Source:
SR/F. Sanga
Ed:
BM
Date:
22 February 2013.
SINGIDA
Mkuu
wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone, jana amemaliza ziara ya siku nne katika
wilaya za Iramba na Mkalama, kukagua
shughuli za maendeleo ikiwemo kilimo na elimu
Katika
ziara hiyo ambayo imeanza February 19 wilayani Mkalama, mkuu wa mkoa amekagua
ujenzi wa maabara zenye vyumba vitatu kwenye shule za sekondari za kata, kwa
ajili ya masomo ya sayansi ya Biolojia,
Kemia, na Fizikia ili ufaulu wa wanafunzi uongezeke kutokana na wanafunzi kufanya
mazoezi ya vitendo
Dk.
Kone amechangia baadhi ya shule ambazo zimefikia hatua nzuri ya ujenzi wa
maabara wilayani humo
Aidha,
Dk. Kone amewataka wakazi wa wilaya hizo kuacha uvivu katika shughuli za
kilimo, na kusisitiza walime mazao yanayostahimili ukame kama mtama, muhogo,
uwele, viazi vitamu, pamoja na zao la biashara la Alizeti.
Source:
SR/O. Samson
Ed:
BM
Date:
22 February 2013.
IGUNGA
Jeshi la polisi wilayani Igunga
mkoani Tabora linamshikilia Bi.Dorothea Zakaria, kwa tuhuma ya kuwaficha
wanafunzi 11 wanaosoma darasa la saba katika shule ya msingi Chipukizi iliyopo
wilayani humo.
Mmoja wa walezi wa wanafunzi hao Bw.
Daniel Winston amesema baada ya kumkosa mdogo wake kwa siku tatu, alifuatilia
shuleni na kubaini wanafunzi hao kuishi kwa mtuhumiwa pasipo walimu kujua
Mmoja wa wanafunzi waliofichwa, Masukuzi
Mohamed amekiri kuishi kwa mtuhumiwa huyo kwa siku tatu pasipo wazazi kujua na
kuongeza kuwa walikuwa wakitishiwa kuuawa endapo watasema wanaishi hapo
Amesema walikuwa wakikesha katika
maombezi ya kumwombea mwanafunzi mwenzao Safina Majaliwa, pamoja na wengine
waliokuwa wakisumbuliwa na mapepo yaliyokuwa yakiwaangusha mara kwa mara.
Mkuu wa polisi wilaya ya Igunga Bw
Abeid Maige, amethibitisha kutokea kwa tukio na kufafanua kuwa mtuhumiwa anatarajiwa
kufikishwa mahakamani Februari 25 mwaka huu
Source: SR/E. Chami
Ed: BM
Date: 22 February
2013.
SINGIDA
Serikali na taasisi mbalimbali mkoani Singida
zimeombwa kuangalia wajasiriamali walioko vijijini kwa kuwawekea miundombinu
ili kuinua uchumi wa nchi kwa ujumla
Mwezeshaji wa wajasiriamali wadogo wadogo
wa shirika la SEDA lilolopo mkoani Singida Bw. Gidion Timoth, amesema
wajasiriamali wengi hukimbia vijijini na kwenda mijini wakiamini ndiko penye
biashara jambo ambalo si sahihi kwani biashara ni popote.
Amesema hata makampuni mengi ya biashara,
benki taasisi zinazotoa mikopo na elimu ya ujasiriamali ziko mjini jambo
linalorudisha nyuma maendeleo ya wajasiriamali vijijini.
Amesema ni vyema elimu ikatolewa kwa
wajasiriamali walioko vijiini ili kuwajengea mazingira mazuri kwani wengi wao
wanapokimbilia mjini hawaendani na mazingira hivyo biashara zao kutoendelea.
Aidha, amesema kila mtu ana fursa ya kuwa
mjasiriamli na suala la ujasiriamali linamkubali kila mtu bila kujali kama
ameajiriwa au hajaajiriwa
Source:
SR/N. LIMU
Ed:
BM
Date:
22 February 2013.
MTWARA
Mkurugenzi mkuu wa
mfuko wa taifa wa bima ya afya NHIF, Bw. Emmanuel Humba, amesema mfuko umeanza mkakati wa kuboresha usajili wa
vitambulisho kwa mfuko wa taifa wa bima ya afya, ili viweze kukidhi mahitaji ya
sasa na ya wakati ujao.
Bw Humba
amesema hayo muda mfupi, kabla ya kumkaribisha Naibu waziri wa afya na ustawi
wa jamii, Dk. Rashidi Suleimani, kufungua kongamano la wahariri na waandishi wa
habari
Amesema tayari wamekubaliana na shirika la
NIDA katika kufanikisha utengenezaji wa vitambulisho hivyo vipya kwa wanachama
wa mfuko wa taifa wa bima ya afya.
Aidha, amesema kuwa lengo kuu la mfuko wa bima
kuanzia sasa, ni kuhakikisha watanzania wote wanajiunga na mfuko wa taifa wa
bima ya afya na ule mfuko wa afya ya jamii CHF.
Source: SR/Lyatuu
Ed: BM
Date: 22 February
2013.
SINGIDA
Wananchi mkoani singida wameitaka
serikali kuboresha taaluma kwa kuongeza vifaa vya kufundishia ili kuongeza
kiwango cha ufaulu wa wanafunzi wa shule za sekondari
Hayo yamesemwa na baadhi ya wananchi hao
Bw. Shira Saimon mkazi wa Singida wakati akizungumza na standard redio
kuhusiana na kutangazwa kwa matokeo mabaya ya kidato cha nne kwa wahitimu wa
mwaka jana.
Bw. Shira amesema kuwa kufeli kwa
wanafunzi wa kidato cha nne ni kutokana na kutokuwepo na vifaa vya kufundishia
ikiwemo uhaba wa vitabu, kukosa maabara pia wazazi kutofuatilia maendeleo ya
watoto wao kitaaluma
Vilevile
kwa upande mwingine amewataka wanafunzi kuwa makini kwa kutotegemea
vipindi vya darasani na badala yake
wajitume na kujishugulisha kusoma kwa bidii.
Sambamba na hayo naye Bw Tobias Mbaga ambaye
pia ni mkazi wa singida amemaliza kwa kusema serikali iandae tume kuu ya
usimamizi wa taaluma ili kuboresha elimu
1 comment:
Hello my family member! I want to say that this post is awesome, nice written and come with approximately all significant infos.
I'd like to look more posts like this .
Feel free to visit my web site :: marketbookmark.com
Post a Comment