Source:SR/Beatrice
& Mary
Ed:
BM
Date:
18 February 2013.
SINGIDA
Mkazi
wa kijiji cha Munghamu kata ya Kinyeto tarafa ya Ilongero Mkoani Singida, Bw. Abbas
Mussa ameachiwa huru baada ya kesi ya ubakaji iliyokuwa inamkabili kukosa
ushahidi.
Akitoa
hukumu hiyo Hakimu wa Mahakama ya Hakimu mkazi Singida Bi. Flora Ndale amesema
amemuachia kutokana na ushahidi wa kesi hiyo kuwa hafifu
Imedaiwa
kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 30, mwaka 2011 majira ya saa tatu na nusu
usiku na kwamba alimbaka Bi. Zainabu Ramadhan wakati akitoka mnadani kwenye
shughuli zake za kujitafutia riziki
Amesema
kuwa alikutana na mshtakiwa Abbas na alipopishana naye kama hatua mbili nyuma
alimpiga ngwara na kuanguka chini, akakabwa kooni na kisha kuingiliwa kimwili
kwa nguvu na mshtakiwa.
Imeelezwa
mahakamani hapo kuwa, mlalamikaji baada ya kuachiwa aligundua kiasi cha
shilingi laki moja na nusu zimepotea na alipiga yowe kuomba msaada kwa majirani
wa eneo hilo la tukio, ambao walimkamata hadi alipofikishwa mahakamani
Source:SR/Pascal Buyaga
Ed:
BM
Date:
18 February 2013.
MUSOMA
Watu wawili wamekufa baada ya kuzamishwa
katika Ziwa Victoria wilayani Butiama mkoani Mara, na watu wanaosadikiwa kuwa wavuvi
haramu waliwagonga mtumbwi na hatimaye mtumbwi wao kuzama
Kamanda wa polisi, Kamishna Msaidizi
Absalom Mwakyoma amewataja watu waliozamishwa majini kuwa ni Mwenge Rwansa, mkazi
wa kijiji cha Kiemba na King Magessa mkazi wa kijiji cha Kabegi kata ya Nyakatende.
Taarifa za awali za jeshi la polisi zinaeleza kuwa watu hao walikuwa
katika msako wa kuwatafuta na kuwakamata wavuvi haramu wanaovua samaki katika
Ziwa Victoria kwa kutumia sumu.
Mwakyoma amesema watuhumiwa walifanikiwa
kutoroka kwa kutumia mtumbwi wao ambao haujajulikana na miili ya marehemu imepatikana
February 16 majira ya saa 5 asubuhi na taratibu za mazishi zinafanyika.
Aidha uchunguzi wa kina umeanza ili kubaini watuhumiwa waliotenda kosa
hilo ili wakamatwe na kufikishwa mahakamani
Source:SR/Matinde
Ed:
BM
Date:
18 February 2013.
MWANZA
Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka
jiji la Mwanza Bw. Robert Masunya amewataka wakazi wa jiji la mwanza kuhifadhi maji
kutokana na tatizo la umeme.
Wito huo umetolewa mapema leo wakati akizungumza na
Standard radio ofisini kwake. Bw. Masunya amesema kuwa tatizo la umeme limekuwa
likiathiri mitambo ya MWAUWASA katika kusukuma maji ambapo umeme umekuwa ukikatika
si chini ya saa 6 hali inayopelekea wakazi hao kukosa maji
Meneja Uhusiano huyo amesema kuwa oparesheni ya kusitisha
huduma ya maji kwa wateja ambao hawalipii bili zao inaendelea pamoja na kuwataka
wakazi kutoa taarifa pindi mwananchi atakapobainiwa kuwa ni mwizi wa maji.
Amewaomba wakazi wa jiji la Mwanza kuwa na utaratibu wa kuhifadhi maji ili yasaidie pindi umeme unakapokatika.
Source:SR/SAADA
Ed:
BM
Date:
18 February 2013.
SINGIDA
Mkurugenzi wa manispaa ya Singida Bw.
Mathias Mwangu amewataka watu wanaofunga vitambaa vya matangazo barabarani
kuviondoa pindi muda wake unapomalizika.
Bw.Mwangu amesema hayo leo wakati akizungumza na Standard Radio.
Ofisini kwake.
Amesema kuwa elimu inatakiwa kutolewa kwa wananchi au wadau
wanaohusika na matangazo ili kutoka vitambaa au mabango ambayo muda wake
umekwisha.
Aidha, Mkurugenzi huyo wa manispaa ya Singida Bw. Mwangu, amesema
elimu itolewe kuhusu athari za kuacha matangazo yaliyopitwa na wakati na
baadaye hatua za kisheria zitachukuliwa kwa atakayekiuka agizo hilo.
Source:SAPA
Ed:
BM
Date:
18 February 2013.
BAMAKO
Vikosi vya jeshi la Ufaransa kwa kushirikiana na vile vya Mali
jana vimeurejesha mji wa Bourem ambao umekuwa ukitumiwa na wapiganaji wa
Kiislam nchini Mali kupanga mashambulizi dhidi ya vikosi hivyo.
Mji wa Bourem upo umbali wa kilomita themanini kaskazini mwa mji
wa Gao katika njia panda ya barabara ziendazo katika miji ya Timbuktu na Kidal,
miji ambayo inadhibitiwa na majeshi ya Ufaransa na Mali.
Serikali ya Ufaransa imesema inatarajia kuondoa wanajeshi wake
wapatao elfu nne nchini Mali mwezi March, na kukabidhi jukumu la ulinzi kwa
jeshi la Mali na lile la Afrika AFISMA linaloungwa mkono na umoja wa mataifa.
Source:
AFP
Ed:
BM
Date:
18 February 2013.
TUNIS
Waziri mkuu wa Tunisia Bw. Hamadi Jebali leo ameanza mazungumzo na
viongozi wa vyama vya siasa ili kuunda serikali mpya, licha ya upinzani mkubwa
kutoka chama chake cha Kiislam cha Ennahda.
Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuanza mazungumzo
hayo, amevitaka vyama vya siasa nchini humo kufikia makubaliano ili kumaliza
ghasia zilizotokea nchini humo tangu February sita baada ya mauaji ya kiongozi
wa upinzani Chokri Belaid.
Hata hivyo mwenyekiti wa Chama cha Ennahda Rached Ghannnouchi
amepinga chama chake kuwa katika serikali ya Umoja wa kitaifa.
Waziri mkuu wa Tunisia Bw. Jebali ametishia kujiuzulu kama
atashindwa kuungwa mkono ili kuunda serikali mpya.
Source:
AFP
Ed:
BM
Date:
18 February 2013.
CAIRO
Maelfu ya raia wa Misri
wameandamana jana katika mji wa Port Said wakidai haki itendeke baada ya mauaji
ya raia wengi yaliyotekelezwa na polisi.
Habari zinasema
waandamanaji hao wamelazimisha shule na maduka kufungwa, na kuziba reli.
Waandamanaji wanataka
haki itendeke kufuatia mauaji ya raia arobaini baada ya kutokea mapigano na
polisi mwezi January baada ya mahakama moja kuwahukumu kifo mashabiki ishirini
na moja wa mpira wa miguu, kufuatia vurugu zilizotokea katika mpira wa miguu
mwaka jana.
Mwezi February mwaka
jana, watu sabini na nne mashabiki wa timu ya Al-Ahly walikufa katika vurugu
zilizotokea katika mji wa Port Said.
Source:AFP
Ed:
BM
Date:
18 February 2013.
CARACAS
Rais Hugo Chavez wa Venezuela ametangaza kupitia mtandao wa
Twitter mapema leo kuwa amerejea nchini mwake baada ya kuwa nchini Cuba
alikokuwa akipatiwa matibabu ya saratani.
Katika ujumbe kwa wananchi wa Venezuela, rais Chavez amesema
amerejea tena nchini mwake na kwamba anamshukuru Mungu na kuwashukuru raia wa
nchi hiyo.
Amesema ataendelea kupata matibabu ya ugonjwa wa saratani akiwa
nchini Venezuela.
Source :SR:BANDOLA
Ed.
Date 17February 2013
SINGIDA
Vijana wametakiwa kusoma kwa bidiii na kutambua kuwa
elimu ni hazina isiyofutika tofauti na vitu vingine katika jamii
Kauli hiyo imetolewa na mlezi wa ukwata mkoani
Singida Mwl Edward Samwel wakati wa hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka
wa kwanza katika chuo cha ufundi VETA ambao ni wanachama wa umoja wa kikristu
wa wanafunzi Tanzania (UKWATA)
Amesema vijana wanapaswa kutumia muda huu kwa
kufanya maandalizi mazuri ya maisha yao kwa kusoma kwa bidii, kwa kutambua kuwa
hivi sasa dunia iko katika utandawazi.
Amesema iwapo vijana hawatajituma kwa kipindi cha
ujana wao ni dhahiri hawataweza kuzalisha baada ya nguvu zao kupungua hali
ambayo inaweza kusababisha familia
kuwa katika mazingira magumu.
Aidha Bw. Samwel ametoa wito kwa vijana kuepuka
utumiaji wa madawa ya kulevya ambayo yanaweza kusababisha kutotimiza malengo
yao.
Source:SR/FS
Ed:
BM
Date:
18 February 2013.
IRAMBA
Mbuzi mmoja amezaa kiumbe
kinachofanana na binadamu katika kijiji cha Kinampanda wilaya ya Iramba mkoani
Singida.
Wamiliki wa mbuzi huyo Bw. Iddi Mssoliya na mkewe Bi. Rehema Danford
wamesema tukio hilo limetokea Februari 15 mwaka huu, na kwamba kiumbe hicho cha
ajabu kilikuwa na ngozi kama ya binadamu.
Akiongeana standard Radio nyumbani kwake jana, Bi. Rehema amesema
baada ya kubaini tukio hilo alienda kwa afisa ughani katika eneo hilo, ambaye
amesema kuwa hiyo ni hali ya kawaida katika suala la ukuaji wa viumbe katika
mfumo wa uzazi.
Aidha, Afisa kilimo na mifugo huyo Bw. Aron Kilazagaye ametoa wito
kwa wananchi kutokuwa na imani potofu kutokana na tukio hilo, bali watambue
hiyo ni hali ya kawaida inayoweza kutokea hata katika mfumo wa uzazi wa
binadamu.
Source: St Im(madeni)
Ed:
Date: February 18, 2013
SINGIDA
Idara za elimu nchini zimetakiwa kuwa na kitabu cha
madeni kama mkakati wa kupunguza tatizo la walimu kutumia muda mrefu kufuatilia
madeni katika halmashauri zao.
Akiongea na wakuu wa idara za elimu mkoani Singida,
Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa Bw
Kassim Majaliwa, amesema hatua hiyo itapunguza malalamiko ambayo yanajitokeza
mara kwa mara, kuhusu upotevu wa nyaraka za walimu wanaodai malipo mbalimbali.
Aidha amesema kuwa iwapo utaratibu huo utafutwa
itakuwa rahisi kwa idara hiyo kuwasilisha majina na kiasi wanachodai walimu ili
waweze kupata stahili zao
Kwa upande mwingine amewataka wakurugenzi na maofisa
wa idara ya elimu kutoa ufafanuzi wa stahili zao, ili kuepusha malalamiko
ambayo yamekuwa yakijitokeza wakati walimu wanapowasilisha madai yao.
Source: St Im(madeni)
Ed:
Date: February 18, 2013
DODOMA
Serikali imedhamiria kusambaza huduma bora za mfuko wa Afya ya Jamii CHF katika mikoa yote nchini, ili watanzania wote hasa wa kipato cha chini waweze kufaidika na huduma za afya
Serikali imedhamiria kusambaza huduma bora za mfuko wa Afya ya Jamii CHF katika mikoa yote nchini, ili watanzania wote hasa wa kipato cha chini waweze kufaidika na huduma za afya
Naibu Waziri, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa, Agrey Mwanri, ametoa kauli hiyo jana wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya
wa menejimenti ya taarifa za bima (IMIS) kwa ajili ya mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa
Amesema huduma bora za afya ni haki
ya kila Mtanzania, hivyo kuzinduliwa kwa CHF iliyoboreshwa, serikali
imedhamiria kusambaza huduma hizo nchi nzima kwa kushirikiana na wadau wengine,
ili Watanzania wengi zaidi waweze kufaidika
Meneja wa Mradi wa Health Promotion
and System Strengthening Project (HPSS), Manfred Stoermer, amesema CHF
iliyoboreshwa, inatumia mfumo mpya wa menejimenti ya taarifa za bima unaotumia
teknolojia ya kisasa zaidi.
Naye
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na mahusiano cha Vodacom, Joseline Kamuhanda,
amesema Vodacom Tanzania inasaidia mradi kama mdau muhimu, kwenye masuala ya
mawasiliano.
Source: St Im(madeni)
Ed:
Date: February 18, 2013
SINGIDA
Wakristo nchini wametakiwa kufuata mafundisho na
kutafuta uzima wa milele na sio pesa, maombezi na mafanikio tu.
Mchungaji Danieli Mwangungulu kutoka Dar es salam amesema
hayo wakati akihubiri jana katika kanisa la T.A.G lililopo eneo la Gineri mjini
Singida
Mchugaji Mwangungulu amesema waumini wamekuwa na
mazoea ya kutamani miujiza, uponyaji, na mafanikio, kuliko neno la mungu jambo
ambalo limezorotesha imani za waumini walio wengi.
Aidha mchungaji Daniel amesema hatua hiyo inaweza
kusababisha waumini kupokea imani potofu na kusahau njia ya uzima.
Kwa upande mwingine amewakumbusha kutafuta uzima wa
milele kuliko kuwapa ajira watumishi matapeli wanaojali maslahi yao jambo
ambalo linatishia imani ya kikristo kwa sasa.
Source: St Im(elimu)
Ed:
Date: February 18, 2013
SINGIDA
Kaimu mkuu wa mkoa wa Singida Bw Manju Msambya
amesema tatizo la lugha ya kufundishia hasa kwa shule za sekondari, ni moja ya
sababu zinazosababisha wanafunzi kufanya vibaya katika mitihani yao.
Akiongea katika
mkutano wa Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa Bw Kassim Majaliwa, ambao
umeshirikisha wakuu wa idara za elimu
mkoani Singida kwa lengo la kuweka mikakati ya kuboresha elimu, Bw Msambya
amesema wakati umefika wa kuangalia lugha ipi ya kufundishia
Insert Musambya
Cue in shule ya msingi
Cue out
kwa kutumia kishwahili
Aidha
amesema inasikitisha kuona viongozi wa kitaifa wakitoa hotuba kwa lugha ya
kiingereza wakati ziara za wageni mbalimbali wanapokuja hapa nchini, huku
wageni hao wakitumia lugha za mataifa yao kama sehemu ya kudumisha utamaduni
wao.
Source: 24
news (madeni)
Ed:
Date: February 18, 2013
MOGADISHU
Serikali ya somalia imetangaza donge la
dola elfu 50 za Kimarekani kwa raia atakayefanikisha kukamatwa kwa mtu anayehusika na mauaji ya
waandishi wa habari nchini humo
Hatua hiyo imetangazwa na waziri mkuu wa
nchi hiyo Bw Abdi Farah Shirdon ambaye amesema serikali yake inasikitishwa na mauji
hayo na kwamba ina nia ya dhati
kuhakikisha waandishi wa habari wanalindwa nchini humo.
Chama cha waandishi wa habari pia kimeunga mkono tangazo hilo la
serikali na kuongeza kuwa kitasaidia kuharakisha kukakamatwa kwa watu
wanaovamia waandishi wa habari.
Zaidi ya waandishi wa habari 18 wameuawa nchini Somalia kwa mwaka
uliopita pekee.
Source: 24 news (madeni)
Ed:
Date: February 18, 2013
KABUL
Waislamu
wa Kishia jana wameandamana katika miji mbalimbali ya Pakistan wakiishinikiza
serikali ya nchi hiyo kuwatia mbaroni waliosababisha milipuko huko Quetta na
kupelekea watu 81 kuuawa na zaidi ya 200 kujeruhiwa.
Shambulio
hilo la kigaidi linahesabiwa kuwa ni la pili kwa ukubwa dhidi ya Waislamu wa
Kishia katika historia ya nchi hiyo.
Familia
za watu waliouawa katika tukio hilo, wamegoma kuwazika watu wao ili kulalamikia
vitendo vya kigaidi wanavyofanyiwa huku serikali ikishindwa kudhibiti vitendo
hivyo.
Shirika
la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch nalo limelaani mauaji hayo ya
kigaidi na kumtaka waziri mkuu wa Pakistan kuwafuatilia waliofanya vitendo
hivyo vya kigaidi na kuwafungulia mashtaka.
Source:AFP
Ed:
BM
Date:
18 February 2013.
NEW YORK
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Ban
Ki-moon anatarajia kuhudhuria katika utiaji saini wa mkataba wa amani ya
mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo utakaofanyika wiki ijayo mjini
Addis Ababa nchini Ethiopia.
Msemaji wa Katibu mkuu wa umoja wa
mataifa, Martin Nersiki amesema Katibu mkuu wa umoja wa mataifa tayari
ameshapata mwaliko na anatarajia kuhudhuria tarehe 24 February mjini Addis
Ababa.
Amesema pia kuwa marais wote walioalikwa
kuhudhuria utiaji saini wa mkataba huo wameahidi kuhudhuria na wengine kuahidi
kutuma wawakilishi.
Nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,
Rwanda, Uganda, Uganda, Burundi, Angola, Congo, Afrika kusini na Tanzania
zinatarajia kusaini mkataba wa muundo, baada ya kukataa kusaini wakati wa
mkutano wa Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa mwezi uliopita.
Vikosi vya kulinda amani katika Jamhuri ya
kidemokrasi ya Kongo vitakuwa na jukumu la kupambana na makundi yenye silaha
ambayo yamekuwa yakifanya uhalifu katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo kwa
miaka kumi na tano iliyopita.
No comments:
Post a Comment