Source:SR/Lyatuu
Ed:
BM
Date:
15 February 2013.
SINGIDA
Walimu
wa shule ya msingi Unyakumi manispaa ya Singida wameiomba serikali kutimiza
mahitaji yao ili kuboresha kiwango cha taaluma
Mwalimu
mkuu wa shule hiyo Bw. Joachim Msechu amesema hayo wakati akizungumza na
Standard radio shuleni hapo.
Amesema
kiwango cha elimu kinaendelea kushuka kutokana na walimu kukumbwa na changamoto
nyingi
Mwalimu
Msechu ametaja changamoto hizo kuwa ni ukosefu wa nyumba za walimu,
kucheleweshewa mishahara, na kulipwa mshahara mdogo
Aidha,
amesema utoro wa wanafunzi katika shule ya Unyakumi umekithiri, kutokana na
wazazi kukosa ushirikiano na walimu hali inayosababisha kudidimia kwa sekta ya
elimu.
Bw
Msechu ametoa wito kwa serikali kuhakikisha mahitaji ya walimu ikiwemo ujenzi
wa nyumba za walimu vinapatikana ili kuinua kiwango cha elimu
Ed:
BM
Date:
15 February 2013.
DAR
ES SALAAM
Menejimenti ya Benki ya NMB imesema imegundua kuwepo kwa taasisi inayojitambulisha kama Tanzania Loans Society ikidai kuwa mshirika wa benki hiyo katika kutoa huduma za kibenki.
Taasisi
hiyo imedaiwa kuwa, kwa kutumia mtandao wake wa intaneti imekuwa ikijinadi kutoa
mikopo ambayo fedha zake zimeidhinishwa na NMB kupitia kwa mameneja wa matawi.
Aidha,
Tanzania Loan Society pia inadaiwa kueleza kwamba fomu za maombi ya mkopo na
malipo ya usajili vinaweza kulipwa kwa kutumia namba ya simu ya mkononi
Menejimenti
ya NMB imezidi kuwatahadharisha wateja wake na umma kwa ujumla kwamba, haina
ushirika ama makubaliano yoyote na taasisi hiyo katika shughuli zake
NMB
imesema kuwa hutoa mikopo kupitia matawi yake tu, na kwamba hakuna namna yoyote
ambayo inaweza kusababisha gharama za maombi ya mikopo au mikopo kutolewa
kupitia simu za mkononi.
Source:Tanzania
daima
Ed:
BM
Date:
15 February 2013.
DAR
ES SALAAM
Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imetoa ajira mpya kwa walimu wa shule za msingi,
sekondari na vyuo vya ualimu nchini.
Waziri
wa wizara ya elimu Dk. Shukuru Kawambwa, amesema utoaji wa ajira hizo umefuata
tathmini zilizofanyika ili kubaini maeneo yenye upungufu wa walimu, ili kuweza
kupeleka walimu kwa wingi katika maeneo hayo
Waziri
Kawambwa amesema kwa sasa taifa lina upungufu wa walimu wa masomo ya Sayansi na
Hesabu, na mwaka huu wameajiri walimu elfu
mbili na thelathini na saba.
Kwa
mujibu wa Waziri Kawambwa, wameajiri walimu zaidi ya elfu kumi na tatu wa ngazi
ya cheti ambapo walimu hao wamepangwa katika shule za msingi zilizopo kwenye
halmashauri, na 41 wamepangwa katika shule za mazoezi zilizo chini yake.
Amesema
kwa upande wa wahitimu wa elimu ya shahada na stashahada, wameajiri walimu zaidi
ya elfu kumi na mbili kufundisha shule za sekondari zilizoko chini ya
halmashauri, 59 wamepangwa kuwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu, huku walimu 21
wamepangwa kufundisha shule za sekondari za mazoezi.
Ed:
BM
Date:
15 February 2013.
GEITA
Jeshi
la polisi mkoani Geita linamshikilia Mchungaji wa Kanisa la PAGT, Isaya Rutta ,
mkazi wa Kijiji cha Katoro, Wilaya ya Geita, kwa tuhuma za kuchinja ng’ombe
mmoja na mbuzi wawili na kusababisha vurugu kati ya waislamu na Wakristo.
Vurugu
hizo zimetokea juzi na kusababisha kifo cha mtu mmoja ambaye ni mchungaji
wa kanisa moja wilayani Geita na watu wengine 10 kujeruhiwa
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Paulo Kasabango, amesema mtuhumiwa amekamatwa juzi katika kijiji hicho ambapo inadaiwa kuchinja mifugo bila ya kuhusisha daktari wa mifugo kwa lengo la kuthibitishwa kama nyama hiyo ni salama kuliwa na binadamu
Kasabango
amesema kuwa mbali na kukamatwa kwa kosa hilo, pia anadaiwa kufanya makosa ya
kuchinja eneo ambalo si rasmi kwa mujibu wa sheria ya kifungu namba 17 ya
mwaka 2003.
Amesema
kuwa mtuhumiwa mwingine Ramadhani Pastory, ambaye kwa sasa amelazwa katika
Hospitali ya Rufaa ya Bugando akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi, anadaiwa
kumuua Mchungaji Mathayo Kachila wa Kanisa la PAGT Buseresere na kwamba
atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo wakati wowote akipata nafuu.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita, Magalula Saidi Magalula, amekemea kitendo walichofanya baadhi
ya wananchi, kujichukulia sheria mkononi na kuhatarisha amani.
Source:Tanzania
daima
Ed:
BM
Date:
15 February 2013.
DAR
ES SALAAM
Jeshi
la Polisi na askari wa ulinzi wa Mamlaka ya Bandari (TPA), wamefanikiwa
kuwakamata maafisa wa serikali na wamiliki wa bandari kavu kwa tuhuma za wizi
wa madini aina ya tantalite yaliyoonesha yametoka Tanzania.
Maafisa
hao saba na wengine watatu ambao hawajakamatwa, wamefunguliwa jalada la kesi ya
wizi wa mali isafirishwayo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Uchukuzi, Dk.
Harrison Mwakyembe, amewataja maafisa hao kuwa ni mfanyakazi wa wizara yake,
Godson Mnkeni, mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Mohamed Mbupu,
ambaye alitoa hati ya mzigo kusafirishwa, mmiliki wa kampuni na wakala wa
kusafirisha mizigo GFC, Francis Mutalemwa na msaidizi wake, Christopher Andrew.
Wengine
waliokamatwa ni mmiliki wa Kampuni ya bandari kavu ya Rudi Holding ambaye ni
raia wa Ufaransa, Gren Baniaux, mmiliki wa Kampuni ya PMM, Judith Mhina na
mtendaji wake, Edward Bachwa, ambao wanahojiwa ili kubaini nani anahusika.
Dk.
Mwakyembe amewataja watuhumiwa ambao hawajakamatwa kuwa ni Ofisa wa Usalama wa
Taifa ambaye alikuwepo wakati wa tukio la wizi huo, Hamisi Haji, Mmiliki wa
Kampuni ya Damco ambaye jina lake halijapatikana pamoja na raia wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC), aliyefahamika kwa jina moja la Christian.
Aidha,
Dk. Mwakyembe amesema kuwa atawataja maafisa wote wanaowakingia kifua watu
waliokamatwa kwa tuhuma mbalimbali bandarini.
No comments:
Post a Comment