Na. PHESTHOW
SANGA;
IRAMBA
Uchaguzi wa
Viongozi wa ngazi mbalimbali
katika chama cha mapinduzi {
CCM}Wilayani Iramba Mkoani Singida umemalizika juzi sept 8Mwaka huu ,Huku wanawake
wakiwabwaga chini vibaya Wanaume
waliogombea katika nafasi za Mwenyekiti .
Chaguzi hizozilizoanza mapema
Septemba 0 4 Mwaka huu, kwa Jumuiya
ya Umoja wa Wanawake Tanzania {
UWT}kwa Jenephar J. Miano , kufanikiwa
kutetea kiti chake tena,
baada ya kutangazwa mshindi na msimamizi
mkuu wa uchaguzi huo { mb} wa singida magharibi mhe
misanga. kwa kupata jumla ya kura
334 dhidi ya 48 za Neema Imaryna 31 za
Hawa Rajabu.
Aidha
kindumbwe-ndumbwe kilikuwepo kwenye Jumuiya mbili
za Umoja wa vijana CCM pamoja na
ya Wazazi, katika Jumuiya yaVijana Ambapo
wagombea walikuwa watatukatika nafasi yamwenyekiti , wakiongozwa na
Ahamed Makame ,Athumani Rajabu, pamoja
na Mwanamke pekee Ziyana J.Mtali.
Katika
Uchaguzi huoUliofanyika Spt.08 Mwaka
huu ambapokulikuwa na Upinzani
kubwa kutokana na wagombea wote kuwa na Elimu nzuri Ingawa Athumani Rajabu ,ni mhitimu
wa chuo kikuu Tumaini Iringa, lakini hawakuweza kufua dafu baada
ya kusaliti Amri kwa Mwana Dada,
Ziyana Mtali aliyetangazwa Mshindi na
Msimamizi mkuu Salumu Mkuya
,kwakupata kura 187kati ya 275zilizo
pigwa.
Hata hivyo
Mapinduzi ya kuwabwaga Wanaume
yaliendeleakwenye Jumuiya ya Wazazi,
ambapo huko nako wagombea walikuwa
watatu kati ya hao Mwanamke alikuwa mmoja pekee Alisimama kuchuana na wanaume kugombea nafasi
ya Mwenyekiti .
Katika
Uchaguzi huo Mwana mama ,Monica Samwely aliibuka mshindi kwa kupata jumla ya kura 111.kati ya kura pigwa 237
nakuwapiga chini Joseph Kidondela aliyepata
kura 78 na Selemani Nyamswa
aliyepata jumla ya kura 48.
Kwa nafasi
ya wajumbe wa mkutano mkuu
wa wataifa, { Uvccm }kulikuwa nawagombea
wanne wawili walishinda ,kati ya hao ni Amri Said,iMhitimu
wa chuo kikuu Tumaini Dsm; na Elilumba Reuben .Wakati katikaJumuiya ya wazazi walioshinda,ni Alberth Makwala ,Monica Samwely na Rehema Mkassa,kati
ya wagombea sita waliojitokeza kugombea nafasi
hiyo.
Katibu wa
chama cha mapinduzi{ CCM} Wilaya ya Iramba
bwn , Mathias Shidagisha Akiongea
na waandishiwa Habari Ofisini kwake leo Asubuhi alisema kuwa Uchaguzi
umefanikiwa kwa Aslimia
95,kutokana na Wajumbe kuhudhuria kwa
wingi ,Ingawa kulikuwa
na shida ya Usafiri mkubwa sehemu
zingine kutokana na jiografia ya wilaya kuwa namabonde pamoja na
milima mikali.
1 comment:
Tunafurahi sana tunapoona habari zianazotolewa na wanahabari wa maeneo husika.Hongereni sana kwa kazi mnayoifanya kwa ajili ya kuwa habarisha Wananchi wa Tanzania.Good work
Post a Comment