Monday, February 25, 2013
HURUMA KWA WAGONJWA
STANDARD RADIO FM Inafurahi kukutangazia kuwa, kipindi kipya cha kuwafariji wagonjwa kimeanzishwa ili kuwawezesha wagonjwa na wanaowauguza kupata faraja na kutuma salaam na ujumbe kwa ndugu jamaa na marafiki
Kipindi hicho kimepewa jina la HURUMA KWA WAGONJWA na husikika kila siku ya Jumanne saa tatu kamili usiku katika masafa ya 90.1 MHz
kipindi hiki kimepangwa saa tatu usiku makusudi ili kiwe na manufaa zaidi, kwani majira hayo watu wengi wanakuwa na utulivu majumbani mwao, hivyo salaam au ujumbe kutoka kwa mgonjwa unaweza kumfikia ndugu, jamaa au rafiki, Tofauti na kutangaza kipindi hicho asubuhi au mchana ambapo kulingana na hali halisi ya maisha watu wengi wanakuwa katika pilika pilika za kusaka mkate wa siku
Tunakuarika kukisikiliza kipindi hicho ili upata taarifa na habari kutoka katika moja ya hospitali za mkoa wa Singida
STANDARD RADIO FM ni SAUTI YA WASIO SIKIKA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment