Thursday, February 28, 2013

MAKTABA NCHINI ZAPEWA CHANGAOTO



Mkuu wa mkoa wa singida Dr Paseko Kone amezitaja maktaba nchini kuwa mstari wa mbele  katika harakati za kuleta maendeleo nchinikwa kupunguza watu wasiojua kusoma na kuandika

Akihutubia katika warsha ya  maendeleo ya sekta ya maktaba Tanzania iliyofanyika mkoani Singida leo, amesema warsha hiyo inasaidia kujadili mchango wa tasnia ya maktaba katika kuchangia juhudi za serikali za kuleta maendeleo na kuboresha sekta ya elimu na hali ya maisha ya Tanzania.

Dk. Parseko Kone amesema ni wajibu wa kila maktaba pamoja na wakutubi kuhakikisha wanatoa huduma sahihi zinazokidhi mahitaji ya watumiaji katika jamii.
 
Wakutubi kutoka mikoa yote nchini wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Singida, wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa wakutubi nchini ambao umefanyika wiki hii mkoani Singida sambamba na kuchagua viongozi wao wa kitaifa. Picha na Edilitruda Chami

Katika mkutano huo Dr. Kone amewataka wananchi hasa waishio vijijini,  kuondoa dhana potofu waliyojijengea kwamba maktaba ni kwa ajili ya wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani tu, kwani kutonakana na fikra hiyo hata idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika inaongezeka.

Amesema maktaba ni sehemu nzuri kwa watu kupumzika huku wakijisomea vitabu, magazeti na kusoma habari mbali mbali kupitia mitandao ya kompyuta hivyo ni vyema watu  kuwa na nguvu ya kuchemsha bongo kwani akili ikichemka mtu hupata furaha na kuongeza maarifa.

STANDARD RADIO YANG'ARA MTANDAONI

Jumla ya watu 17998 kutoka mataifa kumi na saba duniani wametembelea na kuusoma mtandao wa Standard Radio katika kipindi cha mwezi desemba mwaka 2012 hadi february mwaka huu

kwa Mujibu wa Afisa wetu wa Mawasiliano na chumba cha habari, nchi kinara kwa kusoma na kutembelea mtandao wa Standard Radio ni nchi ya Marekani ambapo watu wapatao 8550 walifungua blog ya www.standardradiofm.blogspot.com na kujisomea habari mbalimbali

Aidha Tanzania inashika nafasi ya pili kwa kuwa na wasomaji 7956 ikifuatiwa na nchi ya Uingereza ambao wasomaji wake wamefikia 527, na kufuatiwa na Urusi, Norway, Ujerumani, Ufaransa, Burundi na Uholanzi.


Picha inaonesha Ramani ya dunia na nchi ambazo zinaongoza kwa kutembelea na kusoma mtandao wa Standard radio iliyoko mkoani Singida nchini Tanzania

Aaidha nchi ambayo ilikuwa na wasomaji wachache ni Kenya, Australia na Bangladesh ambazi wasomaji wake walikuwa chini ya watano

Kwa mujibu wa Mratibu mradi na Meneja wa Radio Bw. Prosper Laurent Kwigize, Kampuni ya Standard Voice LTD inatarajia kuiwezesha radio hiyo kusikika katika mtandao pamoja na satelite hivi karibuni

kusikika kwa radio mtandaoni (internet) kutaongeza idadi zaidi ya wasomaji na wasikilizaji duniani kote.

Wednesday, February 27, 2013

HABARI KWA UFUPI KUTOKA STANDARD RADIO


*Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida Bw. Yahya Nawanda amewataka wafanyakazi wilayani humo kuacha tabia ya kuwa na vinyongo kazini, na badala yake washirikiane ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Amesema hayo wakati wa uchaguzi wa baraza jipya la wafanyakazi wa halmashauri ya wilaya ya Iramba linaundwa, katika ukumbi  wa mikutano wa halmashauri  hiyo.

 

*Jeshi la Polisi mkoani Singida limekamata bunduki pamoja na mamia ya risasi ambazo zinatajwa kuwa zilikuwa zikisafirishwa kwenda kutekeleza uharifu.

Mkuu wa jeshi la polisi mkoani Singida Kamishna msaidizi wa polisi Linus Sinzumwa mebainisha hayo leo wakati akiongea na Standard Radio

Amesema msako mkali na doria za kina zinafanyika ili kughakikisha waharifu wa aina zote wanatiwa mbaroni

 

*RAIS Paul Kagame wa Rwanda amemteua Mtanzania, Profesa Silas Rwakabamba kuwa Waziri wa Miundombinu wa nchi hiyo katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanyika Jumatatu iliyopita.


Kabla ya uteuzi huo, Profesa Rwakabamba alikuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda. Ni mmoja wa mawaziri wanaoingiza sura mpya katika Baraza la Rais Kagame ambalo amelifanyia mabadiliko kwa kuunda wizara nyingine mpya.

 

*Kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani Papa Benedict wa 16 amejiuzulu rasimi leo kama alivyoahidi kufanya mapema mwezi huu

Kabla ya kutekeleza azima hiyo, papa Benedict amefanya misa kubwa katika kanisa kuu la mtakatifu Petro mjini Vatican nchini Italia ambapo maelfu ya waumini walifurika kushuhudia tukio hilo

Papa benedict pamoja na mambo mengine ametoa kauli kuwa anafahamu athari za uamzi wake wa kujiuzuru, lakini amebaki kuwa na amani na imani thabiti kwa Mungu na kanisa lake
 
 

*Zaidi ya watu saba wamefariki dunia baada ya gari moja lililokuwa na bomu kulipuka katika eneo la Kidal nchini mali

Tukio hilo limetokea wakati wanajeshi kutoka nchini Ufaransa wakiwa katika mji wa Kidal nchini mali katika operesheni ya kupambana na wapiganaji wa kiislam tangu mwezi January mwaka huu

 

 

 

 

 

 

Monday, February 25, 2013

HURUMA KWA WAGONJWA


STANDARD RADIO FM Inafurahi kukutangazia kuwa, kipindi kipya cha kuwafariji wagonjwa kimeanzishwa ili kuwawezesha wagonjwa na wanaowauguza kupata faraja na kutuma salaam na ujumbe kwa ndugu jamaa na marafiki

Kipindi hicho kimepewa jina la HURUMA KWA WAGONJWA  na husikika kila siku ya Jumanne saa tatu kamili usiku katika masafa ya 90.1 MHz

kipindi hiki kimepangwa saa tatu usiku makusudi ili kiwe na manufaa zaidi, kwani majira hayo watu wengi wanakuwa na utulivu majumbani mwao, hivyo salaam au ujumbe kutoka kwa mgonjwa unaweza kumfikia ndugu, jamaa au rafiki, Tofauti na kutangaza kipindi hicho asubuhi au mchana ambapo kulingana na hali halisi ya maisha watu wengi wanakuwa katika pilika pilika za kusaka mkate wa siku

Tunakuarika kukisikiliza kipindi hicho ili upata taarifa na habari kutoka katika moja ya hospitali za mkoa wa Singida

STANDARD RADIO FM ni SAUTI YA WASIO SIKIKA

TAARIFA YA HABARI KUTOKA STANDARD RADIO


SINGIDA

Jamii imetakiwa kuweka wazi matukio yanayojitokeza kwa viongozi wao wa ulinzi na usalama, ili kufichua wahalifu katika kukabiliana na uhalifu nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo na Kiongozi wa Ulinzi Kata ya Mandewa Bw. Athuman Soteri wakati akizungumza na Standard Radio ofisini kwake.

Amesema ushirikiano miongoni mwa wananchi na viongozi ni jambo la muhimu katika harakati za kukabiliana na uhalifu na matukio mbalimbali nchini.

Amesema kamati ya ulinzi ya kata ya Mandewa imejipanga kufanya doria kila mara kwa kushirikiana na wananchi wa maeneo husika, na tayari wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa na kuwapeleka kwenye vyombo vya dola.

Amesema polisi kata hufika kila siku ya jumanne kutoa elimu kwa viongozi wa ulinzi na kutoa wito kwa viongozi wa vijiji kuandikisha vijana, ili wapewe mafunzo yatakayowawezesha kukabiliana na uhalifu.

Aidha amesema kamati hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile uchache wa askari, wananchi kutokuwa wazi kuelezea matukio yanapotokea, uhaba wa vitendea kazi kama, Virungu, Filimbi pamoja na Tochi ambavyo vinakwamisha utekelezaji wa zoezi hilo.

Ametoa wito kwa serikali kuwasikiliza na kuwa tayari kutoa misaada pale watakapohitaji ili kutekeleza jukumu lao katika jamii.

 


Source SR: Beatrice

Ed:BM

Date: February 25,2013

 

SINGIDA

Mahakama kuu kanda ya Kati mkoani Singida, leo imeahirisha kesi ya mauaji ya Kassim Juma anayekabiliwa na shtaka la kuua kwa kukusudia.

Kesi hiyo, imeahirishwa na Jaji wa mahakama kuu Kanda ya kati, Laurence Kaduri baada ya mshtakiwa kusomewa shtaka linalomkabili na kukana.

Imeelezwa mahakamani hapo kuwa mwezi Juni mwaka 2011, mshtakiwa Kassim Juma alimuua Martin Shilla maeneo ya Shelui wilaya ya Iramba mkoani Singida

Siku ya tukio mshtakiwa akiwa na nyundo mkononi, alimpiga marehemu Martin Shilla kwa nyundo kichwani hali iliyopelekea kuanguka pale pale.

Watu walioshuhudia tukio hilo walimchukua na kumpeleka hospitali ya wilaya ya Iramba mjini Kiomboi ambako alifariki wakati akipatiwa matibabu.

Mshtakiwa alikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi na katika kufanyiwa mahojiano na afisa wa polisi, alikana shtaka hilo na kesi hiyo imeahirishwa hadi kikao kijacho itakaposomwa tena.


 

Ed:BM

Date: February 25,2013

 

IRINGA

Mkuu wa mkoa wa Iringa Dk Christine Ishengoma jana amezindua jengo la upasuaji wa macho katika hospitali ya mkoa huo.

Jingo hilo lenye uwezo wa kuhudumia wagonjwa elfu moja na mia nne na arobaini limekarabatitiwa kwa zaidi ya million sabini zilizotolewa na shirika la kimataifa la kupambana na upovu duniani.

Katika hotuba ya mkuu wa mkoa huo, iliyosomwa kwa niaba yake na mkuu wa wilaya  ya Iringa Dk, Retisia Warioba amewataka watumishi wa hospitali hiyo kulitunza jingo hilo.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka wizara ya afya Dk Salaha Maongezi amesema Tanzania inakabiliwa na changamoto ya vifaa tiba vya macho uchache wa wataalamu wa macho na mwamko mdogo wa wananchi kuhusu ugonjwa wa macho.

Mbali na ukarabati huo, pia shirika hilo limenunua vifaa vya matibabu ikiwemo miwani yenye thamani ya shilingi milioni thelathini.


 

Source SR: Saada

Ed:BM

Date: February 25,2013

 

SINGIDA

Waumini wa dini ya Kiislam mkoani Singida, wametakiwa kushirikiana ili kudumisha amani na upendo nchini.

Sheikh Mkuu wa mkoa wa Singida, Al Haji Issa Simba wakati akizungumza na standard radio ofisini kwake. Amesema matukio yanayotokea yanatokana na kutokuwepo ushirikiano mzuri kutoka madhehebu ya Kikristo na Kiislam.

Amewaomba waumini wa dini ya Kiislam kufuata maadili mema ya dini hiyo na kuachana na mambo maovu na badala yake kufuata mambo mema yatakayowaletea thawabu maishani.

Aidha, Bw. Simba amewashukuru waumini wa dini ya Kiislam mkoani Singida kwa utulivu walionao kutokana na kuzingatia maadili ya dini yao.

 

 

 


 

Source SR:  (kilimo na ujenzi)

Ed

Date: February 25,2013

ZANZIBAR

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad ametahadharisha kuwa huenda kuna watu wenye nia mbaya, ambao wameamua kuyatumia matukio ya kuuawa na kujeruhiwa viongozi wa kidini, kujenga chuki baada ya kuona Wazanzibari hivi sasa ni wamoja.

Maalim Seif alisema hayo juzi usiku alipokuwa akihutubia katika hafla ya Maulid ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) mjini Kiuyu, Wilaya ya Wete Kaskazini Pemba.

Alisema inasikitisha kuona wapo viongozi wenye nia chafu dhidi ya Zanzibar, wenye tabia ya kutoa kauli za kujenga chuki na fitna miongoni mwa Wazanzibari chini ya kivuli cha matukio hayo.

Seif aliongeza kuwa, kinachoonekana kuna ajenda imetayarishwa ya kutaka kulazimisha chuki za kidini Zanzibar, licha ya kuwa kisiwa hicho kina historia ya dahari ya watu kuvumiliana na kuishi kwa pamoja.

Aliwataka wananchi wote wa Zanzibar hivi sasa wawe macho na ajenda zinazolengwa kuwavuruga, na waendelee kuishi kwa mshikamano na umoja kama ambavyo wamekuwa wakiishi.

Seif aliongeza kuwa, vitendo vya kuuawa na kujeruhiwa viongozi wa kidini Zanzibar ni mambo magen, na kwa miaka mingi nchi hiyo imekuwa ni mfano bora wa uvumilivu wa kiitikadi za kidini, licha ya kuwa asilimia 98 ya wananchi wake ni Waislamu.

Alieleza kwamba wingi wa Waislamu Zanzibar haukuifanya ifunge milango kwa watu wa imani nyingine, na kwa wakati wote wamekuwa wakiabudu kwa mujibu wa imani zao bila ya bugudha yoyote.

 

 

Source :

Ed: BM

Date: February 25,2013

 

MOROGORO

Shirika la kimataifa la Reading International la nchini Uingereza linatarajia kujenga maktaba arobaini katika shule za sekondari za kata nchini

Hilo limebainishwa na mwakilishi wa shirika hilo, Bw. George Muthabi wakati wa ufunguzi wa maktaba katika shule ya Nelson Mandela wilayani Morogoro.

Amesema mradi huo umeanza kuwanufaisha wanafunzi katika mikoa ya Morogoro, Lindi, Pwani, Dar es salaam na Mtwara

Kwa upande wake mkuu wa shule ya Nelson Mandela Gaudensi Muowa amesema kuwepo kwa maktaba hiyo kutasaidia wanafunzi kupenda kujisomea

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi waliozungumza na waandishi wa habari, wamesema kuwa maktaba hiyo itawasaidia kujisomea kwa umakini na kufanya vizuri katika masomo yao.

MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA STANDARD BLOGSPOT

Mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Parseko Kone (mwenye kofia) akiteta jambo na viongozi wa wilaya ya Mukalama wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa maabara, kilimo na uwajibikaji wa viongozi na wananchi wa wilaya hiyo hivi karibuni. wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Mukalama Bw. Edward Ole Lenga



























Padre Damas Missanga Mkurugenzi wa Radio Kwizera Ngara akiteta jambo na Bw. Moses Anthon fundi mkuu wa Mitambo wa Standard Radio fm, Missanga alitembelea chumba cha Mitambo ya Standard Radio FM jana. Aidha Moses amewahi kuwa fundi msaidizi wa Radio Kwizera kabla ya kujiunga na Standard Radio FM SIngida

Padre Damas Missanga, kutoka Radio Kwizera Ngara Kagera akisaini Kitabu cha wageni cha Standard Radi Fm Mkoani Singida, Missanga ni mwenyeji wa Mkoa wa Singida. Baadhi ya viongozi wa Standard Radio wamewahi kufanya kazi Radio Kwizera

FEEDBACK FROM THE US VISIT-MATATA PONYO DRC MINISTER

 
The Prime Minister of the Democratic Republic of Congo, Augustin Matata Ponyo Mapon, welcomes the outcome of his visit to New York and Washington from 3 to 9 February
KINSHASA, Dem. Rep. of Congo (DRC) February 15, 2013/ -- Augustin Matata Ponyo Mapon, Prime Minister of the Democratic Republic of Congo, states: “National economic performance, the orthodox management of public finances and the concerted efforts of the authorities in combating corruption were commended by all those I had the opportunity to meet”.
On return from his official visit to New York and Washington, from 3 to 9 February, the Prime Minister of the Democratic Republic of Congo, Augustin Matata Ponyo Mapon, held a press conference in Kinshasa, on 14 February.
He talked notably about his meeting with Ban Ki Moon, Secretary-General of the United Nations, on 4 February. Concerning the situation in the Nord-Kivu region, both leaders expressed their agreement on the signature, planned before the end of this month, of the regional framework agreement making provision for the deployment of an intervention force in this province. They additionally discussed a restructuring of the mandate of the United Nations Organisation Stabilisation Mission in the Democratic Republic of Congo (MONUSCO).
This framework agreement is due to be signed by the Democratic Republic of Congo, Rwanda, Uganda, Burundi, Angola, the Republic of Congo, South Africa, Tanzania, Zambia, Southern Sudan, the Central African Republic and the United Nations. “The intervention force will be deployed under the MONUSCO banner and several SADC countries are prepared to provide the necessary troops”, further indicated the Prime Minster.
Concerning the amendment of the MONUSCO mandate, the Prime Minister – who received guarantees regarding the arrival of drones in the region between June and July – expressed his hope that this would allow the UN troops “to intervene in order to ensure peace which is under threat by armed groups”.
Augustin Matata Ponyo Mapon also held meetings with several other US leaders: Chris Smith and Karen Bass (Chair and Vice-Chair of the Subcommittee on Africa in Congress), Wendy Sherman (Under Secretary of State for Political Affairs), Robert Hormats (Under Secretary of State for Economic Growth, Energy and the Environment), Johnnie Carson (Assistant Secretary of State for African Affairs), Neal Wolin (Acting Secretary of the Treasury), William Joseph Burns (Deputy Secretary of State) and Grant Harris (Special Assistant to the President, Barack Obama, and Senior Director for African Affairs). “The US authorities reiterated their call to those people who support the armed groups to stop”, stated the Prime Minister.
Concerning the economy, on 7 February, Augustin Matata Ponyo Mapon met with Christine Lagarde, Director General of the International Monetary Fund (IMF), and Jim Yong Kim, President of the World Bank. After outlining the economic performance of the Democratic Republic of Congo, the leaders of these two international organisations expressed their desire to continue to work alongside the Congolese government. “This is a definitive commitment”, indicated the Prime Minister.
On the issue of the suspension of the programme by the IMF, on 30 November 2012, due to a lack of transparency in the mining sector, Christine Lagarde and Augustin Matata Ponyo Mapon both called for “a fresh start”. The Prime Minister stated: “The issue of transparency in the mining sector will be dealt with within the framework of bilateral discussions”, having already signed two decrees in January outlining the terms and conditions for the transfer of mining assets.
The Prime Minister then concluded that “under the leadership of the Head of State, Joseph Kabila, we are determined to implement new governance”.
Reminder of the main economic figures for 2012.
Between 2009 and 2012, the annual growth rate in the Democratic Republic of Congo rose from 2.8% to 7.2%, with inflation falling from 46% to 2.7% (a performance not achieved by the country since 1976). The Congolese Franc remained stable, and both public and private investments significantly increased. Tax collections were optimised and public funds more than doubled, whilst national wealth also doubled. Growth forecasts for 2013 stand at 8.2%. It is the first time since 1973 that growth in the Democratic Republic of Congo will rise above 8%.
The government has also launched a series of self-funded programmes which amount to circa 200 million dollars (agriculture, transportation, energy, roads, education, etc.). Civil servant salaries have been “banked”. Mining production figures have exceeded the historic levels between 1970-1980, with over 600,000 tonnes of copper being produced in 2012.
Distributed by the African Press Organization on behalf of the Democratic Republic of the Congo.
Contacts:
Roger Ndaywel Fay, advisor responsible for communication and foreign relations for the Prime Minister.
Telephone: + 243 82 500 195; + 243 97 0000 111
Philippe Perdrix, 35°N agency.
Telephone: + 33 6 84 24 62 96
SOURCE
Democratic Republic of the Congo

RADIO KWIZERA NGARA YATEMBELEA STANDARD RADIO FM



Mkurugenzi wa Radio Kwizera Ngara Padre Damas Missanga SJ (mwenye kofia ya Pama maarufu kama Malboro) katikati, akiwa katika picha ya Pamoja na watangazaji wa STANDARD RADIO FM mkoanii SIngida, alipofanya ziara mapema leo akiwa njiani kwenda Dodoma na Dar es salaam kwa vikao.

 Waandishi wa Habari wa Standard Radio 90.1 MHz SINGIDA wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Radio Kwizera Ngara, Kutoka kushoto mstari wa mbele ni Prosper Kwigize (Project Coordinator wa Standard Radio) akifuatiwa na Padre Misanga wa RK Ngara, Boniface Mpagape Mhariri wa habari, Neema Julius mwakilishi wa Standard kutoka Manyoni, Zaitun Kimu Fundi Mitambo msaidizi, Saada Salum Mtayarishaji wa Kipindi cha naksh Nakshi za Asia, Beatrice Moses Mwanafunzi kutoka AJTC, Edilitruda Chami Mwandaaji wa kipindi cha Uchumi wetu, Michezo na kutoka Mitandaoni, Edna Lyatuu mwanafunzi kutoka AJTC Arusha na wa mwisho ni Bw. Missanga (mdogo wake Padre Misanga) ambaye amefuatana na kaka yake kuzuru ofisi na Studio za Standard Radio.



Ushirikiano huu ukiendelezwa hat

Saturday, February 23, 2013

HABARI FEBRUARY 23, 2013 SR FM


Source: SR/F. Sanga

Ed: BM

Date: 22 February 2013.

 

SINGIDA

 

Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone, jana amemaliza ziara ya siku nne katika wilaya za Iramba na Mkalama, kukagua shughuli za maendeleo ikiwemo kilimo na elimu

 

Katika ziara hiyo ambayo imeanza February 19 wilayani Mkalama, mkuu wa mkoa amekagua ujenzi wa maabara zenye vyumba vitatu kwenye shule za sekondari za kata, kwa ajili ya masomo ya sayansi  ya Biolojia, Kemia, na Fizikia ili ufaulu wa wanafunzi uongezeke kutokana na wanafunzi kufanya mazoezi ya vitendo

 

Dk. Kone amechangia baadhi ya shule ambazo zimefikia hatua nzuri ya ujenzi wa maabara wilayani humo

 

Aidha, Dk. Kone amewataka wakazi wa wilaya hizo kuacha uvivu katika shughuli za kilimo, na kusisitiza walime mazao yanayostahimili ukame kama mtama, muhogo, uwele, viazi vitamu, pamoja na zao la biashara la Alizeti.

 

 


 

Source: SR/O. Samson

Ed: BM

Date: 22 February 2013.

 

IGUNGA

Jeshi la polisi wilayani Igunga mkoani Tabora linamshikilia Bi.Dorothea Zakaria, kwa tuhuma ya kuwaficha wanafunzi 11 wanaosoma darasa la saba katika shule ya msingi Chipukizi iliyopo wilayani humo.

Mmoja wa walezi wa wanafunzi hao Bw. Daniel Winston amesema baada ya kumkosa mdogo wake kwa siku tatu, alifuatilia shuleni na kubaini wanafunzi hao kuishi kwa mtuhumiwa pasipo walimu kujua

Mmoja wa wanafunzi waliofichwa, Masukuzi Mohamed amekiri kuishi kwa mtuhumiwa huyo kwa siku tatu pasipo wazazi kujua na kuongeza kuwa walikuwa wakitishiwa kuuawa endapo watasema wanaishi hapo

Amesema walikuwa wakikesha katika maombezi ya kumwombea mwanafunzi mwenzao Safina Majaliwa, pamoja na wengine waliokuwa wakisumbuliwa na mapepo yaliyokuwa yakiwaangusha mara kwa mara.

 

Mkuu wa polisi wilaya ya Igunga Bw Abeid Maige, amethibitisha kutokea kwa tukio na kufafanua kuwa mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani Februari 25 mwaka huu

 

 

Source: SR/E. Chami

Ed: BM

Date: 22 February 2013.

 

SINGIDA

 

Serikali na taasisi mbalimbali mkoani Singida zimeombwa kuangalia wajasiriamali walioko vijijini kwa kuwawekea miundombinu ili kuinua uchumi wa nchi kwa ujumla

Mwezeshaji wa wajasiriamali wadogo wadogo wa shirika la SEDA lilolopo mkoani Singida Bw. Gidion Timoth, amesema wajasiriamali wengi hukimbia vijijini na kwenda mijini wakiamini ndiko penye biashara jambo ambalo si sahihi kwani biashara ni popote.

Amesema hata makampuni mengi ya biashara, benki taasisi zinazotoa mikopo na elimu ya ujasiriamali ziko mjini jambo linalorudisha nyuma maendeleo ya wajasiriamali vijijini.

Amesema ni vyema elimu ikatolewa kwa wajasiriamali walioko vijiini ili kuwajengea mazingira mazuri kwani wengi wao wanapokimbilia mjini hawaendani na mazingira hivyo biashara zao kutoendelea.  

Aidha, amesema kila mtu ana fursa ya kuwa mjasiriamli na suala la ujasiriamali linamkubali kila mtu bila kujali kama ameajiriwa au hajaajiriwa


 

Source: SR/N. LIMU

Ed: BM

Date: 22 February 2013.

 

MTWARA

Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa taifa wa bima ya afya NHIF, Bw. Emmanuel Humba, amesema mfuko  umeanza mkakati wa kuboresha usajili wa vitambulisho kwa mfuko wa taifa wa bima ya afya, ili viweze kukidhi mahitaji ya sasa na ya wakati ujao.

Bw  Humba amesema hayo muda mfupi, kabla ya kumkaribisha Naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii, Dk. Rashidi Suleimani, kufungua kongamano la wahariri na waandishi wa habari

 Amesema tayari wamekubaliana na shirika la NIDA katika kufanikisha utengenezaji wa vitambulisho hivyo vipya kwa wanachama wa mfuko wa taifa wa bima ya afya.

 Aidha, amesema kuwa lengo kuu la mfuko wa bima kuanzia sasa, ni kuhakikisha watanzania wote wanajiunga na mfuko wa taifa wa bima ya afya na ule mfuko wa afya ya jamii CHF.


 

Source: SR/Lyatuu

Ed: BM

Date: 22 February 2013.

 

SINGIDA

Wananchi mkoani singida wameitaka serikali kuboresha taaluma kwa kuongeza vifaa vya kufundishia ili kuongeza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi wa shule za sekondari

 

Hayo yamesemwa na baadhi ya wananchi hao Bw. Shira Saimon mkazi wa Singida wakati akizungumza na standard redio kuhusiana na kutangazwa kwa matokeo mabaya ya kidato cha nne kwa wahitimu wa mwaka jana.

 

Bw. Shira amesema kuwa kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne ni kutokana na kutokuwepo na vifaa vya kufundishia ikiwemo uhaba wa vitabu, kukosa maabara pia wazazi kutofuatilia maendeleo ya watoto wao kitaaluma

 

Vilevile  kwa upande mwingine amewataka wanafunzi kuwa makini kwa  kutotegemea  vipindi vya darasani na badala yake  wajitume na kujishugulisha kusoma kwa bidii.

 

 Sambamba na hayo naye Bw Tobias Mbaga ambaye pia ni mkazi wa singida amemaliza kwa kusema serikali iandae tume kuu ya usimamizi wa taaluma ili kuboresha elimu

Thursday, February 21, 2013

TAARIFA YA HABARI KUTOKA STANDARD RADIO


Source:sr Im(ziara)

Ed: BM

Date: 21 February 2013

SINGIDA

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida kamishna msaidizi wa Polisi Linus Sinzumwa amwataka wakuu wa polisi wa wilaya zote mkoani humo kutoa ushirikiano na kutitumia Standard Radio ili kupata na kutoa taarifa za uharifu



Kamanda Sinzumwa ametoa kauli hiyo baada kutembelea ofisi za standard radio Singida la kujifunza jinsi radio inavyofanya kazi pamoja na kuafahamiana na waandishi wa habari.

 

Kamanda Sinzumwa amesema standard radio imekuwa mstari wa mbele katika kuelimisha jamii kuhusu masuala ya usalama wa raia na mali zao kupitia habari na vipindi vyake

 

Wakuu wa polisi wilaya za Iramba, Mkarama, Ikungi, Singida na Manyoni pamoja na maafisa upelelezi wamemwahidi kamanda Sinzumwa kuwa watatoa ushirikiano huo kwa kuzingatia maadili ya jeshi la polisi na falsafa ya polisi jamii na ulinzi shirikishi

Naye meneja wa Standard Radio Bw Prosper Kwigize amemwahidi kamanda Sinzumwa kudumisha ushirikiano na jeshi la polisi hasa katika uandaaji wa vipindi vya usalama kwa lengo la kupunguza vitendo vya uharifu nchini
Source:sr NJ(uwekezaji)

Ed: BM

Date: 21 February 2013.

SINGIDA

Wakazi wawili wa manispaa ya Singida wamehukumiwa kifungo cha miaka miwili ama kulipa faini ya shilingi laki moja na elfu 50 baada ya kukutwa na hatia ya kumugonga na piki piki Bi Rehema Salumu

Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa R. B. Massam mwendesha mashtaka Maria Mdulugu amesema tukio hilo lilitokea feb. 18 mwaka huu

Amesema wakati tukio hilo linatokea Bi Rehema alikuwa anatembea kwa miguu na Salumu Kasanga alikuwa anaendesha pikipiki yenye namba za usajili T 565 CBX SUNLG

Aidha Massam amesema mshtakiwa namba moja Salumu Kasanga alikuwa anakabiliwa na makosa matatu ambayo ni kumgonga rehema, kutokuwa na leseni pamoja na bima

Mshtaliwa namba mbili ambaye ni mmiliki wa pikipiki hiyo alikuwa akikabiliwa na makosa ya kuruhusu pikipiki kuendeshwa bila bima na lessen.washitakiwa kwa pamoja wamelipa faini ya shilingi laki moja na elfu hamsini


Source: Daima

Ed: BM

Date: 21 February 2013.

SINGIDA

Waislamu mkoani singida wamelaani kitendo cha mauaji ya padri Evarest Mushi yaliyotokea visiwani zanzibar february 17 mwaka huu

 

Katibu wa bakwata wilaya ya singida mjini Bw Khamis Abrahaman amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari wa standadi redio ofisini kwake.

 

Amesema kitendo hicho cha mauaji kimewaumiza hivyo ameomba wananchi kudumisha upendo na amani ili kujenga taifa

 

Hata hivyo amewataka wananchi kuwa na ushirikiano na serikali ili kuweza kubaini wahusika waliofanya kitendo hicho cha mauaji

 

Aidha amewataka waumini kuwa na subira na kuepuka kujichukulia sheria mkononi na badala yake waiachie serikali kufanya uchunguzi wa mauaji hayo


Source:Tanzania Daima

Ed: BM

Date: 21 February 2013.

 

DAR ES SALAAM

Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kimesema serikali imepata hasara ya shilingi trilioni moja nukta tano, kutokana na wanafunzi walioshindwa kufanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa hivi karibuni.

Naibu Katibu Mkuu wa CWT, Bw. Ezekiah Oluoch, amewaambia waandishi wa habari kuwa, matokeo hayo mabaya ya kiwango cha ufaulu, hayajawahi kutokea tangu uhuru

Akifafanua zaidi, Bw. Oluoch amesema mwanafunzi mmoja hugharimu kiasi cha sh milioni moja nukta saba kwa mwaka katika elimu yake ya sekondari, hivyo ndani ya miaka minne anatumia sh milioni sita nukta nane.

Ametaja mambo makuu matatu ambayo yamesababisha matokeo hayo mabaya kuwa ni pamoja na serikali kuwekeza kiasi kidogo cha fedha katika sekta ya elimu, wanafunzi kufundishwa na walimu waliokata tamaa, na utoro.

Kwa mujibu wa Oluoch, hadi sasa katika bajeti ya serikali ni asilimia moja nukta nne tu katika pato la taifa inayowekezwa katika elimu, huku wanaopata fursa ya kusoma ni milioni kumi sawa na asilimia 25 tu ya Watanzania wote.

Source:Tanzania Daima

Ed: BM

Date: 21 February 2013.

 

DAR ES SALAAM

Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka amesema wananchi wanaotaka kununua nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), wasizinunue kwa mikopo ya benki kama hawana uhakika kulipa.

Ametoa tahadhari hiyo,wakati akizindua nyumba 98 zinazojengwa na shirika hilo eneo la Levolosi zenye vyumba viwili, sebule, jiko choo na bafu zitakazouzwa kwa sh milioni 82 bila kodi ya ongezeko la thamani (VAT)

Amesema kutokana na kiwango hicho cha fedha kuwa kikubwa kwa mwananchi wa kawaida, NHC imeweka mazingira ya kila anayetaka kununua nyumba hizo, kupata mkopo benki ambapo shirika linapewa fedha taslimu na benki halafu mnunuzi anaendelea kulipa deni hilo benki.

Amefafanua kuwa utaratibu huo licha ya kumsaidia mwananchi wa kawaida kumiliki nyumba, lakini una madhara yake endapo mnunuzi atashindwa kulipa deni kwa wakati, kwani benki itakuwa na mamlaka ya kuipiga mnada nyumba hiyo na hivyo kumuingiza katika matatizo makubwa.

Nyumba 98 zinazojengwa Levolosi zikiwa katika majengo matano ya ghorofa nne kila moja, zitagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni tano zitakapokamilika na kuuzwa kwa wananchi watakaokuwa wameomba kuzinunua.

 


Source:sr NJ(uwekezaji)

Ed: BM

Date: 21 February 2013.

 

SINGIDA

Wakamuaji wa mbegu za mafuta ya Alzeti mkoani Singida wametakiwa kuboresha kutumia vipimo sahihi ili kuepuka kuwa nyanyasa wakulima wa zao hilo

Akizindua leo katika kongano la ubunifu la wadau wa ukamuaji wa mbegu za alzeti mkuu wilaya ya Singida mjini Bi Qeeen Mlozi amesema alzeti ni zao muhimu katika mkoa wa Singida hivyo kuwataka wakulima kulipa zao hilo kipaumbele ili waweze kuinua kipato cha mkoa wa Singida

Naye afisa mtendaji wa (TCCIA) Bw Kalvert Nkurlu amesema lengo la taasisi hiyo ni kuongeza uzalishaji kwa nia ya kukuza uchumi wa wakulima wa zao hilo

 

Hata hivyo mwenyekiti wa usindikaji wa mafuta ya alzeti Bw Said Juma Hamod amesema changamoto zinazokwamisha taasisi hiyo ni pamoja na bei za nishati ya  umeme kuwa juu bei ya vipuri na kutokuwa na mahitaji muhimu pamoja na kukosa soko la uhakika jambo linalorudisha nyuma maendeleo ya taasisi hiyo

 

Aidha Bw Hamad ameiomba manispaa ya Singida kutoa eneo la kutosha kwa ajili ya shuguli zao na mitambo ya kusafilisha mafuta pamoja na kuonyesha ushirikiano kwa wadau wa mafuta kwa wadau wa waukamuaji wa mafuta ili waleta maendeleo kwa wakulima wa zao la alzeti

 

 

 

 

UNAENDELEA KUSOMATAARIFA YA HABARI KUTOKA STANDARD RADIO NA SASA NI HABARI ZA KIMATAIFA

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


Source:AFP

Ed: BM

Date: 21 February 2013.

HARARE

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amesema ameyakabidhi maisha yake kwa Mwenyezi Mungu na anajisikia mpweke kutokana na ndugu na marafiki wengi kufariki dunia.

Rais Mugabe amesema hayo Ikulu mjini Harare jana, katika hafla fupi kabla ya kuadhimisha miaka 89 tangu azaliwe, maadhimisho ambayo yatafanyika Machi 2 mwaka huu. 

Rais Mugabe amesema ni kwa kudra za Mungu ambaye ndiye muumba kumwezesha kufikia umri wa miaka themanini na tisa.

Hafla hiyo imehudhuriwa na mawaziri wa serikali, maafisa wa usalama na watumishi wa ofisi yake. Bw. Mugabe amekuwa madarakani tangu mwaka 1980, na ni miongoni mwa marais waliokaa madarakani kwa muda mrefu barani Afrika.

Maadhimisho ya miaka 89 tangu kuzaliwa kwa Mugabe yanatarajiwa kufanyika katika uwanja wa michezo katika mji wa Bindura.


Source:SAPA

Ed: BM

Date: 21 February 2013.

 

 

ABUJA

Polisi nchini Nigeria inamshikilia kiongozi wa Kiislam na wenzake wawili kwa tuhuma za kutumwa na Iran kupeleleza viongozi maarufu nchini humo.

Mtuhumiwa huyo Abdullahi Mustapha Berende, kiongozi wa Washia katika mji wa Ilorin, amekamatwa tangu mwezi Desemba kwa tuhuma za kuhusika na shughuli za kigaidi.

Msemaji wa ofisi ya usalama wa taifa Bi. Marilyn Ogar amesema uchunguzi uliofanya umebaini kuwa Bw. Berende anatuhumiwa kuanzisha mahabusu ya kigaidi kaskazini magharibi mwa Nigeria kwa kushirikiana na wenzake wawili

Amesema mtuhumiwa huyo amrfanya mafunzo nchini Iran na wafadhili wake kutoka Iran walimtaka kukusanya taarifa kuhusu maeneo yenye mkusanyiko na maeneo ya Hoteli zinazotembelewa na raia wa Marekani na Israeli ili kuandaa mashambulizi.

Mtuhumiwa huyo ambaye anatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni, amekanusha tuhuma za kuhusika na ugaidi lakini amekubali kutafuta taarifa muhimu kuhusu baadhi ya watu na taasisi.




 

 


Source:AFP

Ed: BM

Date: 21 February 2013.

 

MEXICO CITY

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, jana limevituhumu vikosi vya usalama vya Mexico kutochunguzwa vyema kutokana na zaidi ya watu mia mbili arobaini na tisa kupotea katika mazingira ya kutatanisha wakati wa utawala wa rais Filipe Calderon.

Shirika hilo limesema watu hao hawajulikani waliko tangu utawala wa Calderon uliomalizika mwaka 2006 na wanahofiwa kuwa wamekufa.

Taarifa ya shirika hilo la kutetea haki za binadamu yenye kurasa mia moja tisini na tatu imesema, vikosi vya uslama vimehusika na kupotea kwa watu hao tangu mwaka 2007, na kuiomba serikali kutaja maeneo walipo watu hao.

Taarifa hiyo imesema katika matukio zaidi ya mia moja na arobaini, ushahidi unaonesha uwepo wa mazingira ya kupotea kwa watu kutokana na shinikizo kutoka serikalini ambapo vikosi vya usalama vilishiriki moja kwa moja.