Source:
E
Ed:Im
Date February 16,2013
SINGIDA
Wito umetolewa kwa
serikali na jamii kutambua mchango wa vikundi
vinavyochipukia katika jamii ili
kuharakisha maendeleo
Akiongea na rdio
standard mwalimu w akikundi cha saa cha
sanaa Gineri Bw.Henry Lyimo amesema kuwa
baadhi ya watu wamekuwa na mtazamo tofauti kuhusu vikundi hivyo pamoja na kutoonyesha ushirikiano pale
unapohitajika.
Aidha amesema jamii ni
lazima itambue umuhimu wa vikundi kwani vinasaidia kuelimisha pamoja na kusaidia jamii kuondokana na
kuzurura bila kazi na pengine kusababisha baadhi yao kujiingiza kwenye vitendo
viovu.
Aidha ameikumbusha serikali
kuvipa msaada pindi viapohitaji ili viweze kufanya kazi kwa ufanisi na kuondokana
na umaskini
Source: E
Ed:Im
Date February 16,2013
MWANZA
Halmashauri
ya wilaya ya magu mkoani mwanza kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi ya wilaya
hiyo imefanikiwa kufanya utambuzi wa watu wenye ulemavu wa ngozi albino pamoja
na kuwapatia ulinzi kwa kutoa elimu kwa jamii dhidi ya imani potofu kwamba
viungo vya albino vinaleta utajiri.
Mkurugenzi
mtendaji wa wilaya ya Magu, Mwl. Naomi Nko amesema hadi sasa watu wenye ulemavu
wa ngozi Albino katika halmashauri ya wilaya ya Magu imetambuliwa kuwa ni mia
moja na nane kati yao wanawake ni arobaini na saba na wanaume ni sitini na
mmoja.
Amesema
mbali na kuwatambua walemavu hao, pia halmashauri imeenda mbali zaidi kwa
kuwapatia huduma za afya walemavu hao ikiwa ni pamoja na kuwapatia mafuta
maalumu ya kulainisha ngozi na kuwapelekea mahali walipo kupitia ofisi ya
ustawi wa jamii na uongozi wao.
Aidha
ameongeza kuwa halmashauli hiyo pia imeanzisha kliniki ya watu wenye ulemavu wa
ngozi katika hospitali ya wilaya ya Magu ambao wanafanyiwa uchunguzi katika
ngozi zao ili kubaini dalili za awali za saratani ya ngozi na kuwapatia rufaa
kwenda katika hospititali za rufaa ili kupata tiba mapema. EndS
Source: E
Ed:Im
Date February 16,2013
DODOMA
Waziri mkuu wa Tanzania
Mizengo Pinda amesema serikali itasaidia kutekelea mpango wa maboresho wa jeshi la polisi ili jeshi hilo liendelee
kuwa kimbilio la raia wema.
Waziri mkuu pinda
emetoa kauli hiyo wakati akifunga mkutano wa maafisa waandamizi wa jeshi la polisi
nchini katika ukumbi wa msekwa mjini
Dodoma.
Aidha amesema kuwa
jeshi la polisi linalohaja ya kuwashirikisha raia wakati wote, kuwapenda kwani
raia wanaweza kuwa chanzo kikubwa cha kukabiliana na vitendo vya uhalifu badala
ya kutengeneza mazingira yatayowafanya raia kuwa maadui wa polisi na hivyo
inawezekana endapo jeshi la polisi likijenga misingi ya mabadiliko ya kifikra
na kuwa na mtazamo mpya unaendana na wakati wa sasa.
Kwa upande wake waziri
wa mambo ya ndani ya nchi Dk Emmanuel Nchimbi amesema jukumu la ulinzi na
usalama wa raia ni la kila mtu takita jamii huku akitoa wito kwa jamii
kulisaidia jeshi hilo katika kukaribiana na vitendo vya uhalifu hapa.
Source: E
Ed:Im
Date February 16,2013
KIGOMA
Mwenyekiti halmashuri
wilaya ya kasulu mkoani Kigoma Bw
Wiliam Nusuli amesisitiza umuhimu wa elimu kwa watoto huku akiwakumbusha
wananchi kuendelea kuchangia mfuko wa maendeleo wa elimu wiyani kasulu.
Nusuli
ametaja malengo ya uanzishaji mfuko huo
wa maendeleo ya elimu wilayani kasulu kuwa ni pamoja na kuwasaidia kuwasomesha watoto wafamilia zisizokuwa na
uwezo ambao wameshindwa kuendelea
na masomo katika ngazi mbali mbali baada
ya kuchaguliwa.
Naye
afisa elimu Sekondari wialya ya Kasulu Patrick Athanas amewaagiza wakuu wote wa
shule za sekondari wilaya ya kasulu na buhigwe kuwasilisha taarifa ofisini
kwake kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao hawajaripoti hadi sasa shule
wazizopangiwa ifikapo February 28 ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya
wazazi na walezi wa wanafunzi hao.
Source: E
Ed:Im
Date February 16,2013
SERENGETI
Watu
wasiojulikana wakiwa na bunduki wilayani serengeti mkoani mara wamepora ng’ombe
zaidi ya mia moja waliokuwa wakichungwa ndani ya hifadhi ya Serengeti.
Kaimu
Kamanda wa Mkoa wa Mara Japheti Lusingu amesema watu hao wakiwa na bunduki
majira ya saa kumi na mbili jioni waliwatishia kuwauwa watu waliokuwa
wakichunga ng’ombe hao endapo wangepiga kelele na ndipo walifanyikwa kuwapora
ng’ombe hao na kutoweka nao pasipojulikana.
Lusinga
amewataja watu walioporwa ng’ombe hao waliokuwa wakichunga kuwa ni pamoja na
Suzana Juma mwenye umri wa miaka arobaini na mitatu na Nchama Peter wote wakiwa
wakazi wa kijiji cha bolanga ambapo ng’ombe hao ni mali ya Juma Kasimu na peter
Kasimu.
Jeshi
la polisi linafanya juhudi za kuwatafuta ng’ombe hao kwa kushirikiana na
wananchi ikiwa ni pamoja na kuwakamata watu waliohusika na uporaji huo.
HABARI ZA KIMATAIFA
Source: E
Ed:Im
Date February 16,2013
CAIRO
Naibu Mkuu wa chama cha
Uhuru na Uadilifu tawi la kisiasa la harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri
amesema kuwa wananchi wa Misri wana uwezo wa kulinda masanduku ya kura.
Usam al Ariyan Naibu
Mkuu wa chama cha Uhuru na Uadilifu ameeleza kuwa matamshi ya baadhi ya
shakhsia juu ya kuweko mahudhurio ya chini katika uchaguzi ujao yanaonyesha
kutohisi majukumu watu hao.
Amesema makundi yote yanapaswa kufanya juhudi
za kukidhi matakwa ya wananchi na kwamba yule anayelinganisha hali ya mambo ya
sasa ya Misri na ile ya kabla ya Januari 25 yuko katika ndoto.
Al Ariyan amesisitiza
kuwa wananchi wa Misri wana uwezo wa kulinda kura zao mbele ya udanganyifu wa
aina yoyote ile na kwamba hawatatoa mwanya wa kutokea jambo hilo.
Source:
E
Ed:Im
Date February 16,2013
KIGALI
Rwanda inalenga kupata mapato ya dola za
kimarekani milioni 317 kutoka kwa sekta ya utalii mwaka 2013.
Akieleza mpango huo kwenye mkutano na waandishi
wa habari, mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Rwanda RDB Clare Akamanzi
amesema nchi hiyo imeshuhudia ukuaji mkubwa wa setka ya utalii katika kipindi
cha miaka sita iliyopita.
Ameongeza kuwa ukuaji huo umetokana na
mazingira mazuri ya biashara ambayo yamesaidia kuimarisha soko na miundo mbinu
ya utalii.
Sekta ya utalii ilichangia sehemu kubwa zaidi
ya mapato ya fedha za kigeni ya Rwanda mwaka 2012 na kuongeza nafasi nyingi
zaidi za ajira nchini humo. Mwaka 2012 nchi hiyo ilipata dola milioni 281.8 za
kimarekani ikilinganishwa na mapato ya dola milioni 251.3 mwaka 2011.
Source: E
Ed:Im
Date February 16,2013
PRETORIA
Mwanariadha
mlemavu wa Afrika Kusini na nyota wa Olimpiki,Oscar Pistorius, amefikishwa
mahakamani akikabiliwa kwa madai ya kumuua mchumba wake baada ya kupigwa risasi
akiwa nyumbani kwa Pistorius mjini Pretoria.
Pistorius aliangua kilio baada ya viongozi
wa mashtaka kusema kuwa wataiambia mahakama kuwa mauaji ya mchumba wake
yaliyotokea nyumbani kwake yalikuwa yamepangwa.
baada ya kufikishwa maghakamani , wakala wa
Oscar alikanusha madai hayo vikali.
Ombi la dhamana ya mkimbiaji huyo limehairishwa
hadi Jumanne wiki ijayo,na yuko mbaroni kwa sasa.
Mwaka jana Pistorius alikuwa mwanariadha wa
kwanza mlemavu kuruhusiwa kushindana na wanariadha wengine wasio na ulemavu
kwenye micheco ya Olimpiki, kwam kutumia miguu bandia.
Source: E
Ed:Im
Date February 16,2013
HAVANA
Serikali ya Venezuela
imechapisha picha za mwanzo za rais wa taifa hilo Hugo Chaves anaekabiliwa na
ugonjwa wa saratani tangu afanyiwe upasuaji mjini Havana, nchini Cuba miezi
miwili iliyopita.
Picha hizo zilizotolewa zinaonamuonesha kiongozi huyo mwenye
umri wa miaka 58 akitabasamu lakini sura yake ikiwa kama imevimba.
Alikuwa amelala katika
kitanda cha hosiptali huku mabinti wake wawili wakiwa pembeni na mwenyewe
akisoma gazeti la serikali ya Cuba Granma.
Habari zinaesema kuwa rais huyo anakuwa katika wakati mgumu
katika kuzungumza lakini anaweza kuelewa mambo yanayoendelea
No comments:
Post a Comment