyo amesema,
jeshi la polisi mkoani Mwanza linaendelea kuwasaka watu waliohusika na tukio
hilo.
Wakati huo huo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Zacharia
Stephano anayekadiriwa kuwa na umri kati
ya miaka 20 na 25 makazi yake
hayakujulikana, ameuawa na wananchi baada
ya kutuhumiwa kuiba betri ya gari.
Kamanda Mangu amesema
tukio hilo limetokea jana majira ya saa kumi na moja alfajiri maeneo ya
Furahisha kata ya Kirumba mkoani Mwanza.
Amesema kuwa marehemu ameuawa
baada ya kutuhumiwa na wananchi kuwa alikuwa akiiba
betri ya gari yenye namba za usajili T.265 AUD aina ya Scania. Mwili wa
marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa Sekou Toure kwa uchunguzi zaidi.
Jeshi la polisi
linamshikilia Slaji Ismail mwenye umri wa miaka (38) mkazi wa Bunda kwa
mahojiano kuhusiana na tukio hilo.
Source:SR/Hawa
Ed:
BM
Date: Feb 11/02/2013
SINGIDA
Wazazi wametakiwa
kutowaficha watoto wao wenye ulemavu badala yake wawapeleke wapate elimu
itakayowasaidia katika maisha yao.
Hayo yamesemwa na mratibu wa
mafunzo ya elimu ya ujasiriamali mkoani Singida Bi Amina Abubakari Msaghaa wakati akizungumza na
standard Redio leo ofisini kwake.
Mratibu huyo amesema walemavu wakipatiwa elimu watajua jinsi gani waendeshe biashara zao,
vilevile njia za kujikinga na maambuzi ya VVU na kuzuia mimba za utotoni.
Bi Amina pia ametoa
wito kwa jamii kutoa ushirikiano kwa walemavu kuhusu suala la kupata elimu ya nadharia na vitendo.
Source:SR/
Ed:
BM
Date: Feb 11/02/2013.
MUSOMA
Watu wasiojulikana wamemuua
kwa kumnyonga shingo mwanamke mmoja kwa kutumia kanga yake katika eneo la
mgarajabo manispaa musoma mkoani Mara
Kamanda wa polisi wa
mkoa wa mara Absalom Mwakyoma amesema tukio hilo limetokea hivi karibuni jirani
na eneo ambalo miaka mitatu iliyopita watu 17 familia moja waliuwawa kwa
kuchinjwa na watu wasiojulikana
Mwakyoma amesema kando
ya mwili wake zimekutwa nguo za ndani zikiwa zimechanwa na dumu la kuchotea
maji likiwa mita 20 tokea mwili ulipokuwa, nywele zake zilikutwa
zimefungwa kwenye kijiti kichakani huku
khanga ikiwa shingoni ulimi wake ukiwa nje na kinyesi
pembeni.
Aidha amesema kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi, sambamba na
kuwasaka watu waliohusika na kitendo hicho cha kikatili. Ametoa wito kwa
wananchi wataokuwa na taarifa za
watu waliohusika na mauaji hayo, wazitoe kwa siri kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili sheria ichukue mkondo wake.
Source:SR/Chami
Ed:
BM
Date: Feb 11/02/2013
SINGIDA
Wanawake wawili wakazi
wa majengo tarafa ya Itigi wilayani Manyoni mkoani Singida, wameachiwa huru na
mahakama kwa miezi kumi na mbili kwa sharti la kutotenda kosa lolote.
Mahakama kuu kanda ya
kati, imewaachia huru wanawake hao waliokuwa wakikabiliwa na shtaka la
kumtorosha mtoto wa miaka mitano na kumtupa kwenye kisima cha maji.
Akisoma shtaka hilo,
wakili wa serikali Bw. Hemed Seif amesema washtakiwa walitenda kosa hilo tarehe
kumi na saba mwezi Machi mwaka 2005 katika eneo la majengo, tarafa ya Itigi.
Walioachiwa huru na
mahakama hiyo ni Bi. Chiku Mlowezi na Mwadawa Hamis, ambao wanadaiwa siku ya
tukio walikwenda nyumbani kwa Hawa Hamis na kumkuta mtoto akicheza na watoto
wenzake na kumchukua wakidai kumpeleka kwa kinyozi kunyoa nywele, na kwenda
kumtumbukiza kisimani.
Mtoto huyo aliokolewa
na wasamaria wema waliompeleka hospitali kupata matibabu na alipopona aliwataja
watu walitenda kosa hilo. Washtakiwa wamekiri kutenda kosa hilo na Jaji Laurent
Kaduri ametoa hukumu ya kesi hiyo.
Source:AFP
Ed:
BM
Date:
11 February 2013.
KHARTOUM
Mtaalam wa haki za
binadamu wa Umoja wa mataifa amesema idara ya usalama nchini Sudan,
inawashikilia viongozi wa upinzani bila kuwafungulia mashtaka na kutowapatia
huduma za afya wanazohitaji.
Mtaalam huyo wa haki za
binadamu wa Umoja wa mataifa Mashood
Adebayo Baderin, ameeleza kusikitishwa kutokana na kukamatwa kwa viongozi wa
upinzani na watu wengine, ingawa hakutoa maelezo zaidi.
Ameitaka serikali ya
Sudan kuwaachia huru au kuwafungulia mashtaka kwa kufuata vifungu vya sheria za
nchi hiyo na kuwafikisha mahakamani.
Taarifa iliyotolewa na
Umoja wa mataifa, imeitaka serikali ya Sudan kukomesha unyanyasaji unaofanywa
na idara ya usalama, ambayo imekuwa ikizuia maandamano na kutovipa uhuru vyombo
vya habari.
Sudan imekuwa ikikumbwa
na maandamano ya mara kwa mara yanayotekelezwa na watetezi wa demokrasia, wanaotaka kufanyika mapinduzi dhidi ya rais
Omar al-Bashir ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1989. Mapinduzi kwa njia
ya maandamano yamewaondoa madarakani viongozi wa nchi za Misri, Libya na
Tunisia.
Source:AFP
Ed:
BM
Date:
11 February 2013.
DAMASCUS
Mwakilishi
maalum wa Umoja wa mataifa katika nchi za Kiarabu amemtaka kiongozi wa waasi
nchini Syria kufanya mazungumzo na serikali ya nchi hiyo, kufuatia mapigano
makali kutokea jana kati ya waasi na vikosi vya serikali.
Mwakilishi
huyo maalum wa Umoja wa mataifa Bw. Lakhdar Brahimi amekutana na kiongozi wa
upinzani Ahmed Moaz al-Khatib katika mji
mkuu wa Misri, Cairo na kumtaka afanye mazungumzo na serikali ya nchi hiyo.
Shirika
la kutetea haki za binadamu nchini Syria, limekuwa likikusanya taarifa kutoka
hospitali za kiraia na kijeshi, limesema watu hamsini wamekufa jana katika
ghasia zilizotokea katika nchi nzima.
No comments:
Post a Comment