Wednesday, February 13, 2013

HABARI FEB 13, SAA 11 JIONI


SINGIDA

 Upungufu  wa walimu,vyumba vya madarasa na  vifaa vya kufundishia, ni moja ya changamoto zinazoikabili shule ya msingi Nyerere, iliyopo manispaa ya singida mkoani humo.

 

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Bw,Yesaya Ramadhani, amesema shule hiyo ina upungufu  wa walimu  sita ,vyumba vya madarasa kumi  na nyumba za walimu.

 

Aidha amezitaja changamoto nyingine zinazoikabili shule hiyo, kuwa ni pamoja na msongamano wa wanafunzi darasani  na hiyo husababisha walimu kushindwa kufundisha  vizuri,

 

Ameitaja changamoto nyingine kuwa ukosefu wa vitabu, ambao unachangia kitabu kimoja kinatumiwa na wanafunzi sita, badala ya mmoja na dawati moja kutumiwa na wanafunzi wanne mpaka sita badala ya watatu.

 


Source:SR/

Ed: BM

Date: Feb 06/02/2013

SINGIDA

 

Wananchi wa kata ya mandewa katika manispaa ya Singida, wametakiwa kushirikiana na manispaa wakati wa shughuli za upanuzi wa mji, ili kuleta maendeleo katika kata na mkoa kwa ujumla.

 

Akizungumza na Standard radio afisa mtendaji wa kata ya mandewa Bw. Bakari Ntandu, amesema wananchi wa kata hiyo ni lazima watambue shughuli za mpango mji unaoendelea, kuwa zinalenga kubolesha maeneo yao

 

Kwa upande mwingine afisa huyo mtendaji amesema, wanaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa maabara kwa kila shule ya kata, ikiwa ni utekelezaji wa kauli ya rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

 

Aidha amewahimiza wananachi  kutoa ushirikiano ili kuhyakikisha miradi yote ya mwaka wa fedha 2012/13 inakamilika kwa wakati

 

Source:SR/

Ed: BM

Date: Feb 06/02/2013

DAR ES SALAAM.

Serikali ya Tanzania imekabidhiwa mashine mbili za mionzi, zinazotumika kutibu ugonjwa wa saratani, katika hospitali ya Ocean Road jiji Dar es salaam.

Mashine hizo zimekabidhiwa kwa waziri mkuu Mizengo Pinda, aliyekuwa amemwakilisha Rais wa jamuhuri ya tanzania Dk, Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa uzinduzi wa jengo jipya, litakalotumika kulaza wagonjwa wa saratani.

Mkurugenzi mkuu wa hospitali ya Ocean Road Prof Twalibu Mgoma, amekiri kuwepo kwa upungufu wa mashine kwa ajili ya ugonjwa huo.

Naye mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za Atomic IAEA, Yukia Amano, amesema shirika hilo litaisaidia Tanzania katika kukuza   teknolojia ya Atomic Afrika Mashariki.


 

Source:SR/

Ed: BM

Date: Feb 06/02/2013

ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar Dk, Ally Mohamed Shein ameishauri mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA, kuwa makini katika kutunza taarifa za wananchi wanaosajiliwa katika daftari la usajili wa vitambulisho vya taifa.

Akizungumza katika uzinduzi wa zoezi hilo la utoaji wa vitambulisho vya taifa,  kwa awamu ya kwanza Zanzibar, Dk Shein amesema utunzaji huo ndiyo njia ya msingi ya kulinda haki ya wananchi wanasajiliwa katika daftari hilo.

Aidha amesema uwepo wa vitambulisho hivyo pia utaweza kuisaidia serikali kuwafahamu wafanyakazi hewa, ambao wamekuwa tatizo kubwa kwa serikali ,jambo ambalo limepelekea kupoteza fedha nyingi kwa sasa.

Dk, Shein amesema, vitambulisho vya taifa vitawasaidia watanzania kutambulika na kumiliki kwa urahisi rasilimali zake, hasa kwa kipindi hiki cha shirikisho la jumuiya ya Africa mashariki.


 

Source:SR/

Ed: BM

Date: Feb 06/02/2013

SIMIYU.

Wakazi wa wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, wanakabiliwa na njaa kutokana na ukame uliyoikumba wilaya hiyo, katika msimu uliyopita.

Hayo yameeleza katika ziara ya mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilayani humo Bw, Mahamoud Mabula.

Wakazi hao wamesema kutokana na ukame huo upatikanaji wa chakula umekuwa mgumu, ambapo debe moja la mahindi linauzwa kati ya shilingi elfu kumi na nne na elfu kumi na tano.

Naye mkuu wa wilaya hiyo Bi, Gorgina Bundala, amesema serikali imetoa tani elfu moja mia saba sabini na moja, chakula ambacho kitauzwa kwa bei nafuu huku kingine kikigaiwa bure kwa watu wasiojiweza.

 


 

Source:SR/

Ed: BM

Date: Feb 06/02/2013

ABUJA

Waandishi wawili wa habari nchini , wamekamatwa kwa mauaji ya wahudumu tisa wa afya waliokuwa wanatoa chajo,  dhidi ya polio mjini Kano Kaskazini mwa nchi hiyo.

Habari zinasema kuwa waandishi hao inadaiwa waliwachochea wananchi kupitia njia ya redio, kupinga chanjo hiyo.

Baadhi ya viongozi wa kiislamu kaskazini mwa Nigeria, wanaamini kuwa chanjo dhidi ya polio huwazuia wanawake kuzaa, na hiyo ni njama ya nchi za magharibi kutaka kupunguza idadi ya waumini wa Kiislamu duniani.

Upinzani kama uwo nchini Nigeria ndiyo moja ya sababu iliyosababisha Nigeria kuwa miongoni mwa nchi tatu, ambazo polio bando ni janga kubwa.


 

Source:SR/

Ed: BM

Date: Feb 06/02/2013

PARIS.

Wafanyakazi wawili wa misaada nchini Ufaransa wamefungwa jela miaka miwili kila mmoja, kwa kosa la kujaribu kuhamisha watoto 103  nchini Ufaransa, kutoka Chadi mwaka 2007.

Erick Braton aliyeanzisha shirika la misaada la Zozek, pamoja na mshirika wake Emilie Leroch, walihukumiwa bila wao kufika mahakamani ingawa walifika mjini Paris kwa hukumu.

Wafanyakazi wengine wanne wa shirika hilo, walipokea vifungo vingine vya nje vya kati ya miezi sita na mwaka mmoja, ambapo shirika la Zozek limetozwa faini ya paundi themanini na sita.

Watoto waliokuwa wanahamishwa waliaminika kuwa ni yatima, kutoka nchi za Sudani, hususani jimbo la Dafuu ambalo linakumbwa na vita pamoja nchi ya Chadi

 


 

Source:SR/

Ed: BM

Date: Feb 06/02/2013

NEW YORK

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limelaani jaribio la tatu la nyuklia, lilofanywa na Korea kaskazini na kuahidi kuchukua hatua zaidi, dhidi ya taifa hilo kwa kitendo hicho.

Tamko hilo la wanachama kumi na tano wa baraza hilo, limepitishwa jana na wajumbe wa mataifa hayo

Wanadiplomasia wamesema kuwa majadiliano ya kuiwekea korea vikwazo vipya, yatachukua muda kwa kuwa, uwezekano wa china kupinga hatua hiyo ikihofia kuvuruga zaidi utawala wa korea ya kaskazini 

No comments: