Thursday, February 21, 2013

TAARIFA YA HABARI KUTOKA STANDARD RADIO


Source:sr Im(ziara)

Ed: BM

Date: 21 February 2013

SINGIDA

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida kamishna msaidizi wa Polisi Linus Sinzumwa amwataka wakuu wa polisi wa wilaya zote mkoani humo kutoa ushirikiano na kutitumia Standard Radio ili kupata na kutoa taarifa za uharifu



Kamanda Sinzumwa ametoa kauli hiyo baada kutembelea ofisi za standard radio Singida la kujifunza jinsi radio inavyofanya kazi pamoja na kuafahamiana na waandishi wa habari.

 

Kamanda Sinzumwa amesema standard radio imekuwa mstari wa mbele katika kuelimisha jamii kuhusu masuala ya usalama wa raia na mali zao kupitia habari na vipindi vyake

 

Wakuu wa polisi wilaya za Iramba, Mkarama, Ikungi, Singida na Manyoni pamoja na maafisa upelelezi wamemwahidi kamanda Sinzumwa kuwa watatoa ushirikiano huo kwa kuzingatia maadili ya jeshi la polisi na falsafa ya polisi jamii na ulinzi shirikishi

Naye meneja wa Standard Radio Bw Prosper Kwigize amemwahidi kamanda Sinzumwa kudumisha ushirikiano na jeshi la polisi hasa katika uandaaji wa vipindi vya usalama kwa lengo la kupunguza vitendo vya uharifu nchini
Source:sr NJ(uwekezaji)

Ed: BM

Date: 21 February 2013.

SINGIDA

Wakazi wawili wa manispaa ya Singida wamehukumiwa kifungo cha miaka miwili ama kulipa faini ya shilingi laki moja na elfu 50 baada ya kukutwa na hatia ya kumugonga na piki piki Bi Rehema Salumu

Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa R. B. Massam mwendesha mashtaka Maria Mdulugu amesema tukio hilo lilitokea feb. 18 mwaka huu

Amesema wakati tukio hilo linatokea Bi Rehema alikuwa anatembea kwa miguu na Salumu Kasanga alikuwa anaendesha pikipiki yenye namba za usajili T 565 CBX SUNLG

Aidha Massam amesema mshtakiwa namba moja Salumu Kasanga alikuwa anakabiliwa na makosa matatu ambayo ni kumgonga rehema, kutokuwa na leseni pamoja na bima

Mshtaliwa namba mbili ambaye ni mmiliki wa pikipiki hiyo alikuwa akikabiliwa na makosa ya kuruhusu pikipiki kuendeshwa bila bima na lessen.washitakiwa kwa pamoja wamelipa faini ya shilingi laki moja na elfu hamsini


Source: Daima

Ed: BM

Date: 21 February 2013.

SINGIDA

Waislamu mkoani singida wamelaani kitendo cha mauaji ya padri Evarest Mushi yaliyotokea visiwani zanzibar february 17 mwaka huu

 

Katibu wa bakwata wilaya ya singida mjini Bw Khamis Abrahaman amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari wa standadi redio ofisini kwake.

 

Amesema kitendo hicho cha mauaji kimewaumiza hivyo ameomba wananchi kudumisha upendo na amani ili kujenga taifa

 

Hata hivyo amewataka wananchi kuwa na ushirikiano na serikali ili kuweza kubaini wahusika waliofanya kitendo hicho cha mauaji

 

Aidha amewataka waumini kuwa na subira na kuepuka kujichukulia sheria mkononi na badala yake waiachie serikali kufanya uchunguzi wa mauaji hayo


Source:Tanzania Daima

Ed: BM

Date: 21 February 2013.

 

DAR ES SALAAM

Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kimesema serikali imepata hasara ya shilingi trilioni moja nukta tano, kutokana na wanafunzi walioshindwa kufanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa hivi karibuni.

Naibu Katibu Mkuu wa CWT, Bw. Ezekiah Oluoch, amewaambia waandishi wa habari kuwa, matokeo hayo mabaya ya kiwango cha ufaulu, hayajawahi kutokea tangu uhuru

Akifafanua zaidi, Bw. Oluoch amesema mwanafunzi mmoja hugharimu kiasi cha sh milioni moja nukta saba kwa mwaka katika elimu yake ya sekondari, hivyo ndani ya miaka minne anatumia sh milioni sita nukta nane.

Ametaja mambo makuu matatu ambayo yamesababisha matokeo hayo mabaya kuwa ni pamoja na serikali kuwekeza kiasi kidogo cha fedha katika sekta ya elimu, wanafunzi kufundishwa na walimu waliokata tamaa, na utoro.

Kwa mujibu wa Oluoch, hadi sasa katika bajeti ya serikali ni asilimia moja nukta nne tu katika pato la taifa inayowekezwa katika elimu, huku wanaopata fursa ya kusoma ni milioni kumi sawa na asilimia 25 tu ya Watanzania wote.

Source:Tanzania Daima

Ed: BM

Date: 21 February 2013.

 

DAR ES SALAAM

Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka amesema wananchi wanaotaka kununua nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), wasizinunue kwa mikopo ya benki kama hawana uhakika kulipa.

Ametoa tahadhari hiyo,wakati akizindua nyumba 98 zinazojengwa na shirika hilo eneo la Levolosi zenye vyumba viwili, sebule, jiko choo na bafu zitakazouzwa kwa sh milioni 82 bila kodi ya ongezeko la thamani (VAT)

Amesema kutokana na kiwango hicho cha fedha kuwa kikubwa kwa mwananchi wa kawaida, NHC imeweka mazingira ya kila anayetaka kununua nyumba hizo, kupata mkopo benki ambapo shirika linapewa fedha taslimu na benki halafu mnunuzi anaendelea kulipa deni hilo benki.

Amefafanua kuwa utaratibu huo licha ya kumsaidia mwananchi wa kawaida kumiliki nyumba, lakini una madhara yake endapo mnunuzi atashindwa kulipa deni kwa wakati, kwani benki itakuwa na mamlaka ya kuipiga mnada nyumba hiyo na hivyo kumuingiza katika matatizo makubwa.

Nyumba 98 zinazojengwa Levolosi zikiwa katika majengo matano ya ghorofa nne kila moja, zitagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni tano zitakapokamilika na kuuzwa kwa wananchi watakaokuwa wameomba kuzinunua.

 


Source:sr NJ(uwekezaji)

Ed: BM

Date: 21 February 2013.

 

SINGIDA

Wakamuaji wa mbegu za mafuta ya Alzeti mkoani Singida wametakiwa kuboresha kutumia vipimo sahihi ili kuepuka kuwa nyanyasa wakulima wa zao hilo

Akizindua leo katika kongano la ubunifu la wadau wa ukamuaji wa mbegu za alzeti mkuu wilaya ya Singida mjini Bi Qeeen Mlozi amesema alzeti ni zao muhimu katika mkoa wa Singida hivyo kuwataka wakulima kulipa zao hilo kipaumbele ili waweze kuinua kipato cha mkoa wa Singida

Naye afisa mtendaji wa (TCCIA) Bw Kalvert Nkurlu amesema lengo la taasisi hiyo ni kuongeza uzalishaji kwa nia ya kukuza uchumi wa wakulima wa zao hilo

 

Hata hivyo mwenyekiti wa usindikaji wa mafuta ya alzeti Bw Said Juma Hamod amesema changamoto zinazokwamisha taasisi hiyo ni pamoja na bei za nishati ya  umeme kuwa juu bei ya vipuri na kutokuwa na mahitaji muhimu pamoja na kukosa soko la uhakika jambo linalorudisha nyuma maendeleo ya taasisi hiyo

 

Aidha Bw Hamad ameiomba manispaa ya Singida kutoa eneo la kutosha kwa ajili ya shuguli zao na mitambo ya kusafilisha mafuta pamoja na kuonyesha ushirikiano kwa wadau wa mafuta kwa wadau wa waukamuaji wa mafuta ili waleta maendeleo kwa wakulima wa zao la alzeti

 

 

 

 

UNAENDELEA KUSOMATAARIFA YA HABARI KUTOKA STANDARD RADIO NA SASA NI HABARI ZA KIMATAIFA

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


Source:AFP

Ed: BM

Date: 21 February 2013.

HARARE

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amesema ameyakabidhi maisha yake kwa Mwenyezi Mungu na anajisikia mpweke kutokana na ndugu na marafiki wengi kufariki dunia.

Rais Mugabe amesema hayo Ikulu mjini Harare jana, katika hafla fupi kabla ya kuadhimisha miaka 89 tangu azaliwe, maadhimisho ambayo yatafanyika Machi 2 mwaka huu. 

Rais Mugabe amesema ni kwa kudra za Mungu ambaye ndiye muumba kumwezesha kufikia umri wa miaka themanini na tisa.

Hafla hiyo imehudhuriwa na mawaziri wa serikali, maafisa wa usalama na watumishi wa ofisi yake. Bw. Mugabe amekuwa madarakani tangu mwaka 1980, na ni miongoni mwa marais waliokaa madarakani kwa muda mrefu barani Afrika.

Maadhimisho ya miaka 89 tangu kuzaliwa kwa Mugabe yanatarajiwa kufanyika katika uwanja wa michezo katika mji wa Bindura.


Source:SAPA

Ed: BM

Date: 21 February 2013.

 

 

ABUJA

Polisi nchini Nigeria inamshikilia kiongozi wa Kiislam na wenzake wawili kwa tuhuma za kutumwa na Iran kupeleleza viongozi maarufu nchini humo.

Mtuhumiwa huyo Abdullahi Mustapha Berende, kiongozi wa Washia katika mji wa Ilorin, amekamatwa tangu mwezi Desemba kwa tuhuma za kuhusika na shughuli za kigaidi.

Msemaji wa ofisi ya usalama wa taifa Bi. Marilyn Ogar amesema uchunguzi uliofanya umebaini kuwa Bw. Berende anatuhumiwa kuanzisha mahabusu ya kigaidi kaskazini magharibi mwa Nigeria kwa kushirikiana na wenzake wawili

Amesema mtuhumiwa huyo amrfanya mafunzo nchini Iran na wafadhili wake kutoka Iran walimtaka kukusanya taarifa kuhusu maeneo yenye mkusanyiko na maeneo ya Hoteli zinazotembelewa na raia wa Marekani na Israeli ili kuandaa mashambulizi.

Mtuhumiwa huyo ambaye anatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni, amekanusha tuhuma za kuhusika na ugaidi lakini amekubali kutafuta taarifa muhimu kuhusu baadhi ya watu na taasisi.




 

 


Source:AFP

Ed: BM

Date: 21 February 2013.

 

MEXICO CITY

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, jana limevituhumu vikosi vya usalama vya Mexico kutochunguzwa vyema kutokana na zaidi ya watu mia mbili arobaini na tisa kupotea katika mazingira ya kutatanisha wakati wa utawala wa rais Filipe Calderon.

Shirika hilo limesema watu hao hawajulikani waliko tangu utawala wa Calderon uliomalizika mwaka 2006 na wanahofiwa kuwa wamekufa.

Taarifa ya shirika hilo la kutetea haki za binadamu yenye kurasa mia moja tisini na tatu imesema, vikosi vya uslama vimehusika na kupotea kwa watu hao tangu mwaka 2007, na kuiomba serikali kutaja maeneo walipo watu hao.

Taarifa hiyo imesema katika matukio zaidi ya mia moja na arobaini, ushahidi unaonesha uwepo wa mazingira ya kupotea kwa watu kutokana na shinikizo kutoka serikalini ambapo vikosi vya usalama vilishiriki moja kwa moja.

No comments: