Na Mwandishi wetu
Waziri
Mkuu,
Bw. Mizengo Pinda, amesema tozo ya shilingi elfu moja iliyopitishwa na Bunge kwa matumizi ya simu za
mikononi hailengi kuwaumiza wananchi, bali mapato yake yatakwenda moja kwa moja
kusaidia kueneza umeme vijijini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
kwa vyombo vya habari juzi na Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri Pinda ametoa kauli
hiyowakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara mjini Songea ikiwa ni sehemu
ya ziara yake ya wiki moja katika Mkoa wa Ruvuma, baada ya kuutembelea Mkoa
mpya wa Njombe.
Amesema wanaopinga tozo
hiyo, hawaitakii mema nchi kwani imepitishwa na bunge lililomalizika mwezi
uliopita, ili fedha zitakazopatikana zisaidie katika mpango mkubwa wa kueneza
umeme vijijini unaoendeshwa na Wakala wa Umeme Vijijini, REA. Kwa Mkoa wa
Ruvuma pekee, vijiji vipatavyo 150 vitapatiwa umeme chini ya mpango huo.
Kabla ya mkutano wa
hadhara, Waziri Mkuu alizindua Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi, VETA, cha
Songea kinachodahili zaidi ya wanafunzi 500 na kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa
ufundi stadi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment