Raia mmoja nchini Kenya ameiomba mahakama kuzuia waangalizi wa uchaguzi
kutoka Muungano wa Ulaya kuingia nchini humo kwa lengo hilo kwa madai kuwa
wanapendelea baadhi ya wagombea.
Katika
kesi iliyowasilishwa mahakamani na mwanaharakati Samson Ojiayo, ameitaka mahakama kuzuia waangalizi hao kwa Misingi
kuwa wanapendelea upande mmoja, huku nchi zao tayari zikiwa zimewaonya wakenya
dhidi ya kumpigia kura mgombea Uhuru Kenyatta.
Balozi
wa Marekani kuhusu maswala ya Afrika Jonny Carson, amewataka wakenya kufahamu
athari za kuchagua baadhi ya wagombea waliojitokeza kuwania urais katika
uchaguzi wa Machi tarehe 4.
Mahakama
imeelezwa kuwa waangalizi hao tayari wameelezea kutompenda Uhuru Kenyatta na mgombea
mwenza wake, William Ruto, kwa kutishia kwa ikiwa wawili hao watashinda
uchaguzi huo , wakenya wajiandae kwa athari zake.
Mwanaharakati
huyo ameitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka, IEBC, kubatilisha idhini ambayo
tayari imetolewa kwa waangalizi hao kutoka Marekani, Uingereza na Muungano wa
Ulaya ambao tayari wamewasili nchini humo.
Wanapingwa
zaidi kwa kupendelea upande mmoja na ikiwa ni hivyo watakuwa wanahujumu misingi
ya uhuru na demkokrasia ya Kenya.
Jaji
Eric Ogolla, anayesikiliza kesi hiyo atatoa uamuzi Februari 18 mwaka huu.
Source:SAPA
Ed:
BM
Date:
15 February 2013.
KINSHASA
Zaidi ya wakimbizi elfu nane na mia tano
wamekimbia kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati na kuingia katika Jamhuri ya
kidemokrasi ya Kongo wakihofia mashambulizi kutoka kwa waasi wa Seleka.
Shirika la kuratibu misaada la Umoja wa
mataifa OCHA limesema wakimbizi wengi ni watoto, ambao wamepotezana na wazazi
wao. Mashirika ya Umoja wa mataifa yameanza kufanya tathimini ya mahitaji ili
kutoa misaada kwa wakimbizi hao ambao hadi sasa wanahifadhiwa katika familia za
raia katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.
Waasi wa kundi la Seleka wanaipinga
serikali ya Rais Francois Bozize tangu mwezi Desemba mwaka jana, ingawa
viongozi wan chi za Afrika ya kati wamesuluhisha mgogoro na kufikia mkataba wa
amani uliosainiwa Januari 11 mjini Libreville nchini Gabon.
Chini ya mkataba huo, Waasi wa Seleka
waliahidiwa kupewa nyadhifa katika serikali ya Umoja wa kitaifa.
Source:
AFP
Ed:
BM
Date:
15 February 2013.
SAO PAULO
Shirika la
kutetea haki za waandishi wa habari duniani limesema idadi ya waandishi
waliofungwa jela katika mazingira yasiyoruhusu uhuru wa vyombo vya habari
imepanda mwaka 2012.
Shirika
hilo Committee to Protect Journalists CPJ
lililo na makao makuu mjini New York nchini Marekani, limesema katika
taarifa yake ya mwaka kuwa waandishi wa habari mia mbili thalathini na mbili
wamefungwa jela mwaka jana, na kwamba idadi hiyo imepanda tangu lifanye
tathimini ya kwanza mwaka 1990.
Ripoti ya
shirika hilo imesema waandishi wa habari sabini wameuawa wakiwa katika
mazingira ya kazi mwaka 2012, ikiwa ni ongezeko la asilimia arobaini na tatu,
ikilinganishwa na mwaka 2011.
Ripoti hiyo
imetaja nchi kumki zilizo katika kiwango cha juu katika mauaji ya waandishi wa habari kuwa ni Pakistan,
Somalia, na Brazil. Nchi nyinine ni Ecuador, Uturuki, Russia, Ethiopia, Vietnam
Iran na Syria.
No comments:
Post a Comment