Na:Mwandishi wetu
Wilaya ya Iramba mkoani Singida, imekusanya zaidi ya shilingi milioni 377 zikiwa ni makusanyo ya ada za uanachama wa
mfuko wa afya ya jamii (CHF), tangu mfuko huo uanzishwe juni mwaka 1998 hadi
sasa.
Hayo yamesemwa mwishoni mwa
wiki na mkuu wa wilaya hiyo, Yahaya Nawanda, wakati akizungumza na waandishi
wa habari ofisini kwake juu ya maendeleo ya mfuko huo, ambao umekuwa mkombozi
mkubwa kiafya kwa wakazi wa wilaya hiyo.
Amesema kiasi hicho cha fedha, ni ada za wakazi wa kaya 37,710 wa wilaya
hiyo zilizojiunga na mfuko huo ambayo ni
sawa na zaidi ya aslimia 50 za kaya 78,000 za wilaya ya Iramba.
Mkuu huyo wa wilaya, amesema
licha ya fedha hizo kugharamia matibabu kwa wanachama, pia zimetumika katika
kukarabati majengo ya vituo vya huduma za afya na nyumba za kuishi watumishi.
No comments:
Post a Comment