Na:Mwandishi wetu
Rais mstaafu, Ali
Hassan Mwinyi, amewataka Watanzania kuzingatia mafundisho ya dini zao ili
kudumisha amani na utulivu nchini.
Rais Mwinyi ametoa rai
hiyo jana wakati akihutubia katika hafla ya kuhitimisha shindano la kusoma
Kurani iliyofanyika katika ukumbi wa viwanja vya Sabasaba, Dar es Salam, ambako
alikuwa mgeni rasmi.
Shindano hilo
liliandaliwa na taasisi ya Al-Hikma Education Centre ya jijini Dar es salaam na
kuwashirikisha vijana wa Kiislamu kutoka katika nchi zote za Jumuiya ya Afrika
Mashariki.
Rais Mwinyi amesema
ili kudumisha amani, utulivu na mshikamano wa taifa ni muhimu kwa vijana na
wananchi kwa ujumla kusoma na kuzingatia mafundisho ya dini zao, na kwamba kwenda
kinyume na mafundisho ya dini kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani kama
ilivyo katika nchi nyingine za Afrika.
Katika shindano hilo
mshindi wa jumla ni Suleiman Omar Ally (10), kutoka taasisi ya Al-Hikma ambaye
amewashinda wenzake tisa na kundi la waliohifadhi juzuu 30, na amezawadiwa shilingi
milioni 10 na zawadi nyingine.
Washindi wengine ni
Abdallah Juma katika kundi la waliohifadhi juzuu 20, na Anwari Yahya amekuwa
mshindi katika kundi la waliohifadhi juzuu 10.
No comments:
Post a Comment