Monday, December 10, 2012

SINGIDA YAAZIMIA KILA JUMATANO KUWA SIKU YA USAFI

Hili ni Dampo la taka lililopo katikati ya mji wa Singida jirani na soko kuu, pembeni kushoto ni maduka na vibanda vya biashara, eneo hilo linatoa harufu mbaya saa hasa wakati huu wa mvua

SERIKALI wilayani Singida, imeagiza kusimamishwa kwa muda shughuli zote za kijamii kila siku ya jumatano kwa ajili ya kufanya shughuli za usafi wa mazingira ya mji wa manispaa ya Singida, ambao kwa sasa unatajwa kukithiri kwa uchafu ambao ni hatari kwa mazingira na afya ya wananchi

Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya ya Singida, mwalimu Queen Mlozi, wakati akizungumza na watendaji wa ngazi mbalimbali wakiwemo wa vijiji, kata, mitaa na vitongoji katika manispaa ya Singida.

Mwl. Queen Amesema hali ya usafi kwa mji wa Singida ni mbaya, inatisha na inatia aibu kubwa kwa wageni wanaoingia na kutoka, na hata kwa wenyeji wenyewe.


hapa ni sehemu ambapo maji taka na taka nyingine za mitaani hupita katika daraja hili lililoko jirani na Hospitali ya Mkoa wa Singida na kuishia kati
"


Kwa hiyo naagiza kuanzia jumatano ijayo desemba 12 mwaka huu,kuanzaia saa 1.30 hadi saa nne asubuhi,kazi/shughuli zote zitasimama ili kupisha kazi ya kusafisha mji ifanyike", amesema Mlozi.




Hili ni eneo maji yenye takataka mbalimbali yanaposambaa na kuacha uchafu wa kutisha, eneo hili liko barabarani jirani na round about, jirani na Hospitali ya mkoa wa Singida. hakika hali ni mbaya na anachoamua DC mlozi kinastahili kufanyiwa kazi

Aidha Mwalimu Mlozi  amesisitiza kuwa, ni kila mkazi mahali alipo atatakiwa kusafisha na kuondoa kila uchafu katika eneo lakena kwamba siku hiyo na muda huo, ofisi zote za serikali, taasisi, za watu binafsi, mahoteli, maduka na vituo vya kuuzia mafuta,zitasitisha shughuli zao na zitajikita katika kufanya usafi katika maeneo yao.

TUJADILI PAMOJA


kwanni kazi hii isipangwe kufanyika siku za jumamosi, ili kutoa fursa kwa shughuli za maofisini kufanyika bila kusababisha maafisa wengi kujifungia maofisini mwao wakikwepa kuwajibika kufanya usafi na kuwaachia kazi hiyo wananchi wa kawaida wasio na ajira au biashara?
Habari hii imeandikwa na Halima Jamal na picha Zimepigwa na Standard radio FM


No comments: