*Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida Bw.
Yahya Nawanda amewataka wafanyakazi wilayani humo kuacha tabia ya kuwa na
vinyongo kazini, na badala yake washirikiane ili kuleta ufanisi katika
utekelezaji wa majukumu yao.
Amesema hayo wakati wa uchaguzi wa baraza
jipya la wafanyakazi wa halmashauri ya wilaya ya Iramba linaundwa, katika
ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
*Jeshi la Polisi mkoani Singida limekamata
bunduki pamoja na mamia ya risasi ambazo zinatajwa kuwa zilikuwa zikisafirishwa
kwenda kutekeleza uharifu.
Mkuu wa jeshi la polisi mkoani Singida
Kamishna msaidizi wa polisi Linus Sinzumwa mebainisha hayo leo wakati akiongea
na Standard Radio
Amesema msako mkali na doria za kina
zinafanyika ili kughakikisha waharifu wa aina zote wanatiwa mbaroni
*RAIS Paul Kagame wa Rwanda amemteua Mtanzania, Profesa
Silas Rwakabamba kuwa Waziri wa Miundombinu wa nchi hiyo katika mabadiliko ya
Baraza la Mawaziri yaliyofanyika Jumatatu iliyopita.
Kabla ya uteuzi huo, Profesa Rwakabamba alikuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda. Ni mmoja wa mawaziri wanaoingiza sura mpya katika Baraza la Rais Kagame ambalo amelifanyia mabadiliko kwa kuunda wizara nyingine mpya.
*Kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani
Papa Benedict wa 16 amejiuzulu rasimi leo kama alivyoahidi kufanya mapema mwezi
huu
Kabla ya kutekeleza azima hiyo, papa
Benedict amefanya misa kubwa katika kanisa kuu la mtakatifu Petro mjini Vatican
nchini Italia ambapo maelfu ya waumini walifurika kushuhudia tukio hilo
Papa benedict pamoja na mambo mengine
ametoa kauli kuwa anafahamu athari za uamzi wake wa kujiuzuru, lakini amebaki
kuwa na amani na imani thabiti kwa Mungu na kanisa lake
*Zaidi ya watu saba wamefariki dunia baada
ya gari moja lililokuwa na bomu kulipuka katika eneo la Kidal nchini mali
Tukio hilo limetokea wakati wanajeshi
kutoka nchini Ufaransa wakiwa katika mji wa Kidal nchini mali katika operesheni
ya kupambana na wapiganaji wa kiislam tangu mwezi January mwaka huu
No comments:
Post a Comment