Na:Iran Radio
Habari kutoka Ufaransa zinasema, Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria
amerejea nchini kwake baada ya kupata matibabu nchini Ufaransa.
Habari zinasema kuwa, Rais Bouteflika ameondoka nchini Ufaransa jana
kuelekea nchini kwake. Rais huyo mwenye umri wa miaka 76 alipelekwa nchini
Ufaransa baada ya kukumbwa na ugonjwa wa kiharusi mwishoni wa mwezi Februari
ambapo awali alilazwa katika hospitali ya kijeshi ya Valde Grace na kupelekwa
katika hospitali nyingine ya mjini Paris, Ufaransa.
Kutokuwepo kwake kisiasa nchini Algeria, kuliibua maswali mengi hasa
kuhusiana na nafasi ya uraisi nchini humo. Hali hiyo ilivifanya vyama na
makundi ya kisiasa yanayoipinga serikali inayoongozwa na Rais Abdelaziz
Bouteflika wa Algeria, vilitaka kufanyika uchaguzi kabla ya wakati kwa mujibu
wa katiba ya nchi hiyo, kutokana na kuugua rais huyo.
No comments:
Post a Comment