Na Iran Radio
Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi ametoa wito kwa jumuiya ya
kimataifa kuisaidia nchi hiyo katika
juhudi za kupunguza umasikini na changamoto zinazoikabili.
Wito huo ametolewa jana katika ufunguzi wa mkutano wa
ufuatiliaji wa wafadhili wa Burundi ambao unafanyika kwa siku mbili mjini Geneva,
Uswisi.
Aidha Rais huyo amewapongeza washirika kwa uungaji mkono na
kusema kuwa tangu mwaka 2005 nchi ya Burundi imepata maendeleo makubwa katika sekta
mbalimbali, zikiwemo utawala bora, amani na usalama, masuala ya hali ya hewa,
elimu, afya na miundo mbinu.
Ametaja changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi hiyo kuwa ni
pamoja na migogoro ya ardhi, ukuaji
mdogo wa uchumi, utapiamlo, kilimo cha kisasa, ongezeko la kasi la idadi ya
watu, ukosefu wa nishati pamoja na
mabadiliko kwenye sekta ya elimu.
Amesema nchi hiyo inahitaji kusaidiwa kuandaa uchaguzi ulio
huru na wa haki na utakaoshirikisha watu.
No comments:
Post a Comment