Thursday, December 6, 2012

GEORGE NANGALE AIPA SOMO TCRA, MFUMO WA DIITALI TANZANIA


 
Mamlaka ya mawasilanao Tanzania imeshauriwa kuhakikisha vituo vyote vya Runinga vya Tanzania vinaonekana Bure katika mfumo wa digitali kupitia katika ving’amuzi vinavyouzwa kwa watanzania

Rai hiyo imetolewa na George Nangale mkurugenzi wa TV Sibuka na Radio Sibuka wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia prof. Makame Mbalawa (MB) na mkurugenzi wa TCRA Prof. John Nkoma kutangaza kuwepo kwa vituo 5 vya TV ambavyo vitaonekana bure baada yakuzima mitambo ya analogia
Picha: Prof Nkoma (Kulia)

Nangale amesisitiza kuwa, kwa sasa TCRA ina Urasimuu ambao umekwamisha vituo vingine tofauti na TBC, ITV, Channel ten, Star TV na EATV kuonekana bure kupitia ving’amuzi vya digitali

Aidha amesisitiza kuwepo na mkakati mahususi wa kuhakikisha elimu zaidi inapelekwa vijijini ili watanzania wote waufahamu mfumo huo mpya wa matangazo ili pia iwasaidie kujipanga kifikra na kiuchumi kununua ving’amuzi vya digitali,

Bw. Nangale amekiri kuwa kwa sasa bado watanzania wengi hawana ufahamu wa kutosha kuhusu uhamisho huo wa analogia kwenda digitali katika mfumo wa matangazo ya Runinga na Radio nchini Tanzania

Baadhi ya vituo ambavyo havimo katika mpango huo wa kuonekana bure ni pamoja na Sibuka, Mlimani TV, Clouds TV, na TV Imani

No comments: