Ed:
BM
Date:
11 February 2013.
SINGIDA
Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mkoani Singida Bw. Manju Msambya amewataka walimu, viongozi na wananchi
Kutokutumia mali za shule kama Viti meza na baadhi ya vitendea kazi shuleni katika
mikutano ya hadhara.
Bw. Msambya amesema hayo
wakati akikagua shule ya sekondari Mwaru, iliyopo katika kata hiyo kabla ya kuelekea kwenye mkutano wa hadhara uliyofanyika
katika kijiji cha Kaugeri jana katika kata
ya Mwaru wilayani Ikungu mkoani Singida.
Bw. Msambya amesema kuwa
meza na madawati ni michango ya wazazi ili kuweza kuepukana na adha wanazopata
wanafunzi na walimu kama vitu hivyo havipo.
Aidha, Mkuu huyo wa wilaya ya Ikungi ameonya kuwa matumizi mabaya ya mali za taasisi kama
Shule, yatasababisha kushuka kwa kiwango cha elimu hapa nchini.
Source:SR/Limu
Ed:
BM
Date:
11 February 2013.
SINGIDA
Mkuu wa mkoa wa
Singida, Dk. Parseko Kone amemsimamisha kazi afisa ardhi wilaya ya Manyoni
pamoja na wasaidizi wake wawili kwa muda usiofahamika, ili kupisha uchunguzi
unaofanywa na tume maalum kuchunguza tuhuma mbalimbali zilizotolewa na wananchi
dhidi ya maafisa hao.
Afisa wa ardhi aliyesimamishwa
kazi wilayani Manyoni ni Bw. Leonard Msafiri na wasaidizi wake ni John Chima na
Kenedi Chigulu.
Mkuu huyo wa mkoa wa
Singida, amesema ameunda tume ambayo inawajumuisha kamanda wa polisi mkoa wa
Singida, mkuu wa mageraza mkoa, mwenyekiti wa baraza la ardhi mkoa, afisa ardhi
mkoa, mkuu wa wilaya ya Manyoni, TAKUKURU mkoa na afisa usalama mkoa.
Dk. Kone amesema tume
hiyo itafanya kazi kwa muda wa wiki moja na itatoa mapendekezo ya kuchukua ili
kumaliza kabisa malalamiko ya wakazi wa Manyoni mjini wanaowalalamikia maafisa
hao wa ardhi.
Hivi karibuni Dk. Kone alisimamisha kwa muda usiofahamika shughuli
zote za ugawaji wa viwanja Manyoni mjini, hadi hapo migogoro ya viwanja
iliyopo, itakapopatiwa majawabu yatakayoridhisha wakazi wa mji huo.
Pamoja na kusimamisha
shughuli za ugawaji viwanja, pia uendelezaji wa viwanja vyote kwa sasa unasimamishwa
kupisha tume maalum kufanya uchunguzi, juu ya migogoro ya viwanja.
Maafisa ardhi wa
halmashauri ya wilaya ya Manyoni wanadaiwa kusababisha migogoro mikubwa ya
ardhi, ikiwa ni pamoja na kupora ardhi za watu na kutolipa fidia.
Source:SR/Eliza
Ed:
BM
Date:
11 February 2013.
SINGIDA
Wito umetolewa kwa watahiniwa mtihani wa Kidato cha Sita wa
taifa ulioanza leo katika vituo vyote vilivyosajiliwa Mkoani Singida, kutoshiriki
udanganyifu kwa njia yeyote ile, ili
kuepuka kufutiwa matokeo yao.
Wito huo umetolewa na
afisa elimu wa mkoa wa Singida Bi. Fatuma Kilimia wakati akizungumza na
Standard Radio ofisini kwake.
Amesema kuwa mkoa huu una vituo 12 vilivyosajiliwa kwa
ajili ya mitihani hiyo ya taifa kidato cha sita inayoendelea nchi nzima ambapo
watahiniwa 843 wamesajiliwa kufanya mitihani hiyo.
Bi. Kilimia amesema
mitihani hiyo iliyoanza leo inatarajiwa kumalizika februari 27 mwaka huu. Amevitaja
vituo vilivyosajiliwa kuwa ni Mwenge, Dung’unyi, Kijota, Ilongero, Tumaini, Itigi,
Mwanzi, tumaini, Manguanjuki, Ikungi, Palloti, Rurumba na kituo binafsi cha
Mwenge.
Aidha amewataka wazazi kutoshiriki
katika udanganyifu wa mitihani kwa namna yeyote ile, bali wawaombee watoto wao
ili waweze kufanya mitihani kwa utulivu na wasipate vishawishi, kwani kufanya
hivyo kutapelekea kufutiwa matokea yao jambo ambalo ni aibu katika jamii na
taifa kwa ujumla.
Source:
Ed:
BM
Date:
11 February 2013.
DAR ES SALAAM
Ofisi ya mkaguzi na
mkaguzi wa hesabu za serika imekuwa ya kwanza kuunganishwa na mkongo wa
mawasiliano wa taifa.
Jumla ya ofisi kumi na
mbili za ofisi ya mkaguzi na mdhibiti wa serikali Rudovic Utto, zimeunganishwa
ili kusaidia utendaji kazi mzuri na wenye ufanisi na haraka zaidi
Mdhibiti na mkaguzi
huyo amesema mkongo huo uliogharimu kiasi cha bilioni mia nne arobaini na saba
utarahisisha mawasiliano tofauti na ilivyokuwa awali, ikiwa ni pamoja na kufanya mawasiliano
yanayojumisha watu wa mataifa na sehemu mbali mbali.
Aidha ameongeza kuwa
kiwango hicho cha fedha kimeweza kulipwa kwa awamu na kukamilisha fedha hizo.
Source:
Ed:
BM
Date:
11 February 2013.
MANYARA
Watu watatu wamejeruhiwa
kufuatia mapigano yaliyotokea baina ya wafugaji wakigombea maeneo ya malisho na
sehemu ya kunyweshea maji.
Mapigano hayo yametokea
katika kata ya Elachini ambapo wabarabaigi na wamang’ati walikuwa wakigombea
maeneo hayo.
Mkuu wa wilaya ya Mbulu
Anatori Choya amedhibitisha kutokea mapigano hayo ambapo majeruhi wamepelekwa
hospitali kwa matibabu na ulinzi umeimarishwa.
Aidha, ameongeza kuwa
chanzo cha ugomvi huo ni kutokana na baadhi ya maeneo kukosa mvua na
kusababisha kuwepo na ukame jambo lililopelekea wafugaji hao kugombea eneo dogo
la kulishia, ambalo lina malisho mazuri na kusababisha kila mtu kutaka kulishia
eneo hilo.
Source:SR/Irimina
& Simtovu
Ed:
BM
Date:
11 February 2013.
SINGIDA
Mratibu
wa mafunzo ya wanawake jamii, ameiomba serikali kuelimisha vijana juu ya elimu
ya ujasiliamali ili kupunguza ongezeko la vijana wa mitaani.
Mratibu huyo Bi. Amina Abubakar Msaghaa
wakati akizungumza na Standard radio ofisini kwake leo. Amesema mradi wa
ushonaji umeanza tangu mwaka 2009, ukiwa na lengo la kupunguza ongezeko la
vijana wasio na kazi, kuwaelimisha na kuwapatia ajira.
Hadi kufikia mwaka huu, mradi huo una
jumla ya wanafunzi mia mbili sabini na mbili walio kwenye mafunzo, wengine kumi
wameshindwa kuendelea na mafunzo kutokana na matatizo ya kijamii.
Aidha, amesema mafunzo hayo hutolewa kwa
walemavu, wajane, yatima na vijana wasiokuwa na uwezo wa kulipia gharama za
mafunzo husoma bure. Amesema mchango unaotozwa kama ada ni mdogo ambao
unamwezesha kila mtu kumudu gharama.
Ametoa wito kwa serikali isaidie
kuwaelimisha vijana kuhusu mafunzo hayo na kuishukuru serikali kwa kuwapa jengo
la kutolea mafunzo, pamoja na shirika la viwanda vidogo vidogo nchini SIDO kwa
kutoa vifaa vya kusindika vyakula.
Source:SR/
Ed:
BM
Date: Feb 11/02/2013.
SINGIDA
Wakazi watatu wa kijiji
cha Ughaugha (B) Manispaa ya Singida, wamenusurika kufa baada ya kushambuliwa
kwa majembe na kundi la watu 12 kwa kile kinachodaiwa kuwa ni ugomvi wa mashamba
Miongoni mwa wakulima
waliovamiwa hivi karibuni wakiwa shambani, ni pamoja John Leonard ambaye amewaambia
waandishi wa habari kuwa siku ya tukio wakiwa shambani, ghafla walivamiwa na
kundi la watu na kushambuliwa
Aidha amesema katika
tukio hilo inaonekana yeye alikuwa mlengwa kwani watu hao walianza kumkata kwa
hengo kwenye paji lake la uso, na kusababisha aanguke chini na kupoteza fahamu.
Watu hao wamelazwa
katika wodi namba tatu katika hospitali ya mkoa Singida, na hali zao
zinaendelea vizuri.
Uvamizi huo unadaiwa
kuwa umechangiwa kwa kiasi kikubwa na ugomvi wa kugombea shamba kati ya John na
Dk. Damas Simbu, anayefanyia kazi jijini Dar-es-salaam.
Source:AFP
Ed:
BM
Date:
11 February 2013.
BAMAKO
Mlipuko mkubwa umetokea
leo asubuhi katika mji wa Gao uliopo
kaskazini mwa Mali, saa chache baada ya mwanamgambo wa kiislam kushambulia kwa
risasi vikosi vya jeshi vya Ufaransa na Mali.
Vikosi vya Mali vimeliambia
shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa sauti ya mlipuko umesikika kutoka
kaskazini mwa mji wa Gao, katika kizuizi cha barabara ambako mashambulizi ya kujitoa muhanga
yalitokea mwishoni mwa wiki.
Ed:
BM
Date:
11 February 2013.
JUBA
Jeshi la Sudan kusini
limesema watu ishirini na nne wamekufa katika mapigano yanayoendelea katika
mpaka wa nchi ya Sudan na Sudan kusini.
Msemaji wa jeshi la
Sudan kusini Philip Aguer amesema vikosi vya jeshi vimewaua wapiganaji saba
wanaoungwa mkono na Sudan baada ya kuvuka mpaka unaotenganisha nchi hizo.
Jeshi la Sudan kusini
limeteka roli la jeshi la Sudan kaskazini lililokuwa likitumiwa na wapiganaji
katika mji wa Obed kwenye jimbo la Upper Nile kaska\zini mashariki mwa nchi
hiyo.
Katika shambulio jingine
katika mpaka huo, waasi wa Sudan’s People’s Liberation Movement SPLM
wanawatuhumu wanamgambo wanaoungwa mkono na Sudan kusini kwa kushambulia kijiji
na kuua watu kumi na saba.
Ed:
BM
Date:
11 February 2013.
BEIJING
Serikali
ya China imetangaza kuwa watu wawili wamepatikana na ugonjwa wa mafua ya ndege
katika mji wa kusini magharibi wa Guiyang.
Shirika
la habari la China, Xinhua limesema wagonjwa hao waliopata maambukizi ya mafua
ya ndege wana hali mbaya. Dalili za watu hao kuugua ugonjwa wa mafua ya ndege
aina ya H5N1 zilizanza kuonekana tarehe mbili na tatu mwezi huu.
Watu
waliokuwa karibu na wagonjwa hao, pia wamafanyiwa uchunguzi, ingawa
hajapatikana aliyepata maambukizi ya ugonjwa huo. Kwa mujibu wa Shirika la afya duniani WHO,
ugonjwa wa mafua ya ndege umeshaua watu mia tatu sitini na tano ulimwenguni,
tangu ulipogundulika mwaka 2003.
China
ni miongoni mwa nchi zilizo katika hatari zaidi ya maambukizi ya mafua ya ndege
kutokana na kuwa na miradi mingi ya ufugaji wa kuku katika maneneo ya vijijini
karibu na maeneo wanayoishi watu.
No comments:
Post a Comment