Na:Iran radio
Rais Joyce Banda wa Malawi amesema
kuwa nchi yake haina nia ya kulegeza kamba katika mgogoro wa mpaka wa Ziwa
Nyasa na Tanzania.
Kiongozi huyo ametoa msimamo huo
baada ya kukutana na marais wa zamani Bw. Joachim Chissano wa Msumbiji na Bw. Thabo
Mbeki wa Afrika Kusini ambao ni wajumbe maalum wa jumuiya ya SADC katika
mgogoro huo.
Rais Joyce Banda amesema madai ya
Tanzania kwamba inamiliki sehemu fulani ya Ziwa Nyasa si ya kweli na kwamba
mpaka uko ufukweni mwa ziwa hilo.
Amesema nchi yake inafuatilia kwa
karibu upatanishi wa SADC na kwamba isiporidhishwa na maamuzi ya jumuiya hiyo
italiwasilisha suala hilo mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu ICJ.
Joachim Chissano na Thabo Mbeki
wanatarajiwa kuelekea Tanzania na kukutana na Rais Jakaya Kikwete ili kujadili mgogoro.
Tanzania inasisitiza kwamba mpaka wake na Malawi uko ndani kabisa ya Ziwa
Nyasa.
No comments:
Post a Comment