SINGIDA
Wito
umetolewa kwa wakazi wa Singida kushirikiana na serikali pamoja na asasi zisizo
za kiserikali katika kupambana na kupunguza ongezeko la watoto wa mitaani au
wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Wito
huo umetolewa leo na mwalimu mkuu msaidizi wa kituo cha asasi ya The Agape
Chriatian Orphans Children Care Support
ACOCAS, kilichopo katika kata ya Mandewa Manispaa ya Singida, Bw. Joel
Manase wakati akizungumza na Standard redio kituoni hapo.
Bw.
Manase amesema, ni jukumu la kila mtu katika jamii kuhakikisha anatumia kila
njia kwa hali na mali ili kupunguza ongezeko la watoto wa mitaani ama waishio
katika mazingira magumu.
Amesema
kuwa, kituo hicho chenye zaidi ya watoto mia moja kinachojishughulisha na kutoa
msaada wa elimu kuanzia ngazi ya chekechea na wengine shule za msingi pamoja na
wale hawakufanikiwa kujiunga na shule.
Amesema
kituo hicho kinakabiliwa na changamoto kama upungufu wa majengo, mahudhurio
mabaya kwa baadhi ya watoto kutokana na walezi au wazazi kuwatumia katika
shughuli za uzalishaji mali. Changamoto nyingine ni kukosa ufadhili kwani kwa
sasa kinaendeshwa na kanisa la TAG.
Source:SR
Ed:BM
Date:
9 February 2013.
BIHARAMULO
Jeshi la Polisi wilayani
Biharamulo Mkoani Kagera limefanikiwa kuzima tukio la uharifu kwa kuwapiga
risasi na kuwaua majambazi wawili wakati wakiwa katika harakati za kuvamia
wafanyabiashara na kuwapora
Tukio hilo limetokea
Februari 8 mwaka huu katika kijiji cha Nyabusozi, ambapo kundi la watu
wanaosadikiwa kuwa majambazi wakijiandaa kuvamia, wanachi walitoa taarifa kwa
jeshi la polisi ambao waliwazingira na kufanikisha kuua wawili huku wengine
wakikimbia
Kamanda wa Polisi mkoani
Kagera Phillip Kalangi ameiambia Standard Radio kuwa katika tukio hilo
majambazi hao wameacha Bunduki aina ya SMG na risasi 20, na kwamba jeshi la
polisi linaendelea kuwasaka wengine
Aidha, kamanda Kalangi amesema mafanikio hayo
yametokana na ziara ya mkuu wa wilaya hiyo Bw. Richard Mbeho na Kamati yake ya
ulinzi na usalama hivi karibuni katika kata ya Runazi, ambapo waliendesha zoezi
la kupiga kura kuwabaini wahalifu na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa
jeshi la polisi
Hata hivyo, kamanda huyo
amewataka wananchi kutoa taarifa kwa viongozi husika pale wanapoona raia
wanaowatilia mashaka ili kuepusha madhara ya uhalifu. EndS
Source:SR
Ed:BM
Date:
9 February 2013.
ZANZIBAR
Zanzibar, nchi yenye
wakazi zaidi ya milioni moja, na wenye kufuata utamaduni wa Kiislam ni miongoni
mwa nchi zilizokuwa na idadi kubwa ya wasichana wanaolazimishwa kuolewa wakiwa
na umri mdogo.
Utafiti uliyofanywa na
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) umeonesha kuwepo kwa
tatizo la kuwalazimisha wanafunzi kuolewa mapema visiwani Zanzibar, mjini na
vijijini.
Hata hivyo, ripoti ya
utafiti huo imebaini kuwa takwimu zilizopatikana ni chache kulinganisha na hali
halisi kutokana na kuwa ndoa nyingi za kulazimishwa hazifikishwi katika vyombo
vya sheria.
Kwa jumla takwimu za
Wizara ya Elimu, ni kesi 32 za kulazimishwa kuolewa zilirekodiwa mwaka 2011, na
kwamba kesi nyingi hazifikishwi polisi isipokuwa wanafamilia husuluhishana
wenyewe kwa wenyewe na kwa wale wanaokataa suluhu ndiyo wanaofikishana polisi
na mahakamani.
Aidha kwa mujibu wa
shirika la kimaitaifa la kuchangia maendeleo ya watoto (PLAN) wasichana zaidi
ya millioni 14 wanaolewa wakiwa na umri chini ya miaka 18 katika nchi za Kusini
mwa Jangwa la Sahara.
Inakisiwa kuwa katika
kila dakika moja, watoto wa kike 19 wenye umri chini ya miaka 18 wanaolewa kwa
nguvu duniani huku nchi za Chad, Niger, na Mali zikiongoza.
Source:SR
Ed:BM
Date:
9 February 2013.
DODOMA
Serikali
imewasilisha bungeni muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali na
kuomba kuzifanyia marekebisho sheria nane ikiwamo ya udhibiti wa fedha haramu.
Akiwasilisha muswada huo bungeni mjini Dodoma, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, amesema sheria hiyo sura ya 423 kwa kuongeza aya C kwenye tafsiri ya neno kufadhili ugaidi.
Amesema sehemu hiyo imefanyiwa marekebisho kwa kuzingatia ushauri wa Kamati ya Bunge na kwamba marekebisho yanayopendekezwa yanalenga kuongeza kwenye tafsiri ya kosa la kufadhili ugaidi.
Amesema tafsri ya neno hilo kama ilivyo sasa haijumuishi matendo hayo na kusababisha kuacha mwanya kwa wahalifu kutumia fursa hiyo kukamilisha malengo yao.
Jaji Werema amesema serikali inapenda kufanya marekebisho kwenye sheria ya kuzuia usafirishaji haramu wa binadamu, kwa lengo la kutoa ufafanuzi kwa mahakama ziwe na uwezo wa kusikiliza mashauri chini ya sheria hii kuwa ni mahakama ya hakimu mkazi au mahakama ya wilaya
No comments:
Post a Comment