Tuesday, December 11, 2012

UJENZI KITUO CHA AFYA ULEMO WAKWAMA


HII NI SEHEMU YA MSINGI KATI MSINGI MKUBWA LA KITUO CHA AFYA CHA ULEMO ULIOKO ENEO LA MSINGIRI UNAO TAKIWA KUBOMOLEWA
Na. Mwandishi wetu Iramba, Singida
Kituo Cha Afya katika kata ya Ulemo Wilayani Iramba Mkoani Singida, kimeshindikana kuendelea kujengwa kutokana na kudaiwa kuwa Ujenzi huo Umesimamishwa na muhandisi wa wilaya.
Ujenzi huo ambao Ulianza 2010 kwa kujengwa msingi ambao hata ulikuwa bado kumalizika,ulisimamishwa haraka na mhandisi kutokana na kukosewa kuchimbwa kwa msingi wake.
HILI NI JENGO LA ZAHANATI YA MISIGIRI ILYOPANDISHWAA HADHI NA KUWA KITUO CHA AFYA KATA YA ULEMO

Standard Radio ilifanya mahojiano na mhandisi wa Ujenzi wa wilaya, Bwana David Malegi kuhusiana na Ujenzi huo,ambapo Alikiri kuwa ni kweli Walisimamisha kuendelea kwa Ujenzi huo kutokana na msingi kuchibwa chini ya kiwango

HILI NI KONTENA LILILOSHEHENI VIFAA LILILOLETWA TANGU MWAKA 2008 NA WASWIDEN IPO HOFU KUWA ZANA ZILIZOKUWA ZIMESHEHENI KATIKA KONTENA HILO HUENDA ZILISHAPORWA NA WAJANJA
Shirika La Kiraia la{ SIKIKA} ambalo makao yake makuu yapo Dodoma, linalo jishughulisha na mambo ya Afya lilitembelea kituo hicho na kujionea lenyewe hali halisi iliyopo katika kituo hicho.
VIONGOZI WA SHIRIKA LA SIKIKA WAKITETA JAMBO KWENYE MSINGI WA KITUO CHA AFYA CHA ULEMO 

Hata hivyo inaelezwa kuwa kukwama huko kunatokana na ushirikiano mdogo wa wananchi na viongozi wao wa kata

No comments: