Monday, December 10, 2012

MAJAMBAZI WATEKA MAITI NA KUIPEKUA, MAMILIONI YAPORWA


JESHI la polisi mkoani Sngida,linawashikilia watu 25 kwa tuhuma za kuteka gari la chuo kikuu cha Sokoine (SUA) Morogoro na kisha kupora mali na fedha za watu waliokuwa wanasindikiza maiti mwanafunzi wa chuo hicho kwenda mkoani Mara kwa ajili ya mazishi.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, Linus Sinzumwa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limetokea jumapili desemba 9 eneo la Kisaki katika wilaya ya Singida na kusema kwa sasa majina ya watuhumiwa hao hayawezi kutangazwa hadharani kwa madai kuwa kitendo hicho kinaweza kuathiri shughuli za upelelezi unaoendelea
 
Kamanda Sinzumwa amebainisha kuwa, watekaji hao baada ya kuora mali za wasindikizaji hao, walivunja jeneza na kasha kuupekua mwili wa marehemu Munchari Lyoba mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo cha SUA,
 
Amelitaja gari lililotekwa kuwa ni Toyota land cruiser lenye namba za usajili SU 37012 lililokuwa likiendeshwa na Kalistus Mapulila, na kwamba mali zilizoporwa ni pamoja na nguo za waathirika, kamera, kompyuta aina ya laptop na simu za mkononi ambavyo jeshi la polisi limefanikiwa kuvikamata.

"Vitu vingine tulivyovikamata ni pamoja na vitambulisho vya kazi, charger mbili za simu,kadi aina ya tembo kadi na shilingi 20,500 zizookotwa eneo la tukio", alisema kamanda huyo na kuongeza kuwa mafanikio hayo makubwa, yamechangiwa na ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi
 
Kamanda Sinzumwa ameongeza kuwa watuhumiwa baada ya kugawana shilingi milioni 19.8 walizopora, walianza kunywa pombe ovyo huku wakijitapa kuwa wana uwezo mzuri wa kiuchumi",

 


 

No comments: