Na:Iran Radio
Serikali za Kenya na Nigeria zimekubaliana kupanua wigo wa
ushirikiano katika sekta mbalimbali hususan biashara.
Hayo yamebainika kwenye mkutano kati ya Rais Uhuru Kenyatta
wa Kenya na mwenzake Goodluck Jonathan wa Nigeria mjini Abuja. Viongozi hao
wamesisitiza umuhimu wa kuimarishwa
biashara miongoni mwa nchi za Afrika huku Rais Kenyatta akisema sera za nje za
serikali yake zitazingatia zaidi biashara na nchi za Kiafrika.
Rais Jonathan kwa upande wake amesema bunge la nchi yake
litajadili njia za kupunguza urasimu ili kurahisisha biashara na Kenya. Rais
Kenyatta yuko nchini Nigeria kuhudhuria mkutano maalum wa Umoja wa Afrika wa
kujadili jinsi ya kupunguza maambukizi ya virusi vya HIV na ugonjwa wa Kifua Kikuu
barani Afrika.
Mikataba ya ushirikiano kati ya nchi na nchi, inatarajiwa
kusainiwa wakati marais wa nchi mbalimbali watakapokutana baada ya mkutano huo.
No comments:
Post a Comment