Na. Edilitruda chami
Wananchi
mkoani singida wametakiwa kujifunza mbinu mbadala za kusindika vyakula ili kuvihifadhi kwa
matumizi ya baadae na kuepukana na njaa ambayo inaweza kujitokeza.
Akizungumza
na standard radio meneja wa viwanda vidogovidogo SIDO mkoani Singida Bi. Shoma Kibende amesema endapo
wananchi watatumia mbinu za kuhifadhi vyakula na hata kufungasha kwa
njia ambayo ni salama hapatakuwepo na upungufu wa vyakula.
Amesema
mkoa wa Singida unazalisha vyakula vingi kama vile nyanya, matunda, mbogamboga, karanga lakini vinaharibika mapema kutokana na watu
kutojua njia sahihi za kuhifadhi vyakula kwa matumizi ya baadaye.
Aidha, amesema Sido ina mpango wa kuhakikisha mwananchi anajikita katika shughuli za kijasiriamali kwa kutoa mafunzo mbalimbali ili kuongeza kipato chao binafsi na kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali pamoja na kujifunza mbinu za usindikaji.
Jumla ya
viwanda 76 vimefikiwa na SIDO katika kutoa mafunzo ya ujasiriamali na
usindikaji bora wa vyakula na matunda, kama njia pekee ya kutokomeza njaa kwa
siku za baadae
No comments:
Post a Comment