Pichani ni kitoto cha mbuzi chenye sura na maumbile ya binadamu
Mbuzi mmoja mali
ya bwana Iddi Mssoliya na mke
wake bi Rehema
Danford wakazi wa kinampanda wilayani
Iramba mkoani hapa februari 15
mwaka huu majira ya
saa moja Asubuhi alikutwa
Amezaa kiumbe ambacho
kilikuwa kinafanana na binadamu
huku kikiwa na ngozi
kama ya mtu.
Pichani ni Mbuzi aliyezaa maajabu hayo
Akiongea na
standard Radio nyumbani
kwake jana bi Rehema , Alieleza kuwa mbuzi
huyo ilikuwa ni
siku ya tatu akihangaika
kuzaa lakini siku
hiyo alipoamka limuona mbuzi
huyo amezaa na alipoangalia kilichozaliwa alishikwa
na butwaa na mshangao
mkubwa .
bi Rehema Danford akiwa nyumbani kwake alishuhudia mbuzi wake akizaa kiumbe cha ajabu
Hata hivyo amesema
kuwa , alimweleza mume wake
na wakaenda kwa afisa
ughani na kumweleza habari
hizo na kwenda kuangalia
kilichojiri , lakini afisa huyo aliwaeleza wananchi
kuwa hiyo ni
hali ya kawaida
tu katika suala
zima la ukuaji
wa kiumbe katika mfumo
wa uzazi,
Aidha Afisa kilimo
na mifugo huyo Bwn
Aron f. kilazagaye ametoa Wito
kwa Wananchi wote
kutokuwa na Imani potofu kutokana
na maajabu hayo ,
ispokuwa Watambue kuwa hicho ni
kitu cha kawaida kabisa;
ambacho kinaweza kutokea
kutokana na ukuaji wa kiumbe
kilichomo katika
mfumo wa Uzazi
iwe ni binadamu
au mnyama inaweza kutokea.
1 comment:
Hi! Do you use Twitter? I'd like to follow you if that would be okay. I'm definitely enjoying your blog and look forward to new posts.
Stop by my website :: comprar seguidores en Instagram barato
Post a Comment