TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Original: English
RIPOTI YA NCHI MASIKINI SANA DUNIANI MWAKA 2012
UKWELI WA MAMBO NA TARAKIMU
Geneva, 26 Novemba 2012
Ripoti ya Nchi
Maskini Sana Duniani ya Mwaka 20121, yenye
kichwa kidogo cha habari
Kutumia Fedha Zinazotumwa na Raia Wanaoishi Nga’mbo na
Weledi Wao Kujenga Uwezo wa Uzalishaji,
Mwelekeo wa uhamiaji
Ø Idadi ya watu ambao
wamehamia Ulaya kutoka Nchi Maskini Sana (LDCs) iliongezeka kutoka milioni 19
mwaka 2000 kufikia milioni 27 mwaka 2010. Hii
ni sawa na 3.3% ya wakazi wote wa nchi hizo.
Ø Nchi Maskini Sana Duniani zinatoa 13% ya wahamiaji duniani kote---idadi
ambayo inalingana na mgawo wa LDCs katika idadi ya wakazi wote duniani (12.1%).
Ø Wahamiaji wanne kati ya watano kutoka
LDCs wanaishi kwenye nchi zinazoendelea (Kusini) na mmoja tu kati wa watano
ndiye anaishi kwenye nchi zilizoendelea (Kaskazini).
Utumaji fedha
Ø Kiwango cha fedha
zinazotumwa na raia waliohamia ng’ambo kwenda kwenye nchi zao kiliongezeka mara
nane kati ya mwaka 1990 na 2011: Kutoka dola bilioni 3.5 kufikia dola bilioni
27. Tangu mwaka 2008 kiasi cha fedha kimeendelea kuongezeka pamoja na kuwepo na
anguko la kiuchumi duniani.
Ø
Mwaka 2011 kiasi
cha fedha zilizotumwa kwenda nchini Tanzania kutoka Uingereza zilikuwa dola
milioni 4.5, kutoka Canada dola milioni 3.2 na kutoka Kenya dola milioni 2.5.
Ø Mwaka 2011, fedha
zilizotumwa kwenda LDCs zilikuwa kama mara mbili ya thamani ya uwekezaji wa
moja kwa moja (FDI) katika nchi hizi (dola milioni 15), na kiwango hiki
kilizidiwa tu na Misaada Rasmi Kutoka
Nje, yaani ODA (dola bilioni 42 mwaka 2010), kama chanzo cha fedha kutoka nje
ya nchi.
Ø Kiwango cha fedha
zinazotumwa kutoka nje kama kingegawanywa kwa mwananchi mmoja mmoja
kiliongezeka kutoka dola 10 kama kila mtu angepokea hadi dola 30 kati ya mwaka
2000 na 2010.
Ø Fedha zinazotumwa
na raia wanaoishi nje zina umuhimu wa pekee kwa LDCs ikilinganishwa na nchi
zilizo katika makundi mengine. Katika LDCs, fedha zinazotumwa na raia kutoka
nje zinachangia 4.4% kwenye pato la nchi na 15% ya thamani ya bidhaa zinazouzwa
nje. Kiwango hiki ni kikubwa kwa mara tatu ikilinganishwa na nchi nyingine
zinazoendelea (ambazo siyo LDCs).
Ø Kuanzia mwaka 2008
hadi 2010, kiasi cha fedha kilichotumwa kutoka nga’mbo kinalingana na zaidi ya
moja ya tano ya pato la taifa la nchi za Lesotho, Samoa, Haiti na Nepal.
Ø Tangu mwaka 2009
hadi 2011, nchi za Nepal na Haiti zilipata fedha nyingi za nje kutoka kwa raia
wao walio ng’ambo kuliko zile ambazo nchi hizi zilipata kutokana na mauzo ya
bidhaa nje.
Ø Kwa LDCs tisa,
kiwango cha fedha zinazotumwa na raia wanaoishi nje kilizidi kile cha uwekezaji
wa moja kwa moja kutoka nje (FDI) na misaada rasmi kutoka nje (ODA) kati ya mwaka 2008 na 2010. Hizi
ni nchi za Bangladesh, Haiti, Lesotho, Nepal, Samoa, Senegal, Sudan, Togo na
Yemen. Kwenye nchi nyingine nane za kundi la LDCs, katika kipindi hicho hicho,
fedha zinazotumwa na raia kutoka ng’ambo zilizidi FDI: Benin, Burundi, Comoros,
Ethiopia, Gambia, Guinea-Bissau, Kiribati na Uganda.
Ø Theluthi mbili ya fedha zinazotumwa na
raia kutoka ng’ambo kwenda kwenye LDCs zinatoka kwenye nchi zinazoendelea.
Ø Duniani kote, gharama ya kutuma fedha
zinafikia 9% ya kiwango cha fedha kilichotumwa; kwa LDCs gharama ni kubwa zaidi
kwa theluthi moja (12%).
Ø Kama nchi zilizo kusini kwa Jangwa la
Sahara zingelipia gharama za uhamishaji fedha kwa wastani wa gharama inayolipwa
duniani kote, mapato yao yangekuwa yaliongezeka kwa dola bilioni 6 mwaka 2010.
Ø Asilimia 66 ya fedha zilizohamishwa
kwenda kwenye LDCs kati ya mwaka 2009 na 2011 ni za nchi tatu tu: Bangladesh,
Nepal na Sudan.
Ø Matumizi ya simu za mkono kwenye LDCs ni
makubwa zaidi (368 kwa kila wakazi 1,000)
kuliko idadi ya akaunti za benki (171 kwa wakazi 1,000). Simu za mkono
zinaweza vile vile kutumika katika kuhamisha na kupokea fedha kutoka ng’ambo.
Kuhama kwa utaalam
Ø Mtu mmoja kati ya
kila watu watatu wenye ujuzi mkubwa (mwenye elimu ya chuo kikuu) kutoka LDCs
anaishi ng’ambo. Kwenye nchi zilizoendelea kiwango
ni mtu mmoja katika kila watu 25.
Ø LDCs sita zina raia wao wataalaum wengi
zaidi wanaoishi nje ya nchi kuliko wale waliobakia nchini mwao: Haiti, Samoa,
Gambia, Tuvalu na Sierra Leone.
Ø Theluthi mbili ya wahamiaji wenye ujuzi
mkubwa kutoka LDCs wanaishi kwenye nchi zilizoendelea; theluthi moja wanaishi
katika nchi zinazoendelea.
Ø Kiwango cha kuhama kwa watu wenye ujuzi
kwenda ng’ambo ni kikubwa (20% ) kwa LDCs nyingi (30 kati ya 48).
Ø Wahamiaji kutoka LDCs wenye elimu ya
chuo kikuu ambao wanaishi na kufanya kazi ng’ambo inafikia milioni 2.
Ø Idadi
ya Watanzania waliohamia Uingereza kwa kumbukumbu za mwaka 2000 ni 10,535.
Ø Aina ya wahamiaji inafuata ukubwa wa
kipato wa nchi mwenyeji. Katika nchi zilizoendelea, 35% ya wahamiaji ni wale
wenye elimu ya chuo kikuu; kwenye LDCs 4% tu ya wahamiaji wana kiwango hicho
cha elimu. Viwango hivi ni kwa wahamiaji kutoka nchi zote, japo viwango ni hivi
hivi kwa wahamiaji kutoka nchi za kundi la LDCs.
Ø Theluthi moja ya wahamiaji kutoka LDCs
ambao wana elimu ya chuo kikuu wanaishi Marekani.
Uwezo wa kiuchumi (Uchumi mpana)
Ø Kiwango cha ukuaji
wa uchumi kwa mwaka kwa LDCs tangu kipindi cha msukosuko wa kiuchumi duniani
(2009-2011) ni 4.7%, ambacho ni chini ya kiwango cha kipindi cha miaka ya
ukuaji mkubwa wa kiuchumi (2003-2008), yaani 7.9%. Hii ina maana kwamba kiwango
cha ukuaji wa kipato kwa mwaka kwa kila mkazi kilishuka kutoka 5.4% miaka ya
ukuaji mzuri wa uchumi hadi kufikia 2.4%.
Ø Wastani wa ukuaji
halisi wa pato la nchi katika LDCs mwaka 2011, yaani 4.2%, ulikuwa chini ya
4.9% ya mwaka 2009 wakati wa anguko la uchumi duniani.
Ø Kile kinachojulikana kama Gross fixed capital formation kwenye
LDCs kilipanda kidogo kutoka 20.7% ya pato la jumla la taifa mwaka katika miaka
ya 2005-2007 kufikia 21.6% miaka ya 2008-2010. Hata hivyo, bado kilibaki chini
ya viwango vya nchi nyingine zinazoendelea, ambazo zilifikia kiwango cha 30.1%.
Ø LDCs zinaendelea kutegemea sana
raslimali kutoka nje. Pengo la pato linalotokana na uagizaji bidhaa na uuzaji
bidhaa nje lilikuwa kubwa kwa 20% ya pato la jumla la taifa katika nchi tano za
kundi la LDCs mwaka 2011, wakati LDCs nyingine 13 pengo lilikuwa asilimia 10 ya
pato la jumla la taifa.
Ø Kiwango cha utegemezi wa rasilimali
kutoka nje katika kulipia uwekezaji wa ndani ya nchi kati ya mwaka 2008 na 2010
kilikuwa 15% ya pato la jumla la taifa kwa LDCs ambazo hazisafirishi mafuta
nje.
Ø Asilimia 62 ya mauzo ya bidhaa nje
kutoka LDCs 48 yalikuwa ni kutoka nchi tano tu: Angola, Bangladesh, Equatorial
Guinea, Yemen na Sudan. Ukiacha Bangladesh, nchi zote hizi zinauza mafuta nje.
Ø Mapato ya LDC kwa mauzo ya bidhaa nje
yanategemea zaidi mauzo ya bidhaa moja (mafuta), ambayo yanaingiza 46% ya jumla
ya mapato yote yanayotokana na mauzo ya bidhaa nje.
Ø Zaidi ya nusu ya mauzo ya nje kutoka
LDCs (54%) yalikuwa yanakwenda kwenye nchi zinazoendelea mwaka 2011, mwelekeo
unaothibitisha umuhimu wa biashara ya kusini-kusini. China ndiyo iliyonunua
bidhaa nyingi zaidi kutoka LDCs (26.4%) ikiwazidi Jumuia ya Ulaya (20.4%) na
Marekani (19%).
ZIKO WAPI NCHI MASKINI
SANA DUNIANI?
Umoja wa Mataifa
unaziweka nchi 48 kwenye kundi la Nchi Maskini Sana Duniani (LDCs). Mgawanyo
wao ni kama ifuatavyo.
Africa (33): Angola, Benin, Burkina Faso, Burundi,
Central African Republic, Chad, Comoros, Jamhuri ya KIdemnokrasia ya Kongo(DRC),
Djibouti, Equatorial Guinea, Eritrea, Ethiopia, Gambia, Guinea, Guinea-Bissau,
Lesotho, Liberia, Madagascar, Malawi, Mali, Mauritania, Msumbiji, Niger,
Rwanda, Sao Tome na Principe, Senegal, Sierra Leone, Somalia, Sudan, Togo,
Uganda, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zambia;
Asia (9): Afghanistan, Bangladesh, Bhutan,
Cambodia, Lao, Myanmar, Nepal, Timor-Leste na Yemen;
Caribbean (1): Haiti;
Pacific (5): Kiribati, Samoa, Solomon Islands,
Tuvalu na Vanuatu.
Mchoro 1 – Nchi 48 za kundi la LDCs
Imetolewa na UNCTAD
Kutengeneza list ya LDCs
List ya LDCs
inapitiwa upya kila baada ya miaka mitatu na Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC)
la Umoja wa Mataifa, kufuatana na mapendekezo ya kamati ya Sera ya Maendeleo
(CDP).
Katika mapitio ya
hivi karibuni, Machi 2012, CDP ilitumia vigezo vifuatavyo:
1. Kigezo cha pato la kila mtu, kwa kufuata
Pato la Jumla la Nchi (GNI) kwa kila kichwa (wastani wa miaka mitatu)
2. Kigezo cha raslimali watu ambacho
kinatumia viashiria kama lishe, afya, kuandikishwa shuleni na kujua kusoma na
kuandika
3. Kigezo cha mazingira hatarishi ya
kiuchumi. Ambacho kinatumia viashiria kama mishtuko ya kiasili, mishtuko ya
kibiashara, udogo na umbali.
Nchi tatu tu
zimefanikiwa kupanda daraja kutoka list ya nchi za kundi la LDCs: Botswana
Desemba 1994, Cape Verde Desemba 2007
na Maldivs Januari 2011. Samoa inategemewa kupanda daraja tarehe 1 Januari
2014.
ECOSOC ilipitisha
pendekezo la CDP kuipandisha daraja Equatiorial Guiones mwezi Julai mwaka 2009
na mwezi Julai 2012 ikakubali pendekezo la CDP kuipandisha Vanuatu. Hata hivyo
ruhusa ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa bado itahitajika ili kuzipandisha
daraja nchi hizi mbili.