Source:
SR/Bandola
Ed:
BM
Date:
14 February 2013.
Vijana
wametakiwa kutumia fursa zinazowazunguka kwa kujifunza ujasilimali ili
kujikomboa kiuchumi
Katibu
wa vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Bw. Ibrahim Mluwa amesema
hayo katika ofisi za Chama hicho manispaa ya Singida wakati akizungumza na
Standard Radio
Bw.Mluwa
ameeleza vijana wakiwa makini na waadilifu watakuwa na uwezo wa kubuni mambo ya
maendeleo kitendo ambacho kitainua uchumi wa taifa kuliko kuwa tegemezi kama
ilivyo sasa.
Aidha
Bw. Mluwa amesema CHADEMA imewezesha vikundi mbalimbali na kuvipa elimu ya
ujasilimali kitu na kusaidia baadhi ya vijana kujiajiri wenyewe
Source:
Tanzania Daima
Ed:
BM
Date:
14 February 2013.
MOSHI
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA
manispaa ya Moshi kikisema mpango wa mkuu wa mkoa huo wa kutaka kurudisha
majimbo yanayoongozwa na upinzani mikononi mwa CCM hauwezi kufanikiwa kwa njia
za visasi
CHADEMA kimemtaka Mkuu wa mkoa wa Kilimanajro
Bw. Leonidas Gama kuacha kuwagawa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro na badala
yake afanye shughuli za maendeleo zilizompeleka mkoani humo.
Meya wa Manispaa ya Moshi, Bw. Japhary Michael,
amesema Gama amekuwa akionyesha upendeleo kwa kuhudhuria mikutano ya CCM huku
akitumia mafuta ya serikali jambo ambalo ni kinyume na taratibu
Hata hivyo amesema uchumi wa mkoa huo kwa miaka
ya nyuma uliyumba, lakini kwa miaka ya hivi karibu umeanza kupanda kutokana na
wawekezaji wengi kuvutiwa na kukubali kuwekeza.
Source:
Tanzania Daima
Ed:
BM
Date: 14 February 2013
SINGIDA
Mwekiti
wa taasisi ya SINGIDA ANTS AIDS GROUP Bw Afred Ngoi awametaka wakazi wa mkoa wa
Singida kuzingatia mafunzo yanayotolewa juu ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa
Ukimwi
Bw
Ngoi amesema lengo la taasisi hiyo ni mafunzo kwa wananchi kuhusu magojwa yanaambukiza kama ukimwi na
kuwasaidia waathirika wa ukimwi mahitaji mbalimbali
Aidha
Bw Ngoi amesema changamoto zinazowakabili ni pamoja upungufu wa vitendea kazi, uhaba wa watoa
mafunzo na uelewa mdogo wa wananchi jambo linalorudisha nyuma maendeleleo ya
tasisi hiyo.
Naye
Bw Sombi Jakson Sombi mmoja wa wanachama wa taasisi hiyo amewataka wananchi
kutekeleza elumu wanayopewa na wahudumu wao na kuonyesha ushikiano ili kuepuka
majanga yanayoikabili jamii
Source:
Tanzania Daima
Ed:
BM
Date: 14 February 2013
SINGIDA
Mahakama kuu kanda ya kati imewaachia huru
washtakiwa Jamali Juma Kuwigwa, Hamza Maagila Simba na Jumaa Msile Zollo wakazi
wa Manyoni mjini waliokuwa wameshtakiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia
Akitoa hukumu ya kesi hiyo jaji wa mahakama kuu
kanda ya kati Laurent Kaduri baada ya washtakiwa kusomewa shtaka hilo na kukiri
kuwa kitendo hicho kilifanywa na wananchi wenye hasira kali.
Chanzo cha kifo hicho kimeelezwa kuwa marehemu
Boniphace Kahonga aliiba simu septemba 25-2011 na ndipo washtakiwa walikwenda
nyumbani kwa marehemu na kuweza kuondoka nae hadi maeneo ya J.Plazza manyoni
mjini.
Imeelezwa kuwa walipofika eneo hilo marehemu kahonga
alijaribu kuwakimbia na dipo walimita mwizi na wananchi walifika eneo hilo na kuanza
kumshmbulia na kumpiga hata kumsababishia majeraha yaliyotoa damu kwa wingi
hata kusababisha kifo chake
Source:
Tanzania Daima
Ed:
BM
Date:
14 February 2013.
SINGIDA
Jamii imeshauliwa
kutowatenga walemavu wa ngozi na badala yake
iwapende na kuwashirikisha kwenye
shuguli mbalimbali za maendeleo katika jamii
Katibu wa chama cha
walemavu Tanzania bi Ziada Ally kwenye ulingo wa ushirikishaji wa shuguli za maendeleo kwa walemavu
wa ngozi uliofanyika katika kata ya Unyambwa
manispaa ya Singida
Mdahalo huo
umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa chama hicho, viongozi wa
serikali pamoja na wananchi
Wakizungumza
katika mkutano huo baadhi ya wananchi wamesema kuwa walemavu wanapaswa
kuheshimiwa kuthaminiwa kupendwa pamoja
na kupatiwa mahitaji mbalimbali yakiwemo kofia za kujikinga na mionzi ya jua na
mafuta ya kulainisha ngozi
Hata
hivyo wananchi hao wameahidi kufikisha
ujumbe kwa jamii ili kuhusu yale yote waliyoyapata katika mkutano huo
No comments:
Post a Comment